MKRISTO KAMA SIMBA*sehemu ya mwisho*

na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe...
Heri ya Christmas mpendwa...

Natumaini U mzima wa afya na umesherekea vizuri sikukuu ya kuzaliwa kwa mwokozi wetu.
Karibu tena tuendelee kupata maharifa ya ki-Ungu kupitia fundisho hili.

Kuwa mkristo ni kufanyika mfuasi wa Kristo.Ikiwa na maana kwamba kama vile Bwana Yesu alivyoishi,nasi tulio wakristo yatupasa kuishi hivyo.
Yeye Bwana Yesu aliuvaa mwili kwa kutuonesha kielelezo cha namna gani mkristo aishi.

Sasa leo ninakufananisha kama Simba wewe unayeishi kama vile Bwana Yesu alivyoishi,maana tuliona yakwamba ;Yesu mwenyewe ni simba wa kabila la Yuda nawe ikiwa umejiungamanisha naye vizuri, U kama simba wa kabila la Yuda,shina la Daudi.

Unafanana na simba kwa ule ujasiri kama Simba aliokuwa nao,Tena Mkristo hufanana kama Simba kwa ile nafasi ya UTAWALA kama vile alivyo simba mwituni, yakwamba yeye simba ni mfalme wa mwituni.

Tusome tena andiko hili;
"Utisho wa mfalme ni kama ngurumo ya simba;
Amkasirishaye huitenda dhambi nafsi yake." Mithali 20:2

Haleluya...

Biblia inatuambia habari nzuri sana hapa katika hili andiko,tazama ile hali ya utisho wa mfalme imefananishwa kama mngurumo wa simba.

Mkristo aliyejipanga sawa sawa,angurumapo uwa na utisho wa kifalme ambapo huo mngurumo wake ni kama wa simba angurumapo.

Simba akinguruma basi watu hukimbia.
Chukulia ndio unasikia mngurumo wa simba,ukweli ni kwamba utakimbia tu.

OK,
Sasa mkristo huwa na utiisho wa ajabu ambao hufanana kama ngurumo ya simba.
Maana ipo nguvu ndani yetu ingurumayo yenye utiisho.

Mkristo ninayemzungumzia hapa sio yule mkristo muumini tu,Bali ni mfuasi kamili wa Kristo Yesu,mkristo aliyeokoka,mwenye kujaa Roho mtakatifu,anayeishi kwa kuyafanya mapenzi ya Mungu Baba. Mtu wa namna hii huwa ni mfalme,ambaye utisho wake ni kama ngurumo ya simba.

Haleluya...

Ninachokitafuta hapa ni kukupa ufahamu yakwamba ipo nguvu ya ajabu ndani yako wewe uliyempokea Bwana Yesu Kristo.
Nguvu hii ipo,lakini huitajika kuchochewa ili ifanye kazi yake ipasavyo.

Imefika wakati sasa yakupasa ujitambue yakwamba U kama simba.

Simba haliagi bali hunguruma tu,hata wewe haikupasi kulia bali upatapo shida nguruma kwa Bwana,
Ngoja nikupe mfano huu;

"Siku moja nilikuwa mjini,Dar (Posta ya zamani karibu na bank ya NBC).Mbele yangu nikaona umati wa watu wamezunguka,wakawa kama wanatazama jambo fulani hivi.
Nami nalikuwa natembea kwa miguu,hivyo nikaamua kupita mbali kidogo maana sikutaka kujua ni kitu gani kilichokuwa kinaendelea;
lakini gafla ndani yangu nikashuhudiwa nisogee karibu ili nami nijionee yanayoendelea pale.

Nilipofika nikamuona mdada mmoja aliyekuwa amambeba mtoto mdogo,akiwa anapiga kelele huku akilia kwa kusema ;
"moto moto moto ,nalipukiwa na bomu"

Gafla nilipozidi kuusogelea ule umati,nikapata nafasi ya kuonana uso kwa uso na huyo dada,
Gafla akanyamaza kimya,kumbe zilikuwa ni nguvu za giza zilizokuwa zinamtesa,mapepo yalimuingia yakamsumbua sana,alitupiwa uchawi.

Lakini yale mapepo yakakimbia mbele yangu maana ule utisho uliokuwa ndani yangu ni mkubwa kuliko uwaye wote,utiisho kama ngurumo ya simba.

Watu waliokuwapo hapo wakashangaa sana,maana wengine wao waliniita mchungaji,wengine wakaniona kama mungu mdogo,wengine wakaniita mtu wa Mungu.
Maana sikuomba Bali nguvu ya giza ilikimbia yenyewe mbele ya utisho uliokuwa ndani yangu,ambao ni kama ngurumo ya simba "

"Maana mimi natakuwa kama simba kwa Efraimu,na kama mwana simba -kwa nyumba ya Yuda;mimi,naam,mimi nitararua,kisha nitakwenda zangu;nitachukulia mbali , wala hapatakuwa na mtu wa kupokonya." Hosea 5:14

Neno linasema yeye atakuwa kama simba,ikiwa na maana ya UTIISHO wake utakuwa ni wa kuogopwa. Anazidi kusema kwamba ATARARUA NA WALA HAPATAKUWA NA MTU WA KUPOKONYA.

Ukiweze kujitambua ya kwamba U kama simba,
Na ikiwa utaweza kuishi kama simba,basi hakuna cha kukutisha,
Iwe ni ugonjwa,
Iwe ni hali ngumu ya maisha,
Yaani iwe iwavyo hakuna cha kukutisha maana Bwana ndiye atakushindia hayo yote.

Unajua ukiwa kama simba hata vinyamkela,wachawi,waganga wote hujua yakuwa wewe ni kama simba,hivyo ni lazima wakimbie mbele yako.
Na ndio maana tunasoma ;

"Aliinama,akalala mfano wa simba,
Na kama simba mke;ni nani atakayemstusha?
Na abarikiwe kila akubarikiye,
Na alaaniwe kila akulaaniye."
Hesabu 24:9

Nakutakia sikukuu njema ya Christmas na mwaka mpya.

Kwa mawasiliano,
0655-111149

UBARIKIWE.

MWISHO.
 
 
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12