MKRISTO KAMA SIMBA *sehemu ya pili*

na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe....

Karibu tujifunze pamoja,
Kupitia fundisho hili litakupa ujasiri wa kupambana na adui katika ulimwengu wa roho kwa jina la Yesu Kristo na utashinda tu dhidi ya adui zako.

Kumbuka katika sehemu ya kwanza tuliishia kusoma andiko moja kutoka Ufunuo wa Yohana.
Tusome tena;

"Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, usilie ;tazama,Simba aliye wa kabila ya Yuda,Shina la Daudi,Yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu,na zile muhuri zake saba." Ufunuo 5:5

Haleluya..

Neno likamjia Yohana na kumuambia USILIE maana yupo mmoja,
Yeye aliyeshinda zaidi ya kushinda,
Yeye mwenye nguvu,
Yeye ambaye vitu vyote viliumbwa kwa ajili yake,
Naye huyo ndiye SIMBA WA KABILA LA YUDA.

Nami leo hii ninakutangazia, nikikuambia USILIE,
Ikiwa mwanadamu ameshindwa,
Ikiwa daktari wako ameshindwa,
Ikiwa waliokusaidia wameshindwa,
Lakini yupo Bwana wa mabwana,
Yeye ni Simba wa kabila la Yuda,Yesu Kristo wa Nazareti,HAJASHINDWA

Pale mwanadamu aliposhindwa ndipo BWANA MUNGU anaanza..
Na leo anakuambia kwanza USILIE.

Anakuambia ``usilie" sababu wewe uliyempokea Bwana Yesu,Simba aliye shina la Daudi,wewe mmoja mwenye haki,unafanana naye,na ikiwa unafanana naye basi hutakiwi kulia,
Sababu Simba huwa halii,
Bali hunguruma.

Wewe uliye na Bwana Yesu,U mtoto wa kifalme,hauitajiki kulia Bali unahitajika kunguruma,
Maana hata mfalme haliagi,bali hunguruma,
sikia ;
utakaponguruma ujue hakuna atakaye bakia,Bali wale wote walio kinyume nawe lazima watimue mbio. Sababu wewe U kama Simba.

Haleluya...

Unapokutana na Simba kwenye himaya zake,wewe uliyeingia katika himaya yake ndio unafanyika adui kwake,hivyo ni wewe ndio utakayekimbia mbele zake,

Alikadhalika shetani anapokutana na Bwana Yesu,shetani ni lazima akimbie mbele za Bwana Yesu.
Wewe uliye kama Simba,
Adui ajapo kwako,inampasa adui akimbie mbele zako. Sio wewe umkimbie,Bali adui ndio akukimbie.

Adui hukimbia sababu kwanza alishapigwa,
Pili hana uwezo tena wa kushindana na wewe uliyembeba Simba wa kabila la Yuda.

Usilie juu ugonjwa uliokuwa nao,
Usilie juu ya kukosa Pesa,
Usilie juu ya kudhulumiwa,
Usilie kwa kukosa mtoto,
Usilie kwa kukosa mume,
Usilie kwa kukosa mke,
Usilie juu ya kusingiziwa,

Bwana wa majeshi,Simba wa kabila la Yuda,Bwana Yesu Kristo Yu HAI,
Bwana Yesu amelipa gharama pale msalabani
Tayari amekupigania kwa yote hayo,
Ni wewe tu kufungua moyo ili siku ya leo apate kukuponya.

* Leo ndio mwisho wa hayo mateso,maana Bwana yupo upande wako wewe usomaye jumbe hii.

Jitambue U kama Simba katika kila hali upitayo.Kamwe usisahau hilo. Bwana hatakuacha.
Tazama andiko hili;

"Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu;
Bali wenye haki ni wajasiri kama simba" Mithali 28:1

Waovu wote,hukimbia hata wasipofuatiwa na mtu,umuonapo muovu basi usiogope maana yeye mwenyewe ni lazima akimbie mbele zako.

Chukulia mtu muovu/mvunja sheria za barabarani;pale amuonapo askari wa barabarani jinsi atakavyokimbia mbele yake hata kama hajafuatiwa na huyo askari.

Sasa huo ni mfano mdogo sana,kwani kwa habari ya mambo ya kiroho waovu hukimbia mbele za wenye haki.

Waovu kamwe hawawezi kuchangamana na wenye haki,maana wenye haki ni kama simba,yaani ile identity yao haifanani kabisa,hivyo hawawezi kutembea pamoja.

Biblia iko wazi kabisa katika andiko hili,
Maana imesema kwamba;
Mwenye haki ni JASIRI kama SIMBA.

Ooh,kumbe!

Mwenye haki pekee ndio anafananishwa na simba,tena huwa ni jasiri.
Kwa lugha nyingine hapo ni sawa na kusema kwamba;
Mtu mwenye haki hufanana na simba wa kabila la Yuda.

Sasa unisikilize mpendwa,
Kuwa mwenye haki ndio namba moja,ili ufanane naye Yeye mwenye haki.
Kuwa mwenye haki ni mchakato wa maisha ya utauwa.

Mtu hawi mwenye haki kwa kujiita kwa maneno matupu kama tulivyozoea,Bali ni mfumo wa maisha.
Nasema kuwa mwenye haki ni mfumo halisi wa maisha ya UTAUWA.

Wakristo wengi hawafanani na Simba wa kabila la Yuda,Yeye ambaye ni Shina la Daudi kwa sababu sio wenye haki.

ITAENDELEA...

Leo nataka niombe na mtu mmoja aliyeelewa ujumbe huu,
Yamkini yapo mateso unayopitia,
Yamkini umekwama sehemu fulani,
Labda yawezekana umekata tamaa,Lakini kumbuka neno la leo lisemavyo;
USILIE yupo Bwana Yesu atakayekushindia.

Kwa maombezi;
*0655-111149.

Usikose fundisho lijalo mahali hapa,

UBARIKIWE.

 
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12