Mauaji ya Padre Mushi Zanzibar Mtuhimiwa wa mauaji apewa dhamana


Mahakama kuu Zanzibar  mapema leo hii imemuachia kwa dhamana Omari Musa Makame ambaye ni mtuhumiwa katika kesi ya Mauaji ya Padre Mushi aliyeuwawa February 17 mwaka huu 2013 huko Zanzibar kwa kupigwa Risasi wakati akielekea kwenye Ibada siku ya jumapili 
Mtuhumiwa wa mauaji ya Padri Evarist Mushi, Omar Mussa Makame (35) aliyevaa shati la rangi ya wardi akiwa Mahkamni kwa mara ya kwanza.
Mtuhumiwa wa mauaji ya Padri Evarist Mushi, Omar Mussa Makame (35) aliyevaa shati la rangi ya waridi akiwa Mahakamni

katika Dhamani hiyo iliyotolewa leo hii wadhamini  wawili wamesaini mahakamani na kutoa dhamana ya pesa taslim kiasi cha Laki 5 kila mmoja
Padre Mushi aliuawa kwa kupigwa risasi Februari 17 mwaka huu wakati akienda kuongoza ibada ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Teresia liliopo Beit el Raas nje kidogo ya mji wa Zanzibar na mtuhumiwa alitiwa mbaroni na Polisi tangu Machi 17 mwaka huu.
Chanzo: Mjapinc blog
 
 
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12