![]() |
Mchungaji Josephat Gwajima, Ufufuo na uzima |
Baada ya mikutano iliyovunja rekodi kwa idadi ya watu yaani Arusha,
Moshi na Tanga; sasa kanisa la Ufufuo na Uzima linahamishia mikutano
yake mkoani Morogoro ambapo Mchungaji Gwajima ambaye pia ni mchungaji
kiongozi wa kanisa hilo anatarajiwa kuhubiri kwa siku nane mfululizo.
Pamoja Mchungaji Gwajima atafuatana na timu ya watendakazi zaidi ya mia
tatu na waimbaji maarufu wa injili kama Flora Mbasha, John Lisu, Jackson
Benty na Mwanamapinduzi Band.
Mkutano huo wa kwanza kufanyika Morogoro kwa kanisa la Ufufuo na Uzima
unatarajiwa kushuhudia misukule wakirudi, wagonjwa wakipona, viwete
wakitembea na mambo mengine mengi ya ajabu.
![]() |
Hapa ilikuwa ni mkutano wa Tanga siku chache zilizopita |
![]() |
huu ni mmoja wa miujiza ambayo BWANA YESU aliitenda Arusha kupitia ufufuo na uzima |
Usikose kuhudhuria na wewe ili kupokea muujiza wako.

Comments