![]() |
Jiji la Jerusaleem ambapo Yakobo Mwana wa Zebedayo aliuwawa wakati akihubiri habari za Kristo |
Maisha ya wanafunzi wa YESU KRISTO na wajibu
waliopewa na BWANA YESU baada yeye kuondoka. Lengo hasa ni kutuwezesha
kujua namna ambavyo waliotutangulia katika wokovu walivyokutana na
changamoto ili na sisi tupige mbio zaidi katika kuutangaza ufalme wa
MUNGU. Hii ni kwa kua tumepokea hiki kijiti toka kwao hivyo na sisi
tunayo safari yetu katika kristo YESU. Habari kuhusu Maisha ya Mitume
hao na namna walivyosambaa duniani kote mpaka vifo vyao zinapatikana
katika vitabu vilivyoandikwa katika kanisa la Kwanza. Schumacher ni
Mwanahistoria wa kanisa aliyefanya utafiti kuhusu maisha ya mitume
(wanafunzi wa kristo) na hivi ni namna ambavyo mitume hao
walivyokuimbana na misukosuko katika kumtangaza KRISTO YESU.
MATHAYO
Mtumishi Mathayo yeye aliuwawa kwa upanga akiwa katika nchi ya Ethiopia
MARKO
Marko
yeye alifia katika mji wa Alexandria nchini Misri mara baada ya
kuburutwa na Farasi katika mitaa ya mji huo mpaka mauti ilipomfika.
LUKA
Yeye aliuwawa huko nchini ugiriki alipokua akitangaza habari za kristo
YOHANA
Yohana
yeye aliwekwa katika kikaango/sinia kubwa lenye mafuta yaliyochemshwa
na kwa Neema ya ajabu akafanikiwa kutoka katika mauti iliyokua
ikimkabili.Baada ya kutoka katika kisiwa cha Patmo alipokua amefungwa na
kufanikiwa kuandika kitabu chaUFUNUO akiwa kisiwani hapo, alikuja kua
Askofu wa Edessa ambayo sasa inajulikana kama nchi ya Uturuki.Yohana
alifariki nakiwa mzee sana na ni mwanafunzi wa kristo pekee aliyekufa
pasipo mateso.
PETRO
Yeye
baada ya kukamatwa akieneza habari za Kristo, aliamriwa asulubiwe
kichwa chini miguu juu kama Kristo Yesu, Lakini petro aliwaomba watu hao
wamsimsulubishe kama namna ambavyo kristo alifanyiwa kwa kua Petro
alisema yeye hana hadhi ya kusulubishwa kama Bwana wake. Ndipo
walipoamua kumsulubisha kinyume na Kristo, hivyo Petro akasulubiwa
kichwa chini miguu juu mpaka mauti ilipomfika.
![]() |
Ramani ya jiji la Jerusalem |
YAKOBO
Yeye
alikua kiongozi wa kanisa la Yerusaremu, alitupwa katika bonde la mita
mia moja pale alipokataa kuikana imani ya Kristo.Walipogundua kua hajafa
adui zake waliamua kumpiga kwa rungu mpaka kufa. Bonde hilo ni lile
ambalo Shetani alimuonyesha Yesu wakati akimjaribu kule nyikani.
YAKOBO MWANA WA ZEBEDAYO
Yeye alikua mvuvi kabla hajaitwa na kristo yeye iliuawa katka jiji la Jerusalem
BATHOLOMAYO
Alijulikana
pia kwajina la Nathania ,alikua ni mmishionari katika bara la Asia,
Alishuhudia habari za kristo katika nchi ya Uturuki.Aliuawa kwa
kukaangwa.
ANDREA
Yeye
alitundikwa msalabani kwa mfumo wa X katika mji wa Patras nchini
ugiriki baada ya kuteswa ipasavyo na askari wapatao saba,kasha
wakamfunga msalabani with cords to plorong his agony.Wafuasi wake
walisema wakati wanampeleka msalabani,Andrea alisema “Nina uamuzi
udumuo na niliutegemea muda huu wa furaha”. Aliendelea kuhubiri akiwa
hapo msalabani kwa siku mbili mpaka pumzi yake ya mwisho ilipokoma
THOMASO
Yeye aliuawa kwa kuchomwa na mkuki huko India alipokua katika moja ya safari zake za kiumishieni kwa ajili ya kufungua kanisa.
![]() |
Geti la kuingilia mji wa Damaskus huko Israel |
Comments