JE UNALO JAMBO LA IMANI LITAKALO MGUSA MUNGU,WAKATI WA KUFA KWAKO? *sehemu ya kwanza*

Na mtumishi Gasper Madumla


BWANA Yesu asifiwe...
Haleluya....

Nasema,
Haleluyaa....

Mimi nijiuliza swali hili kila siku,kwamba ;

*Ikiwa zitakusanywa Biblia zote zilizopo duniani hivi Leo,
kisha zianzwe kuandikwa tena upya katika nyakati hizi,
Kutokana na maisha yetu ya kila siku ya kikristo.

*Je zitaandikwa zikajitosheleze kama Biblia tulizonazo hivi sasa?

Maana Biblia tunazozisoma ni maisha halisi ya watu waliyoyaishi,
Mfano ;

Kwa habari ya maisha ya kina Paulo yalikuwa ni maisha halisi,sio maisha ya kuigiza.

Kupitia maisha yao halisi, ndio yakakusanywa na kuitwa Biblia ambayo tunayojifunza kila siku makanisani.

* Sasa chukulia kwamba;
Biblia ianzwe kuandikwa upya kwa habari ya maisha yako halisi,
Je itakuwaje?

Wakina Paulo tutawaona leo Biblia ikiandikwa upya?
Au,
Wakina Petro watapatikana leo ikiwa Biblia itaandikwa upya?
Au,
Wakina Ibrahim,Isaka na Yakobo watakuwapo leo,kama itaandwa upya?

*We unafikiri itakuwaje?

Haleluya...

Mungu atusaidie sana tuweze kuwa na ALAMA ya kiimani itakayo mgusa BWANA MUNGU.Ambayo kwa hiyo itaweza hata kuandikwa katika vitabu vitakatifu.

Jambo la kiimani ni alama imgusayo Bwana Mungu pale unapokuwa haupo,

Au hata pale upo ,lakini upo katika hatari mbaya labda ya kufa hivi,kwamba hapo ndipo utahitaji Bwana akukumbuke.

Wapo watu walioacha alama zilizomgusa Mungu. Mungu Naye akaachilia jambo kwao,ingawa walikuwa wamekufa.

Ngoja tupitie maandiko kidogo;

Tunasoma ;

"Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa,jina lake Tabita,tafsiri yake ni Dorkasi(yaani paa);mwanamke huyu alikuwa AMEJAA MATENDO MEMA NA SADAKA ALIZOZITOA

Ikawa siku zile aliugua,akafa;hata walipokwisha kumwosha,wakamuweka orofani.

39.Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika,wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye,wakilia na KUMWONYESHA ZILE KANZU NA NGUO alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao." Matendo 9:36-37 & 39

Kilichomsukuma Petro hata kwenda orofani kuomba si kingine ,Bali ni ile ALAMA aliyoiacha Dorkasi.

Laiti kama Dorkasi asing'ekuwa na ALAMA ya kiimani yoyote ile,basi hata Petro asing'efuatwa aende kwa yule maiti Dorkasi,
Na wala asing'ejitaabisha kwa kumuombea.

Tazama sasa,
Dorkasi alikumbukwa kwa sababu ya matendo yake mema aliyoyafanya.

Biblia inasema kwamba walikuwapo wa kumlilia Dorkasi,
Swali kwako,

* Je unao watu wa kukulilia juu ya mambo uliyoyafanya ya kiimani?

Mimi nampenda huyu Dorkasi maana aliacha alama.

Mungu wetu huguswa na alama zako.
Kupitia hizo Alama za kiimani zinawesa kubadili mauti yako.

Haleluya...

Mauti ya Dorkasi ilibadilika kwa sababu ya ALAMA YA KIIMANI,tazama akawa mzima tena.

Uzima aliokuwanao Dorkasi hapo awali ni tofauti kabisa na uzima alioupata baada ya kufa.

Baada kufa alikirimiwa UZIMA utokao kwa BWANA ambao ni uzima wa umilele.

Haya yote yalikuwa hivi kwa sababu ya jambo moja tu,nalo ni ALAMA aliyoiacha Dorkasi.

Kipindi kile cha akina Petro ilikuwa sio rahisi kumuendea mtumishi wa Mungu kwa kumuomba aje kwako,kama hali ilivyo sasa.

Maana sasa waweza hata kumpigia simu mtumishi wa Mungu aje,naye huja.

Sasa zamani kulikuwa hakuna simu wala hakuna barua pepe,Bali kulihitajika kumuendea kwa miguu.

Hawa wanawake wajane haikuwasumbua kufunga safari kumuendea Petro,kwa sababu ya mtu mmoja tu,aliyeacha alama ya kukumbukwa,naye ni Dorkasi.

Tazama namna ambayo Petro alivyoguswa na huu msiba wa Dorkasi kwa sababu tu ya matendo yake mema.

Yale maisha aliyoyaishi Dorkasi ndio yaliyoaandikwa na yakawa sehemu ya maandiko matakatifu.

Wala sio maisha ya tamthilia ,sio maisha ya kuugiza.Bali yalikuwa ni maisha halisi ya Dorkasi.

Je wewe una Alama ambayo kwa hiyo utakumbukwa,na hata maisha yako kuwekwa katika maandiko matakatifu?

Siku ya leo tumuombe Mungu atusaidie tuweze kuwa na ALAMA.

Haleluya...

Tunasoma tena hapa;

" Siku hizo Hezekia akaugua,akawa katika hatari ya kufa.Isaya, nabii,mwana wa Amozi,akamjia akamwambia,BWANA asema hivi,

Tengeneza mambo ya nyumba yako;maana utakufa ,wala hutapona.

Basi Hezekia akajigeuza akaelekeza uso wake ukutani,akamwomba BWANA,akasema,

Nakusihi , BWANA ,ukumbuke sasa,jinsi nilivyokwenda mbele zako. Hezekia akalia sana sana." 2 Wafalme 20:1-3

Ukiendelea kusoma utaona kwamba Hezekia anapewa miaka mingine,ambapo hakustahili kuongezewa tena muda wa kuishi,

Lakini sasa tazama;

Mara tu baada ya kumkumbusha BWANA juu ya ALAMA aliyokuwa ameiacha mbele za BWANA,
Tunaona BWANA akihahirisha mauti ya Hezekia..

Jambo moja tunalojifunza hapa kwa habari ya Hezekia ni kwamba;

Hezekia alikuwa ni mtu aliyemtumaini BWANA kwa kiwango cha juu sana.

Watu wengi tunafikiri kwamba ,Hezikia alikuwa Mtu wa kawaida tu.
Hezekia alikuwa mchaji wa Mungu.

Uchaji wake mbele za Bwana ulikuwa ni ALAMA tosha ya kumkumbusha BWANA.

Sijui wewe una ALAMA gani mbele za BWANA itakayo mgusa BWANA,
Kiasi cha kuokoa mauti yako.

ITAENDELEA...

*usikose fundisho lijalo mahali hapa,
Kwa huduma ya maombezi
* 0655 111149

UBARIKIWE.

Comments