KUFUNGA NA KUOMBA (sehemu ya kwanza)

Na Nickson Mabena, hapo ni mruvango, wilayani siha mpakani mwa mkoa wa Kilimanjaro na Arusha

ISAYA 58:3-8
"3.Husema, mbona tumefunga, lakini huoni?. Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii?. Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu. 4.
Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu....."

Kufunga ni kuuweka wakfu mwili kwa ajili ya kuzungumza na Mungu (Kuomba)

Pia unapofunga unakuwa unajinyenyekeza mbele za Mungu,
Ezra 8:21
"Ndipo nikaamuru kufunga, hapo kwenye mto ahava, ili tupate kujinyenyekeza mbele za Mungu, na kutafuta kwake njia iliyonyooka, kwa ajili yetu sisi wenyewe, na kwa ajili ya watoto wetu, na kwa mali yetu yote"

Kama yanavyotuonyesha maandiko kwamba tunafunga ili kujinyenyekeza mbele za Mungu, na kuisikizisha sauti mbele zake yaani kuomba.
Mtu wa Mungu anatakiwa kufunga ili aombe, kufunga bila kuomba ni sawasawa na kushinda njaa tu! inakuwa ni kazi ya hasara.

Hebu tuangalie pia habari za kufunga kwenye maandiko ya Agano jipya.
YESU ALIFUNDISHA KUFUNGA
".......... Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso," Math 6:16,17
Kumbe kufunga kupo, kama kusingekuwepo, Yesu asingesema "bali wewe ufungapo"

LINI HASA NI SIKU YA KUFUNGA !?
Swali kama hilo pengine kuna watu wanalo, ila niseme kwamba huwezi kuijua SIKU ya kufunga bila ya kujua kwanza SABABU za kufunga!. Zipo sababu nyingi sana za kufunga kwa ajili ya Maombi, lakini kwa neema ya Mungu nimeandaa sababu kadhaa tu, Lakini namwamini Roho Mtakatifu atakufundisha zaidi ya Hapa...

Sasa haimaanishi kwamba mtu akiomba bila ya kufunga, basi hawezi kujibiwa maombi yake, hapana!!

SABABU ZA KUFUNGA NA KUOMBA

a) Ni agizo la Mungu ( ni mapenzi ya Mungu)
Siku zote mwanadamu anatakiwa kutafuta, kuyajua na kuyatenda mapenzi ya Mungu,
Basi mojawapo ni kufunga na kuomba!

"Nao wanafunzi wake Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga; basi walikuja, wakamwambia, Kwani wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wa Mafarisayo hufunga, bali wanafunzi wako hawafungi?....... Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana~arusi, ndipo watakapo funga siku ile" Marko 2:18,20

Yesu aliwajibu waliomuuliza ya kwamba zipo nyakati ambazo wanafunzi wake watatakiwa kufunga.

b) Kufunga na kuomba ni ishara ya Kumtafuta Mungu kwa bidii

"Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona" Mith 8:17
Ili tuweze kumwona Mungu katika maisha Yetu ni lazima tumtafute kwa bidii,
Maana yake tunaweza kumtafuta, ila tusipomtafuta kwa Bidii hatuwezi kumwona. Na njia mojawapo ya kumtafuta Kwa bidii ni kwa kufunga na kuomba.

Suala la kumtafuta Mungu ni La kila siku, Kwa hiyo ni lini hasa mtu anatakiwa afunge na kuomba
Ni siku yoyote ile ambayo Roho Mtakatifu atakuongoza ufanye hvyo, HAKUNA SIKU MAALUM KWA AJILI YA KUFUNGA NA KUOMBA!!

c) Pia Yesu na Mitume walifunga na kuomba.

YESU
"akijaribiwa na ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipo timia aliona njaa" Luka 4:2
MITUME
" Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini" Mdo 14:23

Mungu akubariki kwa kuusoma ujumbe huu!!

By Mwl Nickson Mabena
~~~~~~SOMO LITAENDELEA~~~~~~~~~~~~

Comments