KUFUNGA NA KUOMBA (Sehemu ya Pili)

na Mwl Nickson Mabena na hapo ni mruvango, wilayani siha mpakani mwa mkoa wa Kilimanjaro na Arusha


Isaya 58:3-8

Kwenye somo hili, sehemu ya kwanza tuliishia kuziangalia sababu baadhi za Kufunga na Kuomba...

Kwanza niombe radhi kwa kuchelewesha kuandika sehemu ya pili ya somo hili, ni kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu, lakini tunamshukuru Mungu kwa kuwa ametupa wazo la kutengeneze PAGE ili mtu awe na uwezo wa kupitia hata masomo yaliyotanguli ili apate kujua nini kinaendelea!!.

Nikaona nisimalize Mwaka nikiwa na kiporo cha somo.. Namshukuru Roho Mtakatifu aliyeniongoza kulimazia somo hili leo.
Leo nataka tuangalie kitu kingine kwenye Maombi haya ya Kufunga.

FAIDA ZA KUFUNGA NA KUOMBA

Tutakapozijua faida za kufunga, ndipo tutaweza kutaka kufunga, Zipo faida nyingi sana za Kufunga na Kuomba
Labda kwa nafasi niliyoipata, nikuletee sababu kadhaa;

1)Hutuongezea Viwango vya Imani.

"Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa?. Yesu akawaambia, kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, amin nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule;nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]" Math 17:19-21

Ni moja ya mafundisho ya Yesu, aliwapa suluhisho la tatizo lao la kushindwa kutoa pepo, ndipo aliwaambia ni kwa sababu ya upungufu wa imani yao!! Ila tena akawaambia namna ile haitoki ila kwa KUSALI NA KUFUNGA.
Ambapo neno KUSALI hapo lina maana ya Kuomba.

2)Hutufanya tuwe na Macho na Masikio ya kiroho.

ninaposema masikio ya kiroho, simaanishi tu Kuwa na uwezo wa kusikia sauti ya Roho Mtakatifu ndani yako, ingawaje ni njia mojawapo ya kukuwezesha kusikia sauti hyo
Nina maana ya kwamba, kutambua makusudi ya Mungu katika jambo unaloliombea pia hata katika maisha yako, hata kama umefunga na kuomba kwa ajili ya Jambo lingine tu!.

"Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwaba Ibada na Kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia." MDO 13:2

Roho Mtakatifu hakusema na Kufunua kusudi la Mungu, hadi pale walipofunga.

3)Hutuongezea Nguvu za Mungu ndani yetu.

Ukimwona mtu yeyote ana nguvu za Mungu nyingi, ujue maisha yake ni Ya kufunga na kuomba. Hakuna njia mbadala ya kuongeza nguvu za Mungu ndani yako, isipokuwa kufunga na kuomba.

Na mtu mwenye nguvu za Mungu za kutosha ndiye mwenye uwezo wa kuushinda ulimwengu huu, uliojaa kila aina ya vishawishi pamoja na tamaa. Ukiwa na nguvu za Mungu huwezi kutafuta kuombewa kila wakati, bali utataka kuomba mwenyewe.

4)Hutufanya tutoke kwenye Imani ya akili, kwenda Imani ya rohoni.

Imani ya rohoni ni uwezo wa mtu kuyaweka kwenye matendo mambo ya Mungu. Kwani maombi ya kufunga, yanafanya roho ya mtu iwe active kuliko nafsi au mwili wake.

Imani ya akili -Mtu kushindwa kuyaweka kwenye matendo mambo ya Mungu, ingawa yapo kwenye fahamu zake.

Mfano, mtu anaweza akafahamu ya kwamba ni muhimu kusoma NENO la MUNGU ila hasomi, au anafahamu kwamba Ibada ni mhimu ila bado anaacha ibada.

Yaani kwa kifupi analolisema ni tofauti na analolitenda.

MWISHO.
UBARIKIWE KWA KUUSOMA UJUMBE HUU!!!

NIKUTAKIE HERI YA MWAKA MPYA 2014.

 Mwl Nickson Mabena

 
 Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12