Mkutano mkubwa wa Ufufuo na Uzima na mchungaji Josephat Gwajima
ulihitimishwa kwa tukio la aina yake lililosisimua watu waliohudhuria
mkutano huo. Ni tukio la ajabu kutokea ikiwa ni siku moja tu mara baada
ya mkutano wa Ufufuo na Uzima kuhamia katika jengo moja maarufu mkoani
Tanga.
![]() |
Mkutano wa Mchungaji Gwajima Tanga kabla ya kuhamia katika jengo jipya. |
Akinukuu hay ya kitabu cha Shehe Falsihi wa zanzibar alisema "majini ni
viumbe vya angani ambavyo havina viwiliwili hivyo huwezi kuviona kwa
macho, lakini vinaweza kuvaa ima umbo la kifuu cha nazi au umbo lolote"
alisoma haya hiyo akieleza kuwa uislamu na ukristo wote unataja viumbe
hivi yaani majini.
Wakati somo likiendelea kukatokea jambo la ajabu ambalo kwa tafsiri ya
rohoni ilikuwa ni uthibitisho wa kile ambacho Mchungaji Gwajima amekuwa
akifundisha katika jiji hilo la Tanga.
Mchungaji Gwajima alipokuwa akizunguka katikati ya makutano ili
kuwafungua wenye vifungo, zilisikika kelele za watu zikipiga kelel kuwa
kuna mtu amevaa ushungi yupo kwenye kona ya bati. jambo ambalo lilivuta
hisia za wengi. Kwani mwanamke huyo alionekana na watu wote akiwa kwenye
bati la nyumba moja ya ghorofa pembeni mwa jengo la kuabudia.
Ni kweli kuwa kwa ghorofa lile hakuna ambaye angeweza kupanda, wala
kukaa kule juu na ukizingatia ni mwanamke. Watu wakiwa wametaharuki na
wengine kuliitia jina la Bwana ghafla mwanamke huyo akatoweka mbele ya
macho ya watu wote na kuweka hofu miongoni mwa watu wote.
NI NINI TAFSIRI YAKE?
Akiongea jumapili hii kanisani, Mchungaji Gwajima amesema jambo hili ni
udhihirisho wa kile alichokuwa anakisema; na ya kwamba yeye alimwona
mwanamke huyo kabla watu hawajamuona na kwa kuwa Mungu amekuwa amekuwa
akimwonyesha viumbe vingi vya rohoni akahisi kuwa watu hawajamuona.
Alisema, "Mungu amekuwa akinionyesha viumbe vingi vya rohoni wakati
nahubiri na mara nyingi huwa sitaki kuwatia hofu watu hivyo hukaa kimnya
bila kuwambia "
Kumbe ilikuwa ni uthibitisho wa Mungu kuwa viumbe hawa wapo na pia
wanaweza kuvaa miili ya binadamu kama vile walaika walivyovaa mwili na
kumwendea Ibrahimu na hawa wanavaa miili ili kutekeleza haja zao
duniani. Majini ni halisi lakini kwa jina la Yesu wameshindwa kabisa na
Tanga imekuja kwa Yesu.
Wakati huohuo eneo jipya la kuabudia la nyumba ya Ufufuo na Uzima -
Tanga lipo katika hatua za mwisho za ukarabati ili lianze kutumika
shuhudia pichani.
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12
Comments