USIMPE IBILISI NAFASI.

Raphael GP Mbogo


Shetani na mamlaka zake ni ufalme unaojitegemea.
Na ufalme wa shetani ni ufalme wa giza na ufalme wa Mungu ni ufalme wa nuru.
kulikuwa na nuru halisi amtiaye nuru kilamtu .huu ni ufalme wa Mungu.

sasa ufalme wa giza hauna mamlaka ya kukutawala pasipo ruhusa yako mwenyewe.
Efeso 4:27..ukiona mambo yako hayaendi vizuri ujue kuna sehemu umempa nafasi.
moja ya nafasi ni kukaa na hasira.biblia inasema hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu ila haijasema aliye na hasira ni mpumbavu..hasira ipo ila tatizo ni pale unapoihifadhi ndani huu ni mlango wa adui ndani yako

sehemu nyingine ambayo tunampa ibilisi nafasi ni:
1.Kutojua thamani.
mathayo 13:45-46.Thamani ni mojawapo ya kumpa nafasi adui.huyu akauza vyote alivyo navyo ili aipate lulu yenye thamani.sasa shetani hataki wewe uyaache yote ya ulimwengu kwaajili ya Neno la Mungu.
Watu hatujui thamani ya neno la Mungu katika maisha yetu tunabaki kuvithamini vitu vya ulimwengu kuliko neno la Mungu.
huu ni mlango wa adui,ukithamini mambo ya dunia unampa shetani nafasi..
mbarikiwe.

Raphael Mbogo.
+255655445525
 

Comments