Maombi ni NENO ambalo watu wengi ambao wanalitumia hulitumia tofauti na maana yake halisi ilivyo...
MAOMBI si kukariri maneno Fulani na kuyasema huku umefumba macho au umepiga magoti..Maombi ni zaidi ya kufanya haya!
Kuna maombi ya namna mbalimbali,ambayo yanaombwa kwa jinsi tofauti,kwa kufuatana na imani ya mtu.Lakini yote yanaitwa maombi..
Maombi ni mazungumzo kati ya mwombaji na yule anayeombwa,awe ni MUNGU,shetani au mtu yeyote yule...
Na kwa sisi WAKRISTO,maombi ni mazungumzo kati ya MKRISTO NA MUNGU WETU,KWA NJIA YA YESU KRISTO,MWANA WA MUNGU,BWANA NA MWOKOZI WETU...
MUNGU yule ambaye wana wa ISRAEL,waliogopa hata kusogea mahali alipo,sisi tumepewa nafasi ya kumsogelea MUNGU KWA DAMU YA YESU KRISTO (Waebrania 10:19,20)
Ni tabia ya MUNGU kujibu maombi ya wateule wake,kama ahadi zake zinavyotueleza.
Watu wengi wanaongea na MUNGU kwa njia ya maombi,lakini huwa hawako tayari kusikiliza MUNGU anawaambia nini.Wengine wanazungumza na MUNGU bila ya kuwa na uhakika ya kuwa watajibiwa.
Lakini ukisoma maandiko MATAKATIFU,na ahadi za MUNGU,utaona mahali pote alipowaambia watu waombe ameahidi kujibu.kwa mfano amesema hivi..
"Niite,nami nitakuitikia,nami nitakuonyesha mambo makubwa,magumu usiyoyajua" (Yeremia 33:3)
"Ombeni,nanyi mtapewa........kwa maana kila aombaye hupokea" (Mathayo 7:7)
Comments