MUNGU
akubariki rafiki popote ulipo na karibu katika somo hili ambalo tunajifunza
kwamba ‘’KWANINI INJILI INAHUBIRIWA?
-Injili ni
habari njema za ufalme wa MUNGU ambao umeletwa kwa wanadamu na BWANA YESU KRISTO
.
-Injili ni
mpango wa MUNGU wa kuwaokoa wanadamu kutoka mikononi mwa shetani.
Injili ni
habari za uzima wa milele ambao unapatikana katika YESU KRISTO pekee(Yohana
14:6 , Matendo 4:12).
Mwanzo wa
injili ndio mwanzo wa miaka pia maana kama mwaka huu ni 2013 basi maana ni
miaka 2013 tangu BWANA YESU alete habari njema za ufalme wa MUNGU yaani INJILI.
Tukizungumzia
injili tunazungumzia habari njema za za pekee za kwenda uzima wa milele. Na
kama tutataka tuijue injili basi inapatikana pekee makanisani au kwenye semina
za kiroho na kwenye mikutano ya injili
na chanzo chke ni BIBLIA TAKATIFU na sio kwingine popote. Zile injili ambazo
ziko nje na BIBLIA ni injili za uongo ambazo shetani ndio alizileta kupitia
WAPINGA INJILI YA KWELI yaani WAPINGA KRISTO ambao wanamtumikia shetani na
hawataki kuja kwenye nuru ya ulimwengu yaani kwa BWANA YESU.
ZIFUATAZO NI
SABABU 4 ZA INJILI KUHUBIRIWA KATIKA ULIMWENGU WOTE.
1; KUTII AGIZO LA BWANA YESU.
Marko
16:15-16(Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.
).
Mapenzi ya
YESU ni kwamba tutoke na kuwaendea watu ili HABARI NJEMA iwafikie.
Warumi
10:13-14(kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la BWANA ataokoka.
Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?
).
Ndugu
nimetumwa kwako na yeye na yeye anayejua maisha yako hadi mauti yako, ambaye
anataka umpe yeye maisha yako ili awe BWANA na MWOKOZI wa maisha yako maana nje
na yeye hakuna mwanadamu yeyote kupata uzima wa milele,(Yohana 14:6, Matendo
4:12). Hivyo kama tunataka uzima wa milele lazima tu tumfuate BWANA YESU na
yeye yuko kwenye injili yake yaani kwenye BIBLIA.
2; MUNGU
ANATHAMINI NAFSI YA MWANADAMU KULIKO VYOTE.
Yohana 3:16( Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda
ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee,
bali awe na uzima wa milele.
).
Ndugu
ulimwengu ni wewe hivyo MUNGU anataka uokolewe..
2 Kor 5:19 (yaani, MUNGU alikuwa ndani ya KRISTO, akiupatanisha ulimwengu na nafsi
yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la
upatanisho.
)
3; KUNA
KUZIMU NA MATESO YA MILELE.
Ufunuo
20:11( Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake;
ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.
).
Injili
inahubiriwa ili kwamba hata kama kuna mwanadamu ataenda kuzimu basi aende kwa
kutaka yeye ila maonyo kutoka kwa MUNGU kupitia neno lake ambalo injili ni sehemu
yake aliyapata.
Ndugu penda
injili na penda kujiunga na watu wengine kanisani ili kujifunza na kulijua
kusudi la MUNGU la uzima wa milele.
4; INJILI
HULETA WOKOVU.
Warumi 1:16.(Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa MUNGU uuletao
wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi(wa nyumbani kwako) kwanza, na kwa Myunani(watu wa nje) pia.
)
Waebrania
2:3.(sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao
kwanza ulinenwa na BWANA, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;
)
-Ndugu
Tafuta injili nawe utapona maana injili inaleta badiliko.
-Ingia kwa
YESU na dhambi yako itakoma.
- Wokovu ni
hatua ya kwanza na kuukulia wokovu ni hatua inayofuata hivyo mpendwa wangu
penda kuhudhuria mafundisha kanisani.
-‘’KUMBUKA
UKIPENDA IBAADA UTAKUWA UNAMPENDA MUNGU’’
MUNGU
anakupenda sana ndugu ndio maana alimtuma BWANA YESU KRISTO ili wewe uwe na
uzima sasa kisha uzima wa milele katika yeye.
-
Ndugu
injili ya kweli inaambatana na miujiza,
uponyaji, kufunguliwa na kuwaweka watu huru kutoka kila pando la shetani, hivyo
nenda kanisa ni utapona na pia utajifunza neno la MUNGU.
MUNGU akubariki sana na kama bado hujaokoka , ndugu chukua hatua hiyo leo
na jina lako litaandikwa kwenye kitabu cha uzima, endelea na mafundisho na
maombi na utamwona MUNGU kwa kila hatua ya maisha yako.
AMEN.
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula.
Maisha ya ushindi Ministry.

Comments