Na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima-Moshi; Gwandu Mwangasa
2 Palikuwa na mtu mmoja wa Sora, wa jamaa ya
Wadani; jina lake akiitwa Manoa; na mkewe alikuwa tasa, hakuzaa watoto.
3 Malaika wa Bwana
akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini
utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume.
4 Basi sasa, jihadhari,
nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi;
5 kwani tazama, utachukua
mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake;
maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa
Israeli na mikono ya Wafilisti.
Waamuzi 16:21-28
21
Wafilisti wakamkamata, wakamng'oa macho; wakatelemka naye mpaka Gaza,
wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza.
22 Lakini zile nywele za
kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa kwake.
23 Kisha wakuu wa Wafilisti
wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana
walisema, Mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi mwetu.
24 Na hao watu walipomwona
wakamhimidi mungu wao, maana walisema, Mungu wetu amemtia mikononi mwetu huyu
adui wetu, aliyeiharibu nchi yetu na kuwaua watu wengi miongoni mwetu.
25 Ikawa mioyo yao
iliposhangilia, wakasema, Mwiteni Samsoni, ili atufanyie michezo. Basi
wakamwita Samsoni atoke gerezani, akacheze mbele yao wakamweka katikati ya
nguzo mbili.
26 Samsoni akamwambia yule
kijana aliyemshika mkono, Niache nizipapase nguzo ambazo nyumba hii inazikalia,
nipate kuzitegemea.
27 Basi nyumba ile ilikuwa
imejaa watu waume kwa wake; na wakuu wote wa Wafilisti walikuwamo humo, na juu
ya dari palikuwa na watu elfu tatu waume kwa wake waliokuwa wakitazama, wakati
Samsoni alipocheza.
28 Samsoni akamwita Bwana,
akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara
hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya
macho yangu mawili.
Habari
hii ni ndefu sana lakini tumesoma vipande hivi viwili lakini ninaomba
nikusimulie ujue jinsi ilivyokuwa; kuna wakati wana wa Israel walifanya makosa
mbele za Bwana na hivyo Mungu akawaacha wakawa mateka kwa Wafilisti na
wafilisti wakawatawala,sasa wakati wakiwa wametawaliwa na Wafilisti,Mungu
akaona anastahili kutafuta njia ya namna ya kuwatoa watu wake katika utumwa wa
wafilisti,sasa katika Israel kulikuwa kuna mwanamke ambaye ni mke wa mzee mmoja
aliyejulikana kwa jina la Manoa.Mama huyu alikuwa hajapata mtoto kwa muda mrefu
sana,mimi nataka nikwambie ndugu yangu usimcheke wala kumdhihaki mtu ambaye
hajapata mtoto maana hujui kwenye tumbo lake amebeba nini.Sasa watu wakawa wanamwita
Yule mama kuwa tasa,mana kama ilivyo
kawaida ya wanadamu huwa wanamwita mtu kwa tatizo lake hivyo tatizo linakuzwa
na kuwa kubwa na baadae linachukua jina lako na badala hilo tatizo ndio
linakuwa jina lakeKwa kawaida huwa wanadamu tatizo likionekana kwa Macho huwa
linakuzwa na kuwa utambulisho wako,ila mimi nataka nikwambie usiogope wanadamu
wamekuitaje Mungu aweza kukuita kwa jina lingine tofauti na wanadamu
wanavyokuita hivyo wewe hutakuwa kama wanadamu wanavyokuita bali utakuwa kama
Mungu anavyokuita .
Kwa hiyo
wakati Yule mama pale mtaani wanamwita tasa,Mungu alikuwa na mpango na Yule
mama.Mungu akamtuma malaika akamwambie Yule mama kuwa atapata mimba na atazaaa mtoto
wa kiume ambaye ni mnadhiri wa bwana hivyo asinywe kileo chochote wala asile
chochote kilicho najisi na mtoto atakayezaliwa wembe usipite kichwani
mwake.Baadae Yule mtoto akazaliwa na akakuwa akiwa hajawahi kunyolewa nywele,Biblia
inasema kijana Yule aliua samba,habari hii ni ndefu sana lakini hapa
namuongelea Samson.Samson baadae akamuoa Delila ambaye ndiye huyu mwanamke
aliyemsaliti Samson.
Nataka
nikwambie maisha waliyoishi wana wa Israel ni sura ya kanisa ya leo lakini nina
habari njema leo ya kwamba “nywele” za kanisa zimeanza kuota tena maana kanisa
lilinyolewa nywele likaondolewa nguvu lakini sasa nywele zimeanza kuota tena.
Comments