NGUVU YA MUNGU AJABU INAENDELEA KPC KAWE

Moto umeendelea kuwaka katika ibaada zenye nguvu ya MUNGU katika kanisa la Kawe Pentecostal Church(KPC), Kwa mchungaji Elly Boto, Mtumishi huyu wa MUNGU, MUNGU BABA amekuwa akimtumia katika viwango vikubwa sana , kila jumapili imekuwa ni siku ya kufunguliwa kwani MUNGU ameachilia Baraka zake na uponyaji wake kwa watu wake, Leo pia kulikua na maombezi  ya wale ambao wametoa sadaka zao za shukrani kupitia hapa hapa Maisha ya ushindi blog, wale waliotuma sadaka zao moja kwa moja zimepelekwa kanisani na maombi yao yatakuwa yanaombewa kila mara , katika ibaada za mikesha na ibaada za kawaida, Kama unahitaji maombezi bure kabisa  Wasiliana nami kwa namba 0714252292, pia kama unataka kutoa sadaka yako ya shukrani katika madhabahu hii ya MUNGU aliye hai , tuma kwa namba hiyo na pia tuma pamoja na maombi yako kupitia  namba hiyo, pia kama unataka kuwasiliana moja kwa moja na Mchungaji Elly Boto piga namba 0719640642 au 0752965812. MUNGU akubariki sana.
 pia karibu sana katika mkesha wa Krisimasi Tarehe 24/12/2013 pia karibu katika mkesha wa vijana wa kufunga mwaka Tarehe 29 December 2013 ampapo otakuwa ni mkesha utakaoakusanya vijana kutoka makanisa 6 yakiwemo KPC Kawe wenyeji, DPC kinondoni, PAG mbezi beach, PAG Goigi, PAG yombo na PAG mpopo. Karibu sana pia ndugu kutoka kila pande ya jiji. Zifuatazo ni baadhi ya picha katika Ibaada ya leo

Mchungaji Elly Boto na mzee wa kanisa Paulo wakati ibaada ikiendelea

Teddy Lukindo, mwimbaji binafsi akiimba katika ibaada ya leo

New Elshadai choir wakiimba

New Generation choir wakiimba

Praise & Worship team wakiongozwa na Scholar William Mungusa

Maombezi yakiendea ambapo kaka huyu alifunguliwa.

Moto wa MUNGU umeshuka, na mapepo yakiwaachia watu wa MUNGU

Dada huyu akisimama baada ya kufunguliwa kutoka nguvu za giza.

Mchungaji Elly Boto akimwombea mama huyu

YESU anaendelea kufungua watu wake, kupitia huduma ya mtumishi huyu, Hapa Ester akifunguliwa

Ni wakati wa watu kufunguliwa na kupokea uponyaji

Ulinzi wa MUNGU u juu yako dada

Mama Nashoni akiombewa na mtumishi wa MUNGU

Exaudi Shila akiombewa na mpakwa mafuta wa MUNGU, KPC

Mwenyekiti wa vijana KPC akiombewa na mchungaji Boto


Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12