Maisha ya ushindi ni nini?



Peter Michael Mabula
Maisha ya ushindi Ministry


-Maisha ya ushindi ni hali ya mtu kuishi pasipo kutatizwa na jambo lolote.
-Maisha ya ushindi ni maisha wanayoishi watu waliookoka ambao MUNGU yumo ndani yao.

-Tuna sababu za kuishi maisha ya ushindi kwa sababu YESU mwenyewe alishinda. Ufunuo 1:8 (
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi. )



Ili uishi maisha ya ushindi ni lazima uwe na upendo.

a:MUNGU alitupenda kwanza sisi hivyo tabia ya MUNGU ni upendo. Yohana 3:16(
Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. ) 

 pia 
Warumi 8:37-39 ( Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa MUNGU ulio katika KRISTO YESU BWANA wetu. ) 
 
b:Upendo wetu kwa MUNGU. Mithali 8:17(
Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.)

c: Upendo wetu kwa wengine. 1Kor 13:1-8(
Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.  Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.  Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;  haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;  huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika. )

 ULI UWE UNAISHI MAISHA YA USHINDI LAZIMA HAYA YATOKEE KWAKO.

1: Ulinzi wa MUNGU 1 Samweli 2:9-10(
eye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda; Washindanao na Bwana watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; Bwana ataihukumu miisho ya dunia; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake. )
 
2: Kuepuka majaribu. Waebrania 4:14-16(
Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.
  Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji. )


3:Kushinda dhambi na tamaa.        2 Timotheo 2:22( Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi. )
 
4:Kuenenda nuruni 1 Yohana 1:7(
bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake YESU, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote. )

5: Kuwa na mamlaka Yakobo 4:7(
Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.)

6: Ujazo wa neno la MUNGU moyoni mwako.Yohana 8:31(
Basi YESU akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru. )
MUNGU awabariki sana na kama hujampa BWANA YESU maisha yako nafasi ya kufanya hivyo ni leo maana hakuna mwanadamu ajuaye kesho yake maana bila YESU KRISTO hakuna uzima wa milele hivyo ndugu kumpa YESU KRISTO maisha yako ndilo jambo muhimu kuliko yote maishani mwako, fanya hivyo na jina lako litaandikwa mbinguni kwenye kitabu cha uzima pia baada ya hapo shirikiana na wana kanisa wengine katika mafundisho ya neno la MUNGU na utabarikiwa sana.
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula
Maisha ya ushindi Ministry

Comments