KUKIRI IMANI YETU:



"Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni." (Mathayo 10:32)
Kama kungekuwa na wakati ambapo maneno ya Kristo yapasa yasikiwe, ni sasa... Kwa njia ya utakaso wa ile kweli, tunaweza kubeba ushuhuda wa makusudi kwa ajili ya haki kwa waumini na wale wasio waumini.
Kutoka kwa Wafuasi wake, Kristo anataka waikiri imani kwa uwazi na Ujasiri. KUFICHA IMANI NA MAFUNDISHO YA MUNGU ILI WATU WASIOAMINI KTK ULIMWENGU WASIYAJUE, kwa Kuogopa kuwa imani yako na misimamo yako inapofahamika unaweza usiheshimike sana, ni UPOTOVU MKUBWA na Si SaWA.
Kila mmoja anatakiwa achukue nafasi yake na kuwa kama vile Mungu alivyokusudia awe, yaani kuwa tamasha kwa ulimwengu, kwa malaika na kwa watu. ULIMWENGU WOTE UNATAZAMA KWA SHAUKU KUBWA ISIYOELEZEKA, ILI KUONA MATUKIO YA MWISHO YA PAMBANO KUU KATI YA KRISTO NA SHETANI... Kamwe USIRUHUSU UKWELI WA MUNGU UWEKWE NYUMA, IWE NI KWA WOGA AU SERA ZA KIDUNIA.
MUNGU akubariki sana .
by Renatus Mzurikwao 

Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12