Maana ya kuokoka

na Fadhili  Malaki
Kuokoka ni mabadiliko ambayo yanamtokea mtu yeyote pale anapomukubali bwana Yesu nakuwa mwokozi wa maisha yake 2kor5;17 hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kiya;yakale yamepita tazama yamekuwa mapya..
.Maana yake nikuwa ukishamkubali YESU awe mwokozi wa maisha yako unageuzwa unafanywa upya kwa nguvu ambayo inatokana na MUNGU mwenyewe soma Yohana1;12 bali wote walio mpokea aliwapa uwezo wakufanyika kuwa watoto wa MUNGU.... maana ya mstari huu nikuwa unakuja uwezo ambao unakuvaa na kufanyika mtoto wa MUNGU.kuna mtu mmoja alimfuata YESU usiku huyu Nikodemu alikuwa msomi wa sheria alafu mkuu wa Wayahudi kwamaana nyingine alikuwa kiongozi.Nikodemu akamufuata Yesu siku moja usiku kwakujificha kwasababu alijua iposiku atakufa na baada ya kfa yapo maisha yanayoendelea bila mwili huu wa nyama, Yesu akamwambiaamini,amini,nakuambia,Mtu asipozaliwa mara ya pili,hawezi kuona ufalme wa MUNGU.......... Yohana 3;2-6 Ukisoma mstari wa 4 Nikodemu akauliza Awezaje mtu kuingia kwenye tumbo la mama yake akiwa mzee akazaliwa tena kwa upya?

Ukisoma mstari wa 5 Yesu akajibu,Amini,amini,nakuambia,mtu asipozaliwa kwa maji nakwa Roho,hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu. Mstari 6 anasema kilichozaliwa kwa mwili ni mwili nakilicho zaliwa kwa ROHO ni roho.Yesu anaainisha vzuri kuwa kinachozaliwa kwa mwili ni mwili.Mwili hauwezi kumpendeza MUNGU hatakidogo na mwili unatabia yake,ukisoma Rum 3;6 utaona vile mwili unavofikiria juu ya mauti na unauadui na MUNGU. Mungu ni roho ukisoma katika Yohana 4;24 kuwa Mungu ni ROHO.
Ukirejea katika yn3;3-6 MUNGU anamanisha kuwa ROHO ambaye ni MUNGU ukisoma Yn 4;24 anazaa Roho wengne, kwahiyo mwili utabaki kama kawaida lakini ROHO yako inakuwa imezaliwa upya yaani kama unaumri wa miaka 25 utabaki na umri wako lakini Roho ni changa ndo imezaliwa.Petro anaeleza katika walaka wake 1petro2;2 kama watoto wachanga waliozaliwa sasa.......manaake anaelezea kwa mtu aliyeokoka sasa anatakiwa aweke bidii ili akue sikwamba hajakuwa la hasha! amekuwa kiufahamu na kiumbo na kielimu lakini Roho yake ndo imezaliwa ni chaga.Paulo pia ameeleza kuhusu hali hizi za kukua kiroho waebrania 5;12-14..waefeso4;14 paulo ameeleza vizr katika msitari huu wa waefeso 4;14 ili tusiwe tena watoto wachanga tukitupwa huku na huku........

Mungu anaelezea kuwa wanahudumu kazi ya bwana hapa duniani ni Roho...waebrania1;14 anasema Je! hao wote si roho wantumikao,wakitumwa kuwahudumu wale watakaorithi wokovu? kwahyo wewe unayemtumikia MUNGU ni roho wa bwana.

Roho ni tabia,matendo ..tunaposema mtu anaroho mbaya maanayake anatabia mbaya pia anamatendo mabaya.Unaposema mtu huyu ana roho kama ya mama yake maanaake anatabia kama ya mama ake na anamatendo kama ya mama ake.Tukisema kuwa huyu mtu anaroho ya wizi maanaake huyu mtu anatabia ya wizi pia ni mwizi.Pia unaposema kuwa mama huyu ni mzinzi maanaake anaroho ya uzinzi pia anatabia ya uzinzi,unaposema kuwa huyu ni mlevi ni sawa nakusema kuwa huyu anabia ya ulev,na anaroho ya ulev
Ukisema mtu huyu anaroho nzuri maanaake matendo yake tabia yake ni nzuri..
Yesu anawambia mafarisayo kuwa safisheni kwanza ndani alafu baadae msafishe nje anamaana kuwa mtu azaliwe kwanza ndani na mwili wote utafanywa upya

Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa kitokacho ndicho kimutiacho mtu unajisi....mathayo15;11-18 alafu anasema moyoni hutoka mawazo mabaya,uuaji,uasherat; wivi,ushuhuda wa uongo na matukano.
Kwahiyo mtu anapobadilika au anapozaliwa tunaanza kuona mabadiliko ya tabia.Kwa maana hii utasikia watu wakisema hakuna kuokoka ukiuliza kwanini una ambiwa wapo walokole wanotenda dhambi ukweli ni kuwa hao bado hawajaokoka ni wanafiki,lakini nadhani utakuwa umeona kwa baadhi ya watu ambao hapo awali walikuwa na tabia mbaya lakini baada yakuokoka leo wamebadilika hadi unasikiawatu wakisema kwakweli mdada huyu,mkaka huyu,baba huyu amebadilika.Alikuwa anapenda wanawake lakini asaivi ameacha.
Kwahiyo basi mtu akiwa ndaini yakristo amekuwa kiumbe kipya yakale yamepita tazama yamekuwa mapya ....2kor5;17

MUNGU awabariki sana.

By Fadhili  Malaki
 
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12