IJUE MAANA YA WOKOVU (KUOKOKA)

Na Sam Balele


Shetani amekuwa akiwapumbaza wanadamu ili wasichukue uamuzi wa kupokea Wokovu kwa njia ya Imani katika Bwana Yesu Krsito kwa kuwaambia kuwa Wokovu ama Kuokoka ni aina fulani ya dini ama udhehebu tofauti na dini ama udehehbu waliozaliwa ndani yake. Wengi wa wanadamu, imani walizoshika hata sasa ni zile za kuzaliwa nazo. Kuna rafiki yangu mmoja, aliwahi kutumia phrase hii kutetea msimamo wake akisema Sam why are persecuting me "for my born faith". Imani inayofundishwa na Biblia si ya kuzaliwa nayo. Imani inayofundishwa na Neno la Mungu, msingi wake ni kusikia, tena kusikia kunatokana na kusikia neno la Kristo (Warumi 10:17). Imani ya aina hii ndiyo inayompa mwanadamu Wokovu. Sasa hebu nikupe elimu hii ili utie ufahamu moyoni mwako juu ya habari hii ya Wokovu; labda wewe ni mmoja wa wale waliofundishwa kuwa Wokovu ni udini ama udhehebu. Wokovu ni mpango wa Mungu uliokamilika tayari, wa kumrejesha kwake Mungu, mwanadamu aliyeuzwa kwa Shetani na kuwekwa chini ya utumwa wa nguvu ya dhambi na mauti tangia pale Adamu alipomuasi Mungu katika bustani ya Edeni. Nitagusa mambo makuu matatu ili kuyafumbua macho yako na Roho Mtakatifu, kiongozi wangu ambaye ninafanya kazi pamoja nae atakusaidia kuelewa hapo ulipo, katika Jina la Yesu Kristo.

KUOKOKA/WOKOVU/SALVATION ni nini? na yagusa sehemu ipi ya mwanadamu?. KUFUNGULIWA/UKOMBOZI/DELIVERANCE ni nini? na yagusa sehemu ipi ya mwanadamu?. KUKOMBOLEWA/UKOMBOZI/REDEMPTION ni nini? na yagusa sehemu ipi ya mwanadamu?.

Biblia inasema wanadamu wote wametenda dhambi, wamezaliwa katika dhambi kwa kuirithi kutoka kwa Adamu na Hawa, hivyo hakuna aliye safi, wote wanazaliwa wakiwa ndani ya utumwa wa nguvu ya dhambi na mauti. Na ni kwasababu hii sasa Yesu Kristo alikuja duniani na kufa msalabani ili atengue na kubadilisha the situation that existed and He succeeded and He said "IT IS FINISHED". Hivyo kitu ambacho Mungu anamtarajia mwanadamu kufanya ni kufahamu moyoni mwake kile alichofanya Mwanawe Yesu Kristo, kisha kuwa na moyo wa shukrani na kwa unyenyekevu kuipokea zawadi ya Wokovu kutoka kwake Mungu Muumba.

Nataka ufahamu kuwa kupokea Wokovu ni hatua ya sasa na wala si wakati wa kiyama. Kuokoka kwa mwanadamu ni sasa. Wokovu ni kitendo cha kuzaliwa mara ya pili, na kitendo hiki kinafuatia uamuzi wa mwenye dhambi kutubu dhambi zake [repentance of sins], huku akiamua kumuamini Yesu Kristo kwa moyo wake na kumkiri kwa kinywa chake kuwa Bwana na Mwokozi wake. Kwa uamuzi huu, mwanadamu huyu anahesabiwa haki bure kwa njia ya imani, yaani anapata msamaha wa dhambi zote alizotenda, Wakolosai 1:13. anapatanishwa na Mungu (1 Yohana 1:1-2), na hivyo anapewa neema na fursa ya kuanza uhusiano kwa upya na Mungu katika Yesu Kristo. Hapa kinachozaliwa mara ya pili ni roho ya mwanadamu, Hivyo wokovu unahusu UHUISHO WA ROHO ya mwanadamu ( Yohana 3:3). Yesu alisema mtu asipozaliwa mara ya pili [asipookoka], hawezi kuingia katika Ufalme wa Mungu, Na Ufalme wa Munfu ni nini kwani? Ufalme wa Mungu ni Haki,na Amani na Furaha katika Roho Mtakatifu (Warumi 14:17).

Sasa mwanadamu akishaokoka, akishazaliwa mara yapili, akishapatanishwa na Mungu, yaani akishapokea Wokovu anakuwa ameanza kuishi maisha kwa upya katika haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu ndani ya Yesu Kristo. Katika maisha haya mapya ndipo linapokuja suala la Deliverance, yaani kule kufunguliwa kwa vifungo alivyofungwa huyu mwanadamu. Vifungo hivi ni matokeo ya maisha aliyoishi katika giza akitenda matendo ya giza, kuanzia siku alipozaliwa kwa jinsi ya mwili duniani. Matendo haya ya giza ama walitenda wazazi wake ama alitenda yeye mwenyewe, huwa yanaweka vifungo ambavyo ili kustawi katika wokovu sawasawa na kusudi la Mungu ni lazima hivyo vifungo viondolewe. Kazi za Shetani husababisha vifungo vyenye uonevu kwa mwanadamu huyu kwa namna mbalimbali. Utakuta mtu ameokoka lakini maisha yake ni hopeless kabisa, ni kwa sababu ya hivi vifungo. Hivyo hapa deliverence inaanza ili mwana wa ufalme aishi kifalme na kutawala duniani (Ufunuo 5:9,10). Deliverance huwa ni endelevu kwakuwa vifungo ni vya aina mbalimbali na ndivyo vinavyoathiri mustakabali wa tabia na mwenendo wa mtu, vikiwa vimeshika na kujenga ngome katika fikira, mitazamo, elimu na maisha ya mtu katika ujumla wake. Hivyo deliverance inahusika na UHUISHO WA NAFSI ya mwanadamu. Katika nafsi ndipo penye nia, akili, nguvu ya uamuzi na hisia; haya yakiwa hayako sawa, maisha ya mwanadamu hapa duniani hayatakuwa sawasawa na Kusudi la Mungu.

Kwa hiyo mwanadamu aliyepokea wokovu, anaendelea na kutembea na Yesu Kristo katika njia nyembamba kuelekea uzimani, katika upya wa maisha, Mungu akiendelea kum-transform kila iitwapo leo kwa njia mbalimbali sawa sawa na Neno la Mungu (Warumi 12:1,2). Mtu huyu anakuwa amepigwa muhuri na Roho Mtakatifu, ambaye Biblia inasema ni arabuni [guarantee] ya watakatifu "UNTIL THE REDEMPTION OF THE PURCHASED POSSESSION" (Waefeso 1:13,14). Huyu mwanadamu aliyeokoka, huku akiwa anapata deliverance kila iitwapo leo kutoka vifungo mbalimbali vilivyomfunga, ndiye hiyo Purchased Possession ya Mungu, akiwa amenunuliwa si kwa fedha bali DAMU YA YESU KRISTO, na kutiwa muhuri na Roho Mtakatifu. Mwanadamu akiwa ni that purchased possession ya Mungu, sasa anakuwa katika hali ya kusubiri kwa saburi akiwa na tumaini la utukufu katika siku ile kuu ya Bwana, siku ya ukombozi, ambao ni huo ukombozi wa mwili wake, yaani UHUISHO WA MWILI wa mwanadamu. Ukombozi huu utatokea siku ya unyakuo. Biblia Takatifu inasema kuwa wale waliolala katika Bwana Yesu na hao watakaokuwa hai ndani ya Bwana Yesu siku hiyo ya Bwana, siku ya unyakuo wa watakatifu [watu waliokoka], watabadalishiwa mwili huu wa mauti na kuvalishwa mwili wa utukufu na kunyakuliwa kwenda kumlaki Bwana Yesu mawinguni. Paulo aliandika kuwa, "Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa". (1 Wakorintho 15:50-54).

Hivyo Wokovu ni Mlango [DOORWAY] to a life of deliverance, ili mwanadamu aweze kuishi sawa sawa na Kusudi la Mungu, free fromall forms/types/kinds and manner of bondage, huku akiwa na Imani na kudumu katika saburi na uvumilivu wa lile tumaini la utukufu ujao katika Yesu Kristo, yaani kule kufunuliwa kwa wana wa Mungu, ule ukombozi wa mwili wake uliochapwa laana pale bustani ya Edeni na ambayo Bwana Yesu ameshamalizana nayo, kinachosubiriwa ni udhihirisho wa kazi aliyoifanya katika eneo hilo. Hapa nataka ukamate kitu, ni hivi ili uje kunyakuliwa ni lazima unyakuo ukukute ukiwa ndani ya Bwana Yesu na si vinginevyo, na kuwa ndani ya Bwana ni ndio kuokoka kwenyewe huko sasa, ndio maisha ya wokovu sasa. Mwanadamu asitarajie kufaidika na ukombozi wa mwili wake ikiwa wokovu wa roho yake aliukwepa. Mungu ni Mungu wa utaratibu na kila amekipanga vizuri na ameweka wazi plan yake katika Neno lake, sasa dini ama udhehebu usikuchanganye hapa. Kila mtu atasimama kivyake. Kiongozi wako wa dini/dhehebu hatokushika mkono, hata yeye atakuwa na ya kwake. Angalia Biblia inasemaje.

Now mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu ndo haya na sasa Roho Mtakatifu amekujulisha. Mungu ameweka Wokovu kwanza as a DOORWAY to the other two [Deliverance and ultimately Redemption]. When Adam and Eve disobeyed God, "all three parts of mwanadamu" were affected separately; the spirit, the soul and the body. Therefore all three need a "DIVINE TOUCH", a "DIVINE WORK UP". The entire heavenly decidedly process begins with the spirit part being saved by grace through faith in Jesus Christ, which is the gift of God. Deliverance follows as this saved person [born again]remains in the Lord Jesus Christ grounded in the Word of God and Holy Spirit , whereas his soul gets refined and ultimately he will have the Redemption of his body. This is God's plan, and now you know it. No more excuses.

Sasa kwako wewe ambaye umekuwa unaukataa wokovu kwa vijisababu mbalimbali, labda kwa kutoelewa maana yake, naamini sasa utakuwa umeelewa nini maana ya wokovu na utakuwa umefumbuliwa macho na kupata ufahamu ndani ya moyo wako ili kuona umuhimu wa wewe kupokea neema hii ya wokovu. Chukua leo uamuzi wa kuacha mawazo yako na njia yako, mtafute Mungu maadamu anapatikana tena anasema wala hayuko mbali nawe (Isaya 55:6,7). Yasikilize maneno ya Bwana Yesu aliposema katika Yohana 3:3, kuwa pasipo kuzaliwa mara ya pili hakuna mtu atakayeingia katika Ufalme wa Mungu, yaani haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. Dini na udhehebu haviwezi kukupa ufalme wa Mungu, ni Yesu Kristo pekee ambaye ndio huo wokovu, kwani alisema Yeye ndiye Mlango, na wokovu ni mlango.

Sasa kwako wewe ambaye ulishachukua uamuzi wa kuokoka na unaendelea katika wokovu lakini ulikuwa hujaelewa vizuri hasa hali uliyonayo ina maana gani, naamini utakuwa umepata kitu. Manake , kuna mtu ameokoka lakini akitandikwa swali juu ya kuokoka kwake ataishia kujin'gatan'gata tu, utamsikia anakwambia wokovu ni kujitenga na dhambi na kushika amri 10 za Mungu alizompa Musa kule jangwani, hiyo siyo maana ya wokovu, japo kujitenga na dhambi ni part ya maisha ya wokovu. Niliwahi kumuuliza mpendwa mmoja hili swali akajiumauma tu. Aliye ndani ya plan imempasa kuifahamu plan vizuri.

Wokovu ni lazima. It is mandatory. Kama wataka kuiona Mbingu ya Mungu Muumba, basi I am telling you now, bila kukwepesha macho; kuwa kuokoka ni lazima, usijesema siku ya hukumu kuwa hukuambiwa, mimi nitakuwa shahidi kinyume nawe kuwa nilikuambia lakini ulidharau na kupuuzia na kukumbatia giza na ukaikataa nuru, kwa kuwa unapendezwa na matendo ya giza na starehe za kupita za ulimwengu huu. Mbingu ina gharama lakini sivyo dini na udhehebu zinavyofundisha. Ikiwa una nia ya kuokoka tafuta msaada kwa mtu unayejua ameokoka ili akusaidie kwa hatua zaidi.
Mungu Muumba akubariki sana.


Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12