SIRI KATIKA UTOAJI

Mwl. Sospeter Simon Ndabagoye/ New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.

Mungu Humjaribu Mtu Kupitia Utoaji, Pia Mtu Ameruhusiwa Kumjaribu Mungu Kupitia Matoleo Japo Imeandikwa “Mtu ajaribiwapo, asiseme,Ninajaribiwa na Mungu;Maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu (Yakobo 1:13) ” pia imeandikwa, usimjaribu Bwana Mungu wako, ila hapa kasema, Nijaribuni kwa kunitolea ili muone kama sitawafungulia madirisha ya Mbinguni (Malaki 3:11)
Izingatiwe kuwa; Mungu si masikini, wala Mungu si ombaomba hata ahitaji msaada kutoka kwa binadamu. Mungu hashindwi na lolote. (Mwanzo 18:14) “Kuna neno gani gumu la kumshinda Bwana?..”
Usiwe na kiburi wewe mwanadamu na kujisifu kwaajili ya matoleo yako.(Obadia 1:3-4). Kiburi cha moyo wako kinakudanganya ,Wewe ukaaye katika pango za majabali, mwenye makao yako juu sana. Asemaye moyoni, ninani atakayenishusha mimi?.....Nitakushusha kutoka huko,asema Bwana.
Neno la Mungu linasema “Fedha ni mali yangu,na dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa majeshi” (Hagai 2 :8). Hivyo, ni dhahiri kuwa, mali tulizonazo ni sehemu ndogo tu, aliyotujalia Mungu kuwa nayo. Na kwa kuwa Mungu,katubariki,tunapaswa kuleta nyumbani mwake kama shukrani ya kile alichotupatia. Hii ina maana kwamba, inamaana kwamba, unatonesha kumfahamu aliyekupa,hivyo unakuja kumshukuru.
Kwanini utoaji?
Kwanza kabisa, Mungu mwenyewe kaagiza watu kutoa ili chakula kisije kikapungua nyumbani mwake.
(Kum. 12: 6-7)
“Pelekeni huko sadaka zenu za kuteketezwa , na dhabihu zenu na zaka zenu na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhuri zenu na sadaka zenu za hiari na wazawa wa kwanza wa makundi yenu ya ng’ombe na ya kondoo 7na huko mtakula mbele za Bwana Mungu wenu, nanyi furahuni katika yote mtakayotia mikono yenu, ninyi na nyumba ni mwenu aliyobariki Bwana Mungu wako.17 usile ndani ya malango yako zaka ya nafaka zako,wala ya divai yako ,wala ya mafuta yako wala wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng’ombe, na ya kondoo, wala nadhiri zako uwekazo zote ,wala sadaka zako za hiari ,wala sadaka ya kuinuliwa ya mkono wako”
Tena anakumbusha kuwa, 22 “Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shambani mwaka baada ya mwaka. 23Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapopachagua apakalishe jina lake,zaka ya nafaka zako na divai yako,na mafuta yako na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng’ombe na ya kondoo; ili upatekujifunza kumcha Bwana Mungu wako daima” (Kum. 14:22-23)
(Nehemia 10:37) “tena tuyalete malimbuko ya unga wetu,na sadaka zetu za kuinuliwa , na matunda ya miti ya namna zote,mvinyo na mafuta , kwa makuhani, hapo vyumbani kwa nyumba ya Mungu wetu,na zaka zetu za ardhi yetu kwa walawi kwa kuwa Walawi wazitwaa zaka mijini mwote mwa kulima kwetu”
Hata Yesu mwenyewe ni mtoaji, hivyo sisi kama wafuasi wake,tunapaswa kumuenzi kwa kufanya yote aliyofanya alipokuwa hapa duniani. (Mathayo 17:24-27). Pia Yesu,hakusita kuwapa wahitaji mahitaji yao.Kumbuka alivyowapa chakula mkutano wafatao elfu tano. Lakini pia,tunamuenzi Mungu mwenyewe aliyemtoa mwanae wa pekee kwaajili yetu wote,afe msalabani,kifo cha aibu,kifo cha laana kwaajili ya dhambi zetu.
Pili, tunatoa ili kupata baraka za Mungu.
Hii ndiyo sehemu pekee ambayo Mungu amemruhusu mwanadamu amjaribu. Kumbuka, neno li wazi likisema, usimjaribu Bwana Mungu wako, lakini katika matoleo ameruhusu kumjaribu, hii ni ishara kuwa Mungu anayaheshimu matoleo ya kila mtu,yaletwayo kwa shukrani, sala na uaminifu
“Leteni zaka kamili, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi mjue kama sutawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni Baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha au la. 11Nami kwaajili yenu,nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba , asema Bwana wa majeshi” (Malaki 3:10)
Tatu, kuonesha utiifu kwa Mungu.
(Mithali 3:9) “Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote. 10ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, na mashinikizo yako yatafurika divai mpya”
Hakika kumtii Mungu ni zaidi ya sadaka. Na hapa nataka nikwambie kuwa kuitii sauti ya Mungu, huleta baraka, amani na uzima wa milele; kumbuka Mungu alivyombariki Ibrahimu na uzao wake wote kupitia utiifu wake. (Mwanzo 22:1-14). Na pia sadaka au thabihu utoayo yote kama haitalitii neno la Mungu ni bure (1Samweli 15:22) (Mithali 21:3, Isaya 1:11, Amosi 5:22, Mathayo 9:13,12:7).
Nne, Kupitia matoleo ya sadaka zetu, Tunaweza kupata maono
Kornelio alipata maono kupitia wingi wa sadaka na sala zake alizofanya kila mara(Matendo 10:1- ).Kadharika, Ibrahimu, alipata maono mara nyingi kwa kuwa mtiifu katika kutoa sadaka zake na kuyafuata maagizo ya Mungu.

Je, matoleo haya yatolewe kwa nani?
Mungu amewaweka makuhani wanaomwakilisha hapa duniani kwa kufanya kazi yake kwa sura na mwonekano wa kibinadamu ambao Mungu mwenyewe huwatumia kufanya mambo mbalimbali kadri Roho mwenyewe anavyowajilia.
1Nyakati 26:20 Na katika Walawi, Ahia alikuwa juu ya hazina za nyumba ya Mungu na juu ya hazina ya vitu vilivyowekwa wakfu.
Hesabu 18: 21 Na wana wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa Urithi wao, badala ya huo utumishi wautumikao, maana, ni huo utumishi wa hema ya kukutania.
Nehemia 13:11 ndipo nikagombana na mashehe, nikasema, mbona nyumba ya Mungu imeachwa? Kisha nikawakusanya, nikawaweka mahali pao 12ndipo Yuda wote walipoleta zaka za nafaka, na mvinyo na mafuta kwenye hazina.
Hawa ndio wasimamizi wa matoleo haya, ambayo watu humtolea Mungu kama shukrani na sadaka zao kwa Bwana.
Tena, watu hawa wanapaswa kuwafundisha waumini namna ya kutoa ili wasije wakapa laana kwa kutomtolea BWANA, au kupata laana kwa kumdanganya roho wa Mungu kwa kutokuwa waaminifu yaani kuwa wezi. (Matendo 5:1-10).
Law 27:30-31 Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi au kama ni matunda ya nchi, ni ya Bwana ni takatifu kwa Bwana.Na mtu akitaka kukomboa chochote cha zaka yake,ataongeza sehemu yake ya tano juu yake.(Mwanzo 28:22)Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu ; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea sehemu ya kumi.
Hitimisho.
Mungu ameliweka neno lake katika matoleo, na yeyote atoaje basi huyo anapanda, na yule atoaye zaidi humkopesha Mungu, hata hivyo izingatiwe kuwa kuwasaidia wahitaji kama yatima wajane na masikini ndiyo ibada iliyopata kibali machoni pa Mungu hivyo kila mtu anapaswa kuwa na bidii katika kuwasaidia. Neno linasema, mwenye jicho la ukarimu atabarikiwa maana huwapa masikini chakula chake, (Mithali 22:9) lakini azibaye masikio yake asisikie kilio cha masikini, yeye mwenyewe atalia, lakini hatasikiwa (Mithali 21:13). Lakini Mungu anasema, hatazisahau sadaka zako hata siku ya kufa kwako, angalia Mungu alivyokumbuka sadaka za Thabita hata akabatilisha kifo chake (Matendo 9:36-40).
KUMBUKA MUNGU MWENYEWE,ILI KUUTHIBITISHA UPENDO WAKE KWETU,ALIMTOA MWANAWE WA PEKEE ILI AFE KWAAJILI YETU. JE WEWE UMEMTOLEA NINI?
Mungu awabariki na kuwapa Ulinzi daima. Akupeni uwezo wa kuizishinda njia zote za adui, na mipango yote ya kipepo iwe chini ya nyayo zako. Amen

Mwl. Sospeter Simon Ndabagoye/ New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.
Kwa Mobile +255(0)7 (57/84) 464 141/ 12 909 021.
Au Email sos.sesi@yahoo.com / newelshaddai@gmail.com

Tunakushauri, utembelee kanisa la kiroho lililo jirani yako, kwaajili ya mafundisho zaidi na Ushirika. (Kumbukumbu la Torati 28:6).

Comments