BWANA ATAKUDAI FAIDA YA TARANTA YAKE.*sehemu ya kwanza*

Bwana Yesu asifiwe...
Na Mtumishi Gasper Madumla


" Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri,aliwaita watumwa wake,akaweka kwao mali zake.Akampa mmoja talanta tano,na mmoja talanta mbili,na mmoja talanta moja KILA MTU KWA KADIRI YA UWEZO WAKE;akasafiri. " Mathayo 25:14-15

Haleluya...
Bwana Yesu asifiwe...

Nakukaribisha katika fundisho hili ambalo ndio kwanza leo limeaanza.
Leo ninaweka msingi wa fundisho hili mahali hapa,
Karibu tujifunze;

Bwana Yesu anatufundisha siku ya leo kupitia mfano wa bwana aliyesafiri huku akiwa ameweka mali zake kwa watumwa wake. Akitufundisha siri za ufalme wa mbinguni.
Na anatuambia jambo la ajabu na zuri sana.

Anasema hapo;
"Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri,aliwaita watumwa wake,AKAWEKA MALI ZAKE"

Tazama hapo,
Kwanza huyu mfalme ameweka mali zake kwa watumwa.
Hivyo mali hizo ni za mfamle sio za watumwa.Tena jambo jingine tunaona kwamba mfalme alihakikisha kwamba mali zake haweki kwa mwingine awaye yote,bali kwa watu wake wa nyumbani.

Kwa sababu laiti kama ang'eweza kuweka kwa mtu yeyote yule basi asing'epata FAIDA,maana lengo lake haswa ni kupata FAIDA.

Alikadhalika BWANA MUNGU naye ameweka mali zake kwetu sisi kwa kutafuta FAIDA.
Kumbuka,
Mali ni kitu cha thamani sana kilichowekwa kwa makusudi ya kupata ongezeko,faida.
Mali hizi sio moja,Bali ni zaidi ya moja.

Biblia inatuambia kwamba mali zilizokuwa zimewekwa ni TALANTA.

Hivyo mfalme aliziweka talanta zake kwa watumwa wake kwa lengo la kupata faida,hivyo huyu bwana alikuwa ni mfanyabiashara.

Kwa lugha nyingine,
Zile talanta hazikuwa mali za watumwa,zilikuwa ni mali za bwana wao,Bali watumwa waliaminishwa tu.

Hivyo yeye mwenye kuweka kito cha thamani kwako ,kwanza ni lazima akuamini katika utunzaji wa hiyo mali yake,maana mali ni kito cha thamani sana,la sivyo hawezi kuifadhi kwako ikiwa wewe sio mwaminifu.

Watumwa hawa,bwana wao aliwaamini ndio maana akaweza hata kuweka Mali zake kwao.

Ooh,kumbe.!
Ili BWANA aweke talanta/mali zake kwako,kitu cha kwanza anaangalia uaminifu wako juu ya hiyo talanta.

Sasa angalia;
Huyu bwana aliyeweka talanta zake kwa watumwa wake,anasema;
Aliweka talanta hizo tofauti tofauti kwa watumwa wake KWA KADIRI YA UWEZO WA MTUMWA.
Hii ikiwa na maana kwamba ;

01.Wale watumwa hawakupewa talanta sawa zinazofanana.

02. Kila mtumwa mmoja alipewa talanta kwa kadiri ya uwezo wake.

* Uwezo unaozungumziwa hapa ni ile nguvu ya kuzalisha-productive power.
Hivyo kila mtumwa alikuwa na uwezo/nguvu ya kuzalisha lakini uwezo wao wa kuzalisha ulitofautiana.

Nasema hivi;
Uwezo wao wa kuzalisha ulikuwa haufanani hata kidogo,ndio maana bwana wao hakuwapa talanta za kufanana,maana mmoja alimpa talanta tano,mwingine mbili na mwingine moja.

Jambo moja tunalojifunza siku ya leo juu ya mfano huo wa talanta/mali .
Ni kwamba;
BWANA MUNGU wetu wa mbinguni yeye naye ameweka talanta zake kwetu sisi kwa madhumuni ya kupata faida,
Ameweka kwetu kwa kadiri ya uwezo wetu wa kuzalisha.

kwa kila mmoja amepewa talanta ya tofauti kwa kadiri ya UWEZO wake.

Pia jambo la pili ambalo tunajifunza hapa ni kwamba
BWANA MUNGU naye pia anafananishwa na mfanya biashara ambaye anatafuta FAIDA juu ya talanta alizoweka ndani yetu.

Kanuni mojawapo ya Mungu wetu aliye hai ni kutafuta faida.
Ukiona umeaminishwa talanta ,ujue ataitaka faida. mikononi mwako.

Ukiendelea mbele katika andiko hilo la Mathayo 25:14-30 utaona kuwa
yule bwana anarudi kwa watumwa wake akitafuta faida juu ya kila moja.

Ngoja nikuambie kitu mpendwa,
bwana yule,pale aliporejea hakuzijia zile talanta zake bali alichokilenga ni FAIDA juu ya zile talanta.
Hivyo hakikumsumbua talanta maana aliwaamini kwamba hata atakaporudi atazikuta tu,lakini kilichumsumbua pale ni faida kwamba je atazikuta hizo faida.

Je ajapo BWANA wa mbinguni atapata faida kwako kwa dhamana aliyokupa.?

Haleluya...
Ahh!,
Nalipenda sana hili fundisho.

Labda tujiulize maswali haya kabla hatujafika mbali,

*Talanta ni nini?
* Je ni kweli BWANA atazidai Atalanta zake?

-Talanta ni zawadi,(gift)
-Talanta ni mali ya Bwana inayowekwa kwa watu wake.
-Talanta hufananishwa na Karama,ambapo karama ni utendaji kazi wa Roho mtakatifu kwa watu wa Mungu.

Tazama vizuri katika hilo andiko hapo juu,utagundua kwamba;
Wale waliopewa talanta ni wale watumwa tu wa yule bwana,
yaani ni watu wake yule bwana,ni watu wa nyumbani kwake. talanta zile hawakupewa watu wa mbali na yule bwana.
Hivyo waliopewa talanta zile ni watu wenye mahusiano na bwana wao.

Alikadhalika talanta za Bwana hutolewa kwa watu walio nyumbani mwa BWANA Mungu,watu waliooshwa kwa damu ya mwanakondoo,WALOOKOKA.

Hivyo talanta ni Mali ya BWANA mwenyewe.

Jibu la swali la pili,
Ikiwa talanta ni mali za BWANA basi ni kweli BWANA atazitaka FAIDA hizo kutoka mikononi mwetu.
Sisi tumeaminishwa tu...

ITAENDELEA...
*Usikose kabisa muendelezo wa fundisho hili mahali hapa.

Kwa maombezi,
*0655 111149.

UBARIKIWE.

Comments