ROHO MTAKATIFU YUPO HALISI KUKUSAIDIA.

na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


Tunasoma;
Mwanzo 1 :1-3

'' Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.’’

Bwana Yesu asifiwe…
Haleluya…

Biblia inatueleza vizuri kabisa katika lugha ya kueleweka kwa habari ya uumbaji wake BWANA MUNGU.
Alipoziumba mbingu na nchi Biblia inasema yakuwa nchi ilikuwa UKIWA,tena UTUPU,kisha GIZA lilikuwepo.

Kumbe giza lilikuwepo hapo awali likitanda juu ya uso wa maji.
Nchi ilipokuwa ukiwa na utupu,
Giza hapo lilitanda juu.
Tabia mojawapo ya giza ni sehemu yenye UKIWA na UTUPU.
Katika maisha ya leo unapokuwa na UKIWA na hali ya UTUPU ujue huyu giza yupo hapo,yaani anapatikana maeneo hayo.

Hali ya UKIWA ni sawa na lugha ya kiingereza ambayo ni ‘’ Without form’’
Pamoja na neno UTUPU=Empty waste’’

Sasa pata picha hapo,
Kwamba ukikwa ni mkiwa ni sawa na kuwa ‘’Without form,na pia UTUPU unakuwa Empty waste

Ok,
Sasa siki hili,
Ukiwa na Utupu huleta giza,
Lakini dawa ya giza ni NENO LA BWANA ambalo kwa hilo limevuviwa na Roho mtakatifu.

Tumesoma hapo juu,kwamba pale palipokuwa na UKIWA na UTUPU,BWANA MUNGU akatamka NENO ambalo kwa hilo Roho mtakatifu ndio muwajibikaji.

Mungu akasema; IWE NURU ;NURU IKAWA.

Katika maisha yetu ya kila siku,ikiwa giza lipo nasi yatupasa kutamka neno kwamba IWE HIVI…
Mazingira yanatakiwa yatusikilize sisi na sio sisi tuyasikilize mazingira kwamba yanasemaji.

Tazama hapo mwanzo,mazingira yalikuwa ni UTUPU na UKIWA na GIZA pia,Bali MUNGU akatamka IWE NURU,NAYO IKAWA.
Uwezo ule wa kutamka na ikawa leo hii upo ndani yetu kwa msaada wa ROHO MTAKATIFU Yeye akiwa kazini muda wote.

Nasema Roho mtakatifu yupo kukusaidia katika KUTAMKA
Kwamba IWE NURU nayo itakuwa kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareti.

Kati ya jambo baya kwa mtu sio kifo,
Wala sio ajali,
Wala sio kukosa nyumba,Watoto,Mume/Mke,
BALI NI KUISHI MAISHA YA GIZA.

Nasema na wewe mpendwa,OGOPA MAISHA YA GIZA.maisha ya giza ni hatari,
ni maisha yaliojaa dhambi.Mdhambi yoyote nyumba yake ni GIZA.
Tazama;
Mungu mwenyewe amelitambua hilo,akaumba kitu cha kwanza kabisa NURU alijua siri hii,
kwamba ni hafadhali hukose nyumba,na vinginevyo vote,tena afadhali watu wakudhalau Lakini uweze kuishi maisha ya NURUNI.

Haleluya…
Jina la Bwana libarikiwe sana…

Giza halihiwezi NURU hata siku moja,
Palipo na Giza,Nuru ijapo ,giza hukimbia.
Yeye ambaye amedhamilia kujikana kabisa na kuamua kutembea nuruni,
yajapo mambo ya giza yoyote yale ni lazima yakimbie mbele yake.

Roho mtakatifu yupo kukusaidia,
Biblia inasema ;
‘’Roho ya Mungu IKATULIA…’’
Sikia Yeye yupo ,AMETULIA tu.
Nasema yupo halisi,akisubiri umuite aje na kukusaidia.

Mpango wa Mungu kwetu sisi ni kuishi maisha ya utakatifu ambayo ni maisha ya nuruni.
Kamwe hatuwezi sisi wenyewe kuishi maisha hayo ya NURUNI kwa kutumia akili zetu,
na ndio maana tunamuhitaji Roho mtakatifu sana kuliko hata vile tunavyodhania.

Roho Mtakatifu ametulia…Nasema ametulia tu… Aaaha! Haleluya…

Kutulia maana yake yupo,hai halisi,naye yupo kazini anaweza kushuka pale tu tutakapo muhitaji…

UBARIKIWE.

Comments