![]() |
Na Mwl C. Mwakasege |
Kuna uhusiano gaini kati ya Mungu na mali?
Kuna uhusiano gaini kati ya mkristo na mali?
Kuna uhusiano gaini kati ya wokovu na mali?
Je, nidhambi kwa mkristo kuwa na mali nyingi?
Hebu na tuangalie maneno ya yesu kristo juu ya Mungu na mali.
“Hakuna
mtu awezaye kutumikia mabwana wawili, kwa maana hatamchukia huyu, Na
kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwenzi
Kumtumikia Mungu na mali’’ (mathayo 6:24)
Neno
la kingereza lililotafasiliwana kuandikwa ‘MALI’ ni ‘MAMMON’ na hili
‘mammon’ ni jina la roho ya bilisi anayotawala mali. Kwa maneno mengine
naweza kusema kuwa ‘mammon’ ni jina la pepo.
Kwahiyo,
neon ‘mali’ neon mali lilivyotumika hapa linamaanisha ‘pepo linaloitwa
pepo mali’ ndiyo maana yesu kristo alisema “hakuna mtu awezaye kutumikia
MABWANA wawili…” Yesu kristo asingeliita mali kuwa nimojawapo ya
MABWANA kama hakuwa juu ya roho inayo itwa mali. Roho hii ya shetani
iitwayo mali imefanya watu wengi, hata wakristo waache kumtumikia Mungu
aliye hai, na badalayake waitumikie roho inayowasukuma na kuwatamanisha
juu ya mali, ili waitumie kwa uchoyo na ubinafsi.
Wakristo wngine wanadhani wanaweza kumtumikia Mungu na vile vile
kummtumiakia mali. Yesu kristo alisema; “HAKUNA mtu awezaye kutumikia
mabwana wawili; kwa maana ATAMCHUKIA HUYU, NA KUMPENDA HUYU; AMA
ATASHIKAMANA NA HUYU, NA KUMDHARAU HUYU. Hamwenzi kumtumikia Mungu na
mali.”
Kwakusema
hivi akuwa anamaanisha kuwa na vitu vinavyo itwa mali si vibaya. Kitu
anachosema ni kibaya ni KUITUMIKIA MALI! Bibilia inasema katika Zaburi
24:1 kuwa, “Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana; Dunia na wote
wakaao ndani yake .”
Mtu
hakuumbwa ili aitumikie mali. Mtu aliumbwa kwa ajili ya utukufu wa
Mungu na amtumikie yeye peke yake. Mali ya dunia iliwekwa kwa ajili ya
kumtukia mtu, na siyo mtu aitumikie mali! Mtu aliwekwa juu ya mali yote
na aliingizwa kuitawala (Mwanzo 1:28 – 30).
Kuwa
na mali siyo vibaya, wala siyo dhambi. Mali inakuwa kikwazo katika
maisha ya mkristo inapoaza kumfanya mtu amsahau Mungu na mapenzi yake.
Ndiyo maana Yesu kristo alisema “ kwa shida gani wenye mali watauingia
ufalme wa Mungu” (Luka 18:24) siyo kwamba huwezi kuingia ufalme wa
Mungu. Bali kwa shida wenye mali watauingia ufalme wa mungu. Kwa maneno
mengine ni kwamba wakimtanguliza na kumtumikia Mungu, mali haita kuwa
kwazo katika maisha yao ya ukristo.
Sasa tuishije katika ushauri wa namna hii?
“Kwa
namna hiyo nawaambieni, msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe
nini; wala miili yenu, mvae nini maisha je! Si zaidi ya chakula, na
mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa angani, yakwamba hawa pandi,
wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na baba yenu wa mbinguni
huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? NI YUPI KWENU AMBAYE
AKIJISUMBUA AWEZA KUJIONGEZA KIMO CHAKE MKONO MMOJA? Namavazi ya nini
kuyasumbukia? fikirini maua ya shambani jinsi yameavyo, hayafanyi kazi
wala hayasokoti, nami nawaambieni hata sulemani katika fahari yake yote
hakuvikwa vizuri kama mojawapo yahayo, basi ikiwa mungu huyauvika hivi
majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa karibuni,
JE!HATAZIDISANA KUWAVIKA NINYI, ENYI WA IMANI HABA?. Msisumbuke basi,
mkisema, tule nini? au tunywe nini? au tuvae nini? Kwa maana haya yote
mataifa huyatafuta, kwa sababu baba yenu wa mbinguni anajua mnahitaji
hayo yote.{matayo 6;25-32}
Kuna
wakristo wengi wameyaelewa vibaya maneno ya Bwana YESU kristo hata
kufikia kutokufanya kazi kwa kisingizio cha kwamba Yesu kristo alisema
tusiyasumbukie maisha. Kwao kufanya kazi ina maana kusumbukia maisha.
Lakini napenda kuwaambia yakua Yesu kristo hakua namaana yakutuambia
tusifannye kazi aliposema tusiyasumbukie maisha.
Nadhani
unaamini kuwa ni Roho wa kristo aliyemuongoza mtume PAULO kuwaandikia
wathesolenike juu yamashauri mbalimbali ya kikristo
katika1Wathesolenike3;10b anasema,”ikiwa mtu hataki kufanya
kazi,basi,asile chakula’ Nimuhimu kufanya kazi. Kufanya kazi sio
kusumbuka na maisha na Kusumbuka na maisha sio kufanya kazi.
Jambo
ambalo Bwana Yesu alitaka tufahamu wakati alipokua akisema
tusiyasumbukie maisha nikwamba katika kila jambo tumshirikishe Mungu na
kumtanguliza yeye. Wakiristo wengi wanadhani wanaweza kula, kunywa na
kuvaa bila msaada wa Mungu.Yesu kristo alisema katika Yohana15:5b kuwa;
‘…..maana pasipo mimi ninyi hamuwezi kufanya neno lolote’’{HILI NIPAMOJA
NA KULA NA KUVAA} ndio maana katika wakilipi4:13 imeandikwa
kuwa”nayaweza mambo yote katika YEYE anitiaye nguvu” Yesu kristo ndiye
atutiate nguvu.
Yesu kristo alitoa muongozo mzuri sana wa jinsi ya kuishi hapa ulimwenguni alisema;
Bali utafuteni KWANZA ufalme wake,na haki yake,na hayo yote mtazidishiwa”{mathayo 6;33}
Ukiyaangalia
maisha ya watu wengi utadhani Yesu kristo alisema”bali utafuteni kwanza
ufalme wake, na haki yake, na hayo yote MTAONDOLEWA” Inahuzunisha kuona
watu wengi wakiokoka maisha yao yanageuka kuwa duni, wanashindwa kula
vizuri wala kuvaa vizuri.
Ngoja
nirudie kusema SI MAPENZI YA MUNGU UWE MASIKINI. SI MAPENZI YA MUNGU
TUKOSE CHAKULA WALA MAVAZI. Ni Mungu yupi ambaye atawapenda ndege
akiawavika na kuwalisha, nakuacha watoto wake aliowaumba kwa mfano wake
wakose chakula na mavazi?. MUNGU wetu tunayemuabudu na kumtumikia katika
kristo Yesu,anapenda tuishi maisha mazuri, tule na kuvaa
vizuri.Tunachotakiwa kufanya nikuutafuta kwanza ufalume wake,na haki
yake, na hayo yoye{chakula na mavazi}TUTAZIDISHIWA na sio TUTAONDOLEWA.
Ukiona
mtu anasema ameokoka halafu anajikuta amekosa chakula na mavazi, huku
anafanya kazi,basi ujue anafanya kazi na kukusanya vitu hivyo pasipo
Bwana kwa kuwa asiye kusanya pamoja na Bwana hutapanya.
Source: Mwl C. Mwakasege
Comments