Neno linasema: "KWA SABABU HIYO NINYI NANYI JIWEKENI TAYARI; KWA KUWA KTK SAA MSIYODHANI MWANA WA ADAMU YUAJA" (Math 24:44)
=>Fikiria kama leo Kristo angetokea kwenye mawingu ya mbinguni, ni nani... Angekuwa tayari kumpokea?

Mungu anajua
endapo tunazishika sheria zake ktk ukweli. Anajua kabisa lile
tunalo(ifanya, tunaloliwaza na kulisema. Je TUNAJIANDAA KUMPOKEA MFALME?
Atakapokuja kwenye mawingu akiwa na nguvu na utukufu mkuu, utaweza
kusema, "TAZAMA HUYU NDIYE MUNGU WETU, NDIYE TULIYENGOJA ATUSAIDIE"
(Isa. 25:9)? Kwa hao watakaosema, Kristo atawaambia, "PANDENI JUU ZAIDI
Mkapokee TAJI YA UZIMA"
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12 MUNGU akubariki sana
by Renutus Mzurikwao
Comments