ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula |
BWANA YESU
asifiwe ndugu.
MUNGU
amekupa uzima na nafasi ya kujifunza somo hili kwa kusudi lake maana ana mpango
mwema sana na wewe.
karibu.
Tuko huru
kwa sababu BWANA YESU ametuweka huru
Uhuru
ulianza lini?
Uhuru wetu
unaanzia Golgotha/ Kalvari pale msalabani ambapo BWANA katika kuukamilisha
uhuru wetu na kutupa wokovu alisema IMEKWISHA-Yohana 19:30.
-IMEKWISHA =
yaani hatuhitaji tena kuwafuata waganga
wa kienyeji ili kutuponya, hatuwezi tena kuwafuata wasoma nyota, wasoma bao,
wasihiri wala hatuhitaji tena kutumia mazindiko ya aina yeyote, hatupaki tena
dawa ya kuondoa mikosi wala hatupulizii
tena udi na uvumba maana BWANA YESU
ametuweka huru.
-Tunakuwa
huru kwa kumpokea BWANA YESU kuwa BWANA na MWOKOZI wa maisha yetu.
- Tukimpokea
BWANA YESU tunakuwa watoto wa MUNGU (Yohana 1:12- 13 ''Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake;
13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU.'' ).
13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU.'' ).
-Tukimpokea
BWANA YESU tunakuwa na kibali na haki ya kutokuvamiwa wala kuonewa na wachawi,
majini au mapepo.(Isaya 54:17) Hivyo ndugu ni wajibu wako tu leo kumpokea BWANA
YESU moyoni mwako na baada ya hapo utakuwa na kibali na haki ya kuharibu kazi
zote za shetani.
omba tu
leo kwamba wachawi waachie watoto wako
kwa jina kuu la YESU KRISTO.
-Tuko huru
kwa sababu BWANA YESU ametuweka huru.
-Katika
kukamilisha ukombozi pale msaabani
=PAZIA LA
HEKALU LILIPASUKA.(Marko 15:38) hiyo inamaanisha mapazia yote waliyokuwekea
adui zako ili usipandishwe cheo kazini
tunayapasua leo kwa jina la YESU KRISTO,
Shetani amewafunika
ukoo wenu kwa pazia ili kwamba kila mtoto anayezaliwa katika ukoo
wenu lazima avishwe hirizi shingoni, kiunoni, mikononi, miguuni tena anavishwa
haya baada tu ya kuzaliwa. Lakini leo tunaondosha utawala huo wa shetani kwa
jina la YESU KRISTO aliyetuweka huru.
Ndugu
utakuwa huru kama BWANA YESU KRISTO akikuweka huru.
Shetani amewawekea
pazia/ mpaka ukoo wenu hamtakiwi kusoma hadi chuo kikuu nyie ukoo mzima
mmeishia darasa la saba tu, leo tunapasua pazia hilo kwa jina la YESU KRISTO
anayeweka watu huru mbali na shetani.
-Ndugu
ukimpokea BWANA YESU hakika utakuwa huru na yeye anasema katika Yeremia
15:20-21(Nami nitakufanya kuwa kama ukuta wa boma la shaba juu ya watu hawa; nao
watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, ili
nikuokoe, na kukuponya, asema BWANA.
Nami nitakuokoa na mkono wa watu wabaya, nami nitakukomboa katika mkono wao wenye kutisha.
).
Ndugu,
shetani haogopi jina lolote ila anaogopa jina la YESU KRISTO pekee, na unajua
kwa nini shetani na malaika zake wanaogopa jina moja tu yaani jina la YESU
KRISTO? Biblia katika Mathayo 28:18 inajibu swali hilo.''YESU akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
''
-Tunapozungumzia
jina la YESU KRISTO tunazungumzia mamlaka ya maamuzi kwa kila jambo, mamlaka ya
YESU KRISTO ni ya mwisho kwa utukufu wa MUNGU BABA.
Ndugu,
itumie mamlaka hii shetani na watoto wake yaani magonjwa, wachawi na majini
wataogopa na kukukimbia.
Ndugu yangu,
-BWANA YESU
alipokuwa katika kukamilisha wokovu wetu tukio jingine lililotokea ni
=MAKABURI YA WATAKATIFU YALIFUMKA na
watakatifu wakatoka makaburini (Mathayo 27:22).
Kaburi ni
kitu chochote kilichokufunga ili shetani akutese, kaburi linaweza kuwa ni
ugonjwa, ukimwi,umaskini,kufeli masomo kila siku N.k.
Wewe ni mmoja
wa watakatifu hao ambao kaburi lililokufunga lazima liachie kwa jina la YESU
KRISTO, Makaburi ya magonjwa lazima yafumke na wewe mtakatifu wa MUNGU utoke
salama.
-Makaburi ya
madeni lazima yafumke na wewe utoke salama.
Makaburi ya
kuteswa na maroho ya ukoo, mizimu na mapepo lazima leo yakuachie wewe uliyeko
kwenye makaburi hayo kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Utakuwa huru
mbali na ukimwi unaokutesa kwa jina la YESU KRISTO, na mimi katika maisha yangu
ya wokovu nikiwa Zanzibar tuliwahi kumwombea dada mmoja aliyekuwa na ukimwi
ambaye alikuwa ameshapima hospitali tatu yaani Mnazi mmoja, Bububu na Al-rihma ambazo
ndizo hospitali kubwa zaidi Zanzibar lakini pote alikutwa na ukimwi, walimleta
kanisani tukamwombea baada ya maombezi akaondoka sikumwona tena ila baada ya
wiki 2 nikiwa natoka Darajani naenda chukwani niliposhuka tu kituo cha chukwani
mwisho nikasikia mtu akiniita kwa nguvu sana akisema ‘’Mchungaji, mchungaji,
mchungaji’ nikageuka nikamkuta ni yule dada ambaye wiki mbili nyuma aliletwa
kanisani akiwa kakonda na mwili wake kubaki mifupa na hadi ndugu waliokuja nae
walikuwa wanamwogopa kwa jinsi alivyokonda lakini kwa maombi BWANA YESU
akashuka na kumweka huru. Na alijikuta akinikimbilia kwa furaha huku akiniita
mchungaji kumbe wala mimi sio mchungaji ni muumini tu kanisani, na aklikuwa
amepima Hospitali 4 tofauti na kukutwa hana tena ukimwi, sifa,heshima, adhama
na utukufu ni kwa BWANA YESU anayefungua watu, ndugu mpe maisha yako leo na
utakuwa huru tena huru kabisa. Na ninapokueleza juu ya kuwekwa huru nimeona kwa
macho yangu matendo hayo makuu ya BWANA YESU akiwaweka watu huru mbali na
magonjwa na mapepo na kila aina ya maonezi ya shetani. Ndio maana 1Yohana 3:8
Iinasema kwamba ‘’BWANA YESU ALIDHIHILISHWA ILI AZIVUNJE KAZI ZA SHETANI.’’
Ndugu Biblia
inasema ukikubali na kutii utakula mema ya nchi. Na leo mimi nakuambia kwamba ‘’UTAKUWA
HURU KAMA BWANA YESU AKIKUWEKA HURU’’

Utakuwa
mbali na kifo cha mapema bali JEHOVAH MUNGU atatimiza hesabu ya miaka yako
aliyokukusudia.
Mpe YESU
maisha yako leo ndugu maana ukiwa ndani ya KRISTO Tazama umekuwa kiumbe kipya,
ya kale yamepita na sasa yamekuwa mapya (2 Kor 5:17)
YESU
akikuweka huru kakika utaishi MAISHA YA USHINDI.
UTAKUWA HURU
LEO KAMA BWANA YESU AKIKUWEKA HURU.
Ni mimi ndugu yako Peter Michael
Mabula.
-Maisha ya ushindi
Ministry.

Comments