KIJANA HII NI FURSA YAKO USIKOSE KABISAAA


Askofu Sylvester Gamanywa, Rais wa WAPO Mission International.



Hili litakuwa kongamano kubwa la kitaifa na la aina yake la kufunga mwaka. litakalowashirikisha vijana wote wa umri wa miaka 12 – 35.

Litafanyika jumamosi ya tarehe 21 dec 2013

Taarifa iliyotolewa na Askofu Silvester Gamanywa mwangalizi wa kitaifa na kimataifa wa WAPO MISSION INTERNATIONAL ndiye mwenye maono haya, amesema kuwa kila kitu kwa ajili ya maandalizi ya siku hiyo yako tayari. ameongeza kusema kuwa ktk kongamano hili linalotarajiwa kukusanya vijana 4000 litakuwa na walimu 3 na yeye akiwa ni mmoja wao atakayefundisha juu ya kurithisha vijana wa kizazi kipya maono aliyonayo kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.

Kwa mujibu wa askofu Gamanywa kufikia 2028 vijana wa kizazi hiki wawe wana uwezo wa kufanya vitu vyao bila kuitegemea serikali na bila kutegemea msaada kutoka nje!

Kuhusu vijana wanasemaje kuhusu kurithishwa maono haya, wamefurahia kuona mtumishi gamanywa akiwajali vijana wote bila kubagua itkadi zao za kidini, hivyo ni kitu nadra sana kupatikana watu wa jinsi hii katika jamii tuliyo nayo. Wamempongeza sana askofu kwa maono haya, nao wakiahidi kuwa waaminifu kwa kile watakachopata kutoka kwake.

Wito kwa vijana wote mnakaribishwa jumamosi tarehe 21 dec 2013 ya t katika ukumbi wa BCIC mbezi beach kituo cha jogoo.

 
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12 
             chanzo. Gospel kitaa blog

Comments