 |
Askofu
Mpya wa jimbo la Dar es salaam Thomas Dige akizungumza wakati ya hafla
ya kumsimika rasmi akichukua nafasi ya Askofu Elly Mwende
aliyestaafuJimbo hilo la Dar es salaam linajumuisha mikoa 9 ya
Serikali ambayo ni Dar es salaam, Lindi, Pwani, Mtwara pamoja na mikoa
Miwili ya Pemba na mikoa mitatu ya Unguja. |
Mchungaji Thomas Dige wa kanisa la Pentecostal Assemblies
of GOD , Mbezi beach amesimikwa rasmi kuwa askofu wa jimbo la Dar es
salaam na Zanzibar wa kanisa la Pentecostal Assemblies of GOD( P A G).
Nafasi ameipata baada ya uchaguzi mkuu wa kanisa hilo ambapo anachukuwa
nafsi ya Askofu Elly Mwende ambaye amestaafu. Askofu Mwende amekuwa
askofu wa jimbo hilo kwa muda wa miaka 12 yaani toka mwaka 2001 hadi
mwaka huu wa 2013, amefanya mengi sana katika jimbo hilo kwani kipindi
anaingia madarakani alikuta makanisa 4 tu yakiongozwa na kanisa mama la
DPC yaani Dar es salaam Pentecostal Church, lakini hadi anastaafu leo
ameacha makanisa 29 katika jimbo hilo.Askofu Dige ambaye amechaguliwa
kuwa askofu kabla ya cheo hicho kipya alikuwa ni katibu wa jimbo wa
kanisa hilo. Pia amechaguliwa askofu msaidizi ambaye ni mchungaji Noel
Tabejo kutoka Mkoa wa Pwani na katibu mkuu wa jimbo Mchungaji Gradius
Theonest wa Tegeta PAG . licha ya viongozi hao wamechaguliwa pia
waangalizi wa kanda ambapo Mchungaji Amos Lukanula amekuwa mwangalizi
upande wa Unguja na Pemba pamoja na wengine katika kanda zingine za
Lindi na Mtwara. na wajumbe ni pamoja na Mchungaji Elly Boto wa Kawe
Pentecostal Church (KPC) . Kiongozi mkuu kutoka ngazi ya Taifa na
msimamizi alikuwa ni Katibu mkuu wa PAG
Tanzania na ambaye pia ni Mkuu wa chuo za Biblia cha Mwanza, ndugu
Primus Ngeiyamu.zifuatazo picha za tukio hilo la kumpata askofu mpya
pamoja na wasaidizi wake.
 |
Katibu mkuu wa kanisa la PAG na mkuu wa chuo cha Biblia Mwanza Mchungaji Primus Ngeiyamu ambaye ndiye alikuwa msimamizi wa tukio hilo akiwapa nasaha viongozi wapya wa jimbo la Dar es salaam na katikati ni askofu aliyestaafu, Elly Mwende |
 |
Baadhi ya wachungaji na maaskofu wakisikiliza neno la MUNGU kutoka kwa Mchungaji Primus Ngeiyamu |
 |
Kutoka kushoto, askofu msaidizi Noel Tabejo, Askofu Thomas Dige na askofu aliyestaafu Elly Mwende |
 |
Askofu mstaafu Elly Mwende akizungumza machache ikiwemo mafanikio rukuki wakati wa uongozi wake kabla ya kukabidhi rasmi madaraka kwa askofu Thomas Dige |
 |
Wachungaji, wakuu wa idara wapya wa kanisa la PAG jimbo la Dar es salaam wakiombewa na kuwekwa wakfu kwa kazi ya MUNGU |
 |
Kutoka kushoto, Askofu mpya wa jimbo la Dar es salaam Thomas Dige, katikati ni Mchungaji Paul Safari na kulia ni Askofu aliyestaafu Elly Mwende wakati maombi yakiendelea. Jimbo hilo la Dar es salaam linajumuisha mikoa 9 ya Serikali ambayo ni Dar es salaam, Lindi, Pwani, Mtwara pamoja na mikoa Miwili ya Pemba na mikoa mitatu ya Unguja. |
 |
Askofu Thomas Dige baada ya kuwa askofu mpya wa jimbo la Dar es salaam |
 |
Askofu anayestaafu Elly Mwende akimkaribisha rasmi askofu mpya Thomas Dige |
 |
Askofu mpya Thomas Dige, askofu aliyestaafu Elly Mwende na Mkuu wa chuo cha Biblia Mwanza Primus Ngeiyamu wakimuombea Mchungaji Amos Lukanula ambaye ndiye mwangalizi wa kanisa hiyo kule Unguja na Pemba. kanisa lake liko Chukwani , Zanzibar |
 |
Askofu msaidizi Noel Tabejo akiombewa. |
 |
Mkurugenzi mpya wa vijana wa jimbo akiombewa |
 |
Mkurugenzi mpya wa Wamama wa jimbo akiombewa |
 |
ilikuwa ni shangwe , hapa ni Pastor Mpapai akiimba |
 |
Askofu Thomas Dige akimwombea Mchungaji Paul Safari ambaye ni mjumbe |
 |
Baada ya hayo yote ilikuwa ni kula na kula na kushiba katika jina la YESU |
Comments