Mambo gani yalitokea Baada ya Yesu kupandishwa Msalabani ?




  1. PAZIA LA HEKALU LILIPASUKA ; hii inamaanisha ushindi mkubwa wa mkristo. Pazia kupasuka kunamaanisha kuwekwa huru. Kuondolewa kwa vizuwizi vyote mbele yako.
Ikumbukwe kuwa, pazia, liliwekwa kuwazuwia watu wasiingie wala hata wasiweze kupaona patakatufu pa patakatifu. Mahali hapa,aliingia kuhani peke yake. Baada ya pazia kupasuka, kizuwizi kiliondolewa kwa yeyote kufika hapo. Kifo cha Yesu msalabani, kimeondoa dhambi zako, kimekupa kibali cha kunena kwa lugha kwa raha zako.

  2. TETEMEKO KUBWA; Tetemeko hili,liliambatana na giza nene,ikiwa ni ishara ya nguvu kubwa yenye utisho wa ajabu sana. Tetemeko hili, lilionesha uwezo ulio juu ya uwezo wote,nguvu inayozidi nguvu zote. tetemeko hili, lilidhihirisha kuwa kweli Yesu ni mwana wa Mungu, na yule mlinzi alishuhudia kwa kinywa chake. Hata leo, maisha ya mtu aliyeokoka, yanapaswa kudhihirika mbele za watu wote, kuwa kweli kuna nguvu mpya na uweza wa ziada ndani ya mtu aliyeokoka.

 3. MAKABURI YALIFUNGULIWA.  baada ya Yesu kushuka kuzimu, watakatifu walio lala  wakaamka, wakatangaziwa uzima upya. Wakawa katika uzima wa milele pamoja na Yesu ; baada ya Yesu kumnyang’anya funguo za kuzimu ibilisi, akawa hana mamlaka tena, uwezo wake wote na mamlaka yote akawa amenyeng’anywa. Nguvu ya msalaba, ni nguvu inayoshinda mauti. Yesu ni zaidi ya mateso yote, ni zaidi ya kifo, ni zaidi ya magonjwa, ni zaidi ya kukata tamaa, ni zaidi ya umasikini, nguvu ya msalaba iko juu ya laana na vifungo vyote.

  4.TAMKO LA USHINDI LIKATOLEWA, tamko la ushindi lilitolewa rasmi Yesu aliposema (IMEKWISHA). Kauli ya Yesu iliashilia kufikia mwisho kwa mateso yote, uonevu, laana, mikosi na vifungo vyote. Kauli ya Yesu inatufundisha nini aliposema Imekwisha? Kwa mtazamo wa ndani zaidi, ilimaanisha, kukamiliaka kwa kazi yake iliyomleta duniani ambayo ilikuwa ni ukombozi. Kumweka huru kila mtu ili asipotee, bali awe na uzima wa milele. Kwa maelezo mengine tuseme kuwa, Msalaba wa Yesu, ulibadirisha Historia ya Ulimwengu wote na kuweka utamaduni mpya.

  5. MWSAMAHA WA DHAMBI ULITOLEWA; kupitia mauti ya msalaba wa Yesu, msamaha wa dunia ulitangazwa. Kupitia kifo cha msalaba, toba kwa ulimwengu ilipatikana. Kifo cha msalabani, kinatupa maji ya uzima, kinatupa pumziko la kweli, kina tuhesabia haki. Wakati wayahudi walidhani wanakomesha, kumbe agano la Mungu linatimia kwa ulimwengu, kuwa Mtu hatafika mbinguni ila kwa njia ya Yesu Kristo. Kupitia kifo cha Yesu, mlango wa kuiendea mbingu ilifunguliwa wazi kwa wote wampokeao na makao yao yakaanza kuandaliwa tangu hapo. Hata leo, ukiokoka, makao yako yanaanza kuandaliwa leo.

MUNGU akubariki.

Comments