TOBA

RGP Mbogo
0655 445525.

Toba-ni hali ya unyenyekevu, ya kumwendea Mungu na kuwa muwazi kwake.
Ni kumwomba Mungu msamaha kwa makosa na dhambi zako.
Kutubu-ni hali ya unyenyekevu(tendo la unyenyekevu) anayokuwa nayo mtu ili kuomba msamaha.
tunaomba msamaha ili tuupate.Ukiupata msamaha umeokoka na laana ya dhambi.Toba ni unyenyekevu kwahiyo unapokuwa unatubu unamaanisha kujutia kosa ulilolitenda.
Zaburi 51:1-11
napenda tumtafakari mtumishi wa Mungu Daudi.Daudi aliomba msamaha kwasababu aliletewa ujumbe na mtumishi wa Mungu Nathani.
Daudi alifanyakosa sana kwa kumwua Uria kisa kikubwa ni kumpenda mke Wa Uria.
sasa kabla sijaendelea nataka msomaji uelewe tofauti kati ya dhambi na kosa.
Dhambi hutangulia tena hauwezi kuiona hukaa ndani ya mtu kwa lugha nyingine dhambi ni roho.Pia dhambi huja kwa mfumo wa mawazo huwezi kuyazuia mawazo mtumishi wa Mungu ila unao uwezo wa kuyafukuza mawazo kwa jina la Yesu. sasa dhambi hukaa ndani
Kosa ni matokeo ya ile dhambi iliyo ndani yako.Evil is the result of existing power of sin inside you.
tukisema mtu amefanya dhambi yaani ameyafanya yale yaliyomo ndani yake.
Daudi kwanza alivutiwa na uzuri wa mke wa Uria na mawazo yalivyoitawala akili yake akapata wazo la kumwua Uria ili amtwae mkewe.
Kwanini Daudi aliomba msama kwa Mungu?
1.Aliyatambua makosa yake.
unaweza kujiuliza hivi wakati anayafanya hakutambua?mawazo ya dhambi yakimtawala mtu yanamtawala.soma Rumi 6:12 dhambi ikitawala unamwaga sumu utakuwa kama maamuma unalolifanya hulijui.Rumi 7:17sio wewe ila hiyo dhambi ndani yako.
Daudi alitambuaje makosa yake? Ni baada ya kuambiwa na mjumbe wa Mungu.watu leo tunaposikia neno la Mungu hatutaki kusikia ila Daudi alikiri...neno la Mungu linaingea juu ya habari ya maisha yako wewe.

2.Kujutia kosa.
Daudi alijutia kosa baada ya kutambua makosa yake. majuto ndiyo yaliyoonesha wazi ni kwa jinsi gani Daudi alijutia.(2samweli 12:13).
Daudi alijutia sana kwa aliyoyatenda.

3.Hasira ya Mungu
Daudi alitambua kuwa Amemkasirisha Mungu kwa kitendo alichokifanya.kinachosikitisha watu wanafanya maovu alafu wanachekacheka tu!wakati Mungu anachukizwa....
Mungu awabariki sana kwa kusoma najua kuna mengi umeyapata
Mbarikiwe.

RGP Mbogo
0655 445525.

Comments