UHAI KATIKA NJIA YA HAKI,NA MAPITO YAKE.

na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


Tunasoma;
"Katika njia ya haki kuna uhai;
Wala hakuna mauti katika mapito yake." Mithali 12:28.

Bwana Yesu asifiwe...
Haleluya...

Nakukaribisha mpendwa katika fundisho hili mahali hapa ambapo imekuwa ni Neema ya pekee kupata mafundisho mazuri ya IMANI.

Siku ya leo Bwana anazungumza nasi kwa namna ya tofauti kabisa. Nami namkaribisha Roho mtakatifu Yeye ambaye ni mwalimu wetu, atufundishe.

Katika andiko hilo hapo juu,tunaambiwa habari ya NJIA YA HAKI,kwamba upo uzima ndani yake.

Ikiwa ipo njia ya HAKI,basi pia ipo njia isiyo ya haki, njia ya DHURUMA.
Na ikiwa upo UHAI katika njia ya haki,
Basi ipo MAUTI katika njia ya dhuruma.

Haleluya...

Nataka niseme na mtu mmoja mahali hapa,fungua tu moyo wako, ili Bwana apate nafasi ya kukuhudumia siku ya leo.

*Uhai hupatikana katika njia ya haki tu,
Pia mauti hupatikana katika njia ya dhuluma.
Njia zote hizi zina mwisho wake yaani ;
" All these have got the end products."

Njia ya uzima ina matokeo yake.
Pia njia ya mauti ina matokeo yake.

Njia hizi mbili zipo tu,
yaani zipo tu,tena
tumewekewa mbele yetu,
ni mimi na wewe yatupasa kuchagua mojawapo ya njia ya MAUTI au ya UZIMA.

" Angalia,nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema,na mauti na mabaya."Kumb.30:15

Ukiyachunguza vizuri maandiko hayo utagundua jambo moja ambalo limewekwa mbele yako,nalo ni
*Uchaguzi
-Uchagunzi uliotumika hapo ni uwezo au fursa uliyopewa ya kuchagua mema au mabaya.

Mema au mabaya ni njia ya uzima au mauti ambayo mwenye uchaguzi huo ni wewe mwenyewe.

Sasa angalia,
( katika andiko la Mithali 12:28)

Tunaambiwa,
Uhai upo katika njia ya haki.

Kumbe!
*Yeye atembeaye katika njia ya haki,U na uzima.

Swali la kujiuliza,
Je njia ya haki ni njia ya namna gani?

Kwa mujibu wa maandiko matakatifu,anatajwa mtu mwenye haki ni yule mcha- Mungu.

Mfano mmojawapo kati ya mifano mingi wa mtu mwenye haki ni Yusufu (mumewe Mariamu) soma Mathayo.1:19

Hivyo mtu mwenye haki,ni yule ambaye ni adui wa dunia,Bali rafiki wa Mungu.

* Hivyo njia ya haki ni njia ya kumuishia Mungu tu.
Ni njia ya kutembea na Bwana Yesu.

Biblia inaeleza vizuri katika Mithali 12:28,kwamba;
"Kwa njia ya haki kuna UHAI..."
Ambapo ni sawa sawa na kusema;
" Katika njia ya kumuishia Bwana,kuna uhai.."

Haleluya...

Uhai unaozungumziwa hapo ni uzima wa milele ambao uzima/uhai huo hupatikana kwa BWANA YESU TU.

Ngoja nikuambie kidogo hapo,;
Akina Adamu na Hawa walipokula mti wa ujuzi wa mema na mabaya,walifukuzwa kotoka bustani ya Edeni kwa maana wasije wakala mti wa UZIMA wakaishi milele (maana kulikuwa na aina mbili za miti katika bustani ya Edeni,mti wa ujuzi wa mema na mabaya,na mti wa UZIMA) Mwanzo 3:22

Hivyo wakafukuzwa watoke katika bustani wakiwa wamekufa Kiroho kama Bwana alivyosema kwamba hakika watakufa wakila matunda ya mti waliokatazwa.

Tazama sasa,
Bwana Yesu Yeye amekuja akiwa ndio mti wa UZIMA,na ndio maana Bwana Yesu alimwambia Martha Dada yake Lazalo

" Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo,na UZIMA.Yeye aniaminiye mimi ,ajapokufa,atakuwa anaishi " Yoh.11:25.

Njia ya haki ina uzima
Njia ya Yesu pekee,ndio njia ya haki yenye uzima.
Maana Uzima u ndani yake Bwana.

Haleluya...

Yeye aliye ndani ya njia hii ya haki kamwe hawezi kufa,Bali atapitia tu,mautini na kuingia uzimani.

Kufa nikuzungumziapo ni kufa Kiroho na wala sio kimwili.

Hivyo jambo moja tunalojifunza kupitia fundisho hili ni kwamba,
Uhai wapatikama ndani ya Yes Kristo sababu Yeye ndio. Uzima,Yeye Bwana ndio njia ya haki.

Haleluya...

Biblia inaendelea kueleza vizuri kabisa juu ya njia ya UZIMA,kwamba
Hakuna mauti katika njia hiyo ya haki.

Bali yapo MAPITO katika njia ya haki.Maana ikiwa Yesu mwenyewe alipitia mapito ili sisi tuwe na uzima,basi iweje sisi watu wa kawaida?

Biblia inasema;
"...Wala hakuna mauti katika mapito yake" Mithali 12:28b

Mapito kwa mkristo ni lazima,Yeye asiyekuwa na mapito katika ukristo wake,basi ni dhahili ukristo wake utakuwa na matatizo.

Maana ili upande Kiroho ni lazima kuwe na mapito,ambayo kwa hayo yanakuhimalisha.

Hakuna dawa ya kuondoa Mapito kwa mkristo,Bali ni lazima utayapitia tu,ili ukomae kiimani.

Mapito hayaombewi kwamba yasikuje,
Mapito hayakemewi kwa Maombi kwamba yasije,

Yenyewe yatakuja tu,
Bali yakupasa uyavuke kwa USHINDI mkubwa ukisaidiwa na Roho mtakatifu.

* Mapito ni kipimo cha IMANI.
*Mapito ni mitihani,yakupasa ushinde,ufaulu kwa kiwango cha hali ya juu.

Kwanza yakupasa;
Umkubali Bwana Yesu,uokoke ili kwa huyo Bwana uwe na uzima wa milele maana Yeye Bwana Yesu ndie njia ya haki.

Pili uishi maisha ya HAKI,yaani maisha ya utauwa.

Nataka niombe na wewe muda huu,

Mawasiliano yangu ni ;
* 0655 111149
* 0783 327375

MWISHO.

UBARIKIWE.

Comments