Kati ya mambo ambayo yamewatoa vijana kutoka hatua moja
iliyochoka kwenda hatua nyingine madhuhuri na yenye matumaini kiroho na
kimwili, basi ni Operesheni Takasika. Vijana kutoka maeneo mbalimbali ya jiji
la Dar es Salaam na viunga vyake wamefanikiwa kwa hatua kubwa kupata mabadiliko
kwenye maisha yao, na kumpa nafasi Roho Mtakatifu awe kiongozi wa maisha yao.
Gospel Kitaa ambayo imekuwa ikipata simu kadha wa kadha kwa
nyakati tofauti kuhusiana na watu wanaohitaji kufika kwenye operesheni hiyo,
imeshuhudia maelfu ya vijana waliofika kwa hatihati wakiondoka kwa amani na
furaha, mara baada ya kupata mafundusho ya namna ya kuenenda maishani, kwenye
kilele cha operesheni hiyo, ambayo imekuwa msaada mkubwa si tu kwa kanisa, bali
pia kwa taifa kiujumla, katika kurejesha maadili, na kumrudia Mungu kwa waliogeuka kuwa baridi.
Askofu Sylvester Gamanywa |
Mbeba maono wa operesheni hiyo, Rais wa WAPO Mission
International, Askofu Sylvester Gamanywa, ambaye anaeleza kuwa ni wakati wa
kurithisha maono kwa kizazi kipya, hachoki – na Mungu ambariki, kwani kwa hivi
sasa ni mkakati wa kuhakikisha kuwa baada ya kupata muongozo wa Roho Mtakatifu,
ifikapo mwaka 2028 vijana wa Kitanzania
walioamua kuishi maisha ya uchaji Mungu
wawe wamewezeshwa kifedha na wawe pia wamefanikiwa kujitegemea kiuchumi,
kupitia Operesheni Wezesha.
Operesheni hii inakuhusu moja kwa moja, Gospel Kitaa
itaendelea kukufahamisha kuhusiana na operesheni hii hatua kwa hatua kwa
kadri
ambavyo taarifa zitakuwa zikipatikana, na kama hukufanikiwa kuwepo siku
ya hitimisho ya Takasika, GK itakuletea picha zote, jitayarishe.
chanzo:Gospel kitaa blog