WACHAWI WADONDOKA MKUTANO WA GWAJIMA TANGA, MWINGINE AKAMATWA AKIMWAGA CHUMVI UWANJANI



Zikiwa zimepita siku nne tangu mkutano wa injili unaoendeshwa na kanisa la Ufufuo na uzima viwanja vya Tangamano jijini Tanga uanze, matukio mengi tayari yamekuwa yakitukia katika viwanja hivyo ikiwemo wachawi kudondoka wakati wa maombi, popo wasio na idadi kutimka majira ya saa 10 za jioni katia viwanja hivyo, pamoja na matukio ya watu kuja kumwaga chumvi viwanjani hapo.

Tukio la wachawi watatu kudondoka lilitokea juzi wakati mkutano huo ukiendelea ambapo mmoja wao ni mama mtu mzima huku wengine waliangukia walipokaa watu ambao walianza kuwapiga kabla hawajaokolewa na timu ya kanisa hilo ambao waliwachukua na kuwapandisha jukwaani kwa mahojiano huku watu wakipiga kelele za kuwataka washushwe ili wawaadhibu, lakini mchungaji Josephat Gwajima aliwaelewesha watu hao juu ya jambo walilokuwa wanataka kulifanya kwamba si jema zaidi ya kuwaombea ambapo maelfu hayo yalisikia sauti ya mchungaji Gwajima nakuwasamehe.

Matukio mengine uwanjani hapo ni watu wazima ambao walikamatwa majira ya mchana kwa nyakati tofauti, mmoja akiwa mwanamke alionekana akimwaga chumvi uwanjani hapo lakini alikamatwa akitaka kuelekea madhabahuni ambapo watumishi wa kanisa hilo walipokuwa wakianza kumhoji walitokea polisi ambao waliamua kumchukua kumfungulia mashtaka kituoni hata hivyo haikujulikana kama kweli alienda kufunguliwa mashitaka hayo.


Bibi aliyedondoka uwanjani hapo akiwa kwenye mambo yake ya ushirikina.
Mchungaji Gwajima akimhoji bibi huyo.
Mke wa Gwajima ama first lady wa Ufufuo na uzima kushoto akimhoji bibi huyo.
Watu walipokuwa wakipiga kelele kutaka mchawi huyo ashushwe wampige.
Wachawi walioanguka mkutanoni hapo wakiwa wamekaa pamoja huku mchungaji Gwajima akiwaangalia.
Wachawi wakiwa wamekaa.
Mchungaji Gwajima akiwaombea msamaha wachawi hao. 
Maelfu ya watu wa Tanga wakiwa mkutanoni hapo.
Picha ikionyesha watenda kazi wa Ufufuo wakimvuta binti anayedaiwa kuwa ni mchawi kutoka mikononi mwa wananchi.
Maombi yalipopamba moto.
Mti wenye umbo la sura ya mtu ukiwa maeneo ya uwanja wa Tangamano.
Vifuko vyenye chumvi alivyokamatwa navyo msichana mwenye picha inayofuata chini.
Mmwagaji chumvi uwanjani mchana kweupe.
Walifika kusikiliza mkutano.
Haijalishi umetoka dini gani wala dhehebu mbele za Mungu.
Acha kabisa, walifika walikuwepo kusikiliza neno.

Popo waliofumuka mida ya saa kumi wakati Gwajima anaanza kuhubiri, kisha likafuata vumbi na mvua juu, lakini neno lilipigwa na maombi yakafanywa.
Tanzania kwa YESU.

Comments