Maombi ya ushindi Katikakati ya vita


Kutana na Mtu wa Mungu pale katika Hema ya Kinabi Nyankumbu Mkoani Geita Tanzania,

USHINDI KATIKATI YA VITA
Utangulizi:              
Kila mwanadamu anayeishi hapa Duniani kwanza ifahamike lazima ana Adui anayepambananaye kila siku Hayo mapambano ndiyo Ninayoyaita Vita lakini Baada ya Mungu kunipa Mafunuo Haya ndipo nikafahamu pamoja na vita tunayopambana kila siku,Ushindi unaweza kuoatikania katikati ya Vita, Yesu kristo ni Bwana wa vita, na Vita vyote vinaanzia Rohoni, Bunduki Haiuwi bali anayeuwa ni Mtu,
Waefeso 6:12, kushindana kwetu si juu ya Damu na mwili,
Ushindi maana yake ni nini?
Maana ya Ushindi ni kufanikisha jambo ulilokuwa umekusudia kulifanya likafanikiwa maana yake umeshinda ugumu au kizuwizi,hadi kufanikiwa, kushinda,kufaulu,kupita, ni maana zinazoweza kukusaidia
Vita ni Mapambano ya jambo flani amkubaliani nalo katika pande mbili, maana vita ina pande Mbili ila siku ya siku lazima Ushuhudiwe ushindi upande Mmoja,
Fahamu kuwa Dui yako Mkuu Niibilisi wale unaokutana nao katika uwanja wa mapambano ni wafuasi,watumwa,watenda kazi,maaskari ila jemedari  wao yupo nyuma yao,
Nilifundisha siku mmoja kuwa ibilisi ni yule yule wa kila siku ila anajifunuwa au kujidhihirisha kwa nanma tofauti tofauti kupitia Matukio Mbali mbali,
kwa Mfano ukifuatilia Habari ya Ayubu, utagunduwa Matukio yote yaliyokuwa yamempata Ayubu yaliruhusiwa na ndiyo kona Ibilisi alijifichia kutaka kumtatiza na kumtenganisha Ayubu na Mungu,
Hatuwa ya kwaza ya Ushindi katikati ya Vita
·         Usikubali kutenganishwa na Mungu kwa Namna yeyote ile
·         Usikubali kutoa siri zako  kwa Mtu yeyote
·         Usikubali kuruhusu uwoga ukaingia Ndani ya Moyo wako
·         Ondowa Mitego ya adui kwa umakini ujasiri huwa unaondoa Mitego  iliyotegwa na Maadui
·         Mtumaini Bwana Mungu wako siku zote nawe Utakuwa salama,
Mithali 29:25 Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye Bwana atakuwa salama.

katika vita inatumika Nguvu ya kila Namna Ilimradi ushindi upatikane sasa watu wengi wanaenda vitani Bila Nguvu ya kutosha kwakuwa kunakila ainaya mbinu na vifaa vitakavyotumika na wewe lazima ufahamu kuwa unatakiwa uende na aina gani ya viifaa,
Mambo ya kuzingatia katika kupata ushindi,
v  Lazima umfahamu Adui yako vizuri si kwakusontewa kidole,
v  Lazima ufahamu Kwa uhakika Maskani ya adui yako ni ipi,
v  Lazima ufahamu Nguvu yake ni kubwa kiasi gani na ni ipi,
v  Lazima ufahamu Mbinu zake,
Ndugu yangu  usijaribu vita ya kupoteza yaani vita unayojuwa utashindwa lakini wewe unalazimisha kupambana ,na pia usianzishe vita unayoona kuwa utashindwa maana itakumaliza,
Msome adui yako vizuri kabila ya kuingia Uwanjani, jitasmini wewe mwenyewe juu ya mapambano, kisha hakikisha Una Nguvu ya kutosha kupambana ndipo uanze vita,
Matendo ya Mitume 1:8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
Mtu yeyote Jasiri lazima kuna kitu anachokitegemea au kuna Nguvu anayoitegemea yamkini ni Mali,fedha, Madaraka,yaani Mmlaka,Nguvu za Mungu,Nguvu za Giza,
Matendo ya Mitume 4:13Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.
Usiende vitani Peke yako Nenda na Bwana wa Vita Yesu Kristo Mwana wa Mungu,
Matendo ya Mitume 5:29B Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.
Ushindi katikati ya Vita Ni kwamba  utaaza kuuona ushindi kwanzia katikati kwakuwa aliye vitani na wewe ni Mkuu sana Yeye alishinda vita alishinda mauti,aibu,Mateso, matatizo unayoyapitia siyo kushindwa bali ni Dalili Ukombozi na ushindi Katikati ya hilo tatizo,
Tatizo ulilo nalo ni vita Lazima lishugulikiwe likiachwa linasababisha Mauti
Utasa wako ni Vita Lazima ushugulikiwe
Umaskini wako Ni vita lazima Ushughulikiwe  angalia Upande wako yupo nani Mshindi au Aliyeshindwa, na Asikilizwe Nani? Ibilisi au Mungu?
Tafakari: Ukitembea na Mtu aliyeshindwa  atakupa wewe Sababu ya kushiwa na Ghafla ukija shutuka Umishindwa kila jambo, Mbaya sana,
Tito 2:15Nena maneno hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote.
  • 1 Petro 2:12 Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.

Pata Mosomo mengine mengi ya Mtu wa Mungu Nabii Samson

Upenyo wa kumiliki

siri kuu tatu za kutunza siri zako zote

Nguvu ya kinya 

Ushindi katikati ya vita

jifunze kusamehe,

Hatima iliyopindishwa

yapo mengi unaweza ukaagiza ukapata

 0756 809 209 Mtu wa Mungu anaptika wakati wote yupo hewani

 

 

Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12