Kumbukumbu ya miaka 25 ya Ndoa ya Mtume Prosper Ntepa na Mchungaji Deborah Ntepa.

Mtume Prosper Ntepa na Mchungaji Deborah Ntepa ni waanzilishi wa Huduma ya The Oasis of Healing Ministries iliyopo Ubungo Jijini Dar es salaam nyuma ya Ubungo Plaza. Kwa muda sasa huduma yao imekuwa ya mafanikio katika kuihubiri Injili ya Yesu Kristo na kuwa msaada kwa watu wenye shida katika mafundisho na Ukombozi nchini Tanzania.

Mtume Prosper Ntepa amemuoa  Deborah Ntepa miaka 25 iliyopita hivyo kwa sasa akiwa ni mtenda kazi mwenzake katika huduma Bwana aliyompa ya Oasis of Healing Ministries.Katika Miaka yao ya ndoa Mungu amewabariki na watoto 4 wakike  (Alice, Angela, Faraja and Shaddai).

Mwaka huu Mtume Prosper Ntepa na Mchungaji Deborah Ntepa wanasherekea 25 ya Kumbukumbu ya Ndoa yao.

Uongozi mzima wa Blog na wadau wake tuna watakia Miaka Mingi yenye utosherevu na mafaniko katika Ndoa na Kumtumika Mungu.



                 
               


chanzo: Jesus vision blog

Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12