![]() |
Mchungaji Dk na MB wa Viti Maalum(CCM), Getrude Rwakatare |
Kesi hiyo namba 70 ya mwaka 2012, iliyofunguliwa ili kuizuia NEMC
kubomoa nyumba hiyo ilitajwa juzi katika mahakama hiyo chini ya Jaji
Hamisa Kalombola.
Baada ya kusikilizwa kwa kesi hiyo, Mwanasheria wa NEMC, Manchare
Heche, alisema kesi hiyo imehairishwa ili pande zote mbili kuwasilisha
hoja za mwisho kwa maandishi na baada ya hapo mahakama itatoa uamuzi.
“Kesi imehairishwa ili tuwasilishe hoja za mwisho kwa maandishi halafu
baada ya hapo sasa mahakama itatoa uamuzi,” alisema Heche.
Pingamizi ya Kesi hiyo ilifunguliwa na Mbunge huyo kupinga NEMC
kubomoa nyumba yake iliyojengwa kando ya mto Mbezi Beach eneo la
Mndumbwe, jijini Dar es Salaam katika eneo la hifadhi ya mikoko
Comments