Nifanye Nini Maombi Yangu Yajibiwe?

ili Maombi yako yajibiwe haraka

Utangulizi:
 
Maisha ya mkristo ni zaidi ya kuishi  na kule anakokufikiria yeye,
kila mmoja anaishi kwa fikira za Akili alizope na Mungu na kwa mipango ilyopo moyoni mwake   na kwa imani iliyondani ya Moyo wake akiaamini kwamba  anayetowa reziki zote na baraka ni Mungu, hili halikataliwi na Mtu,
japo watu wanahitaji kufanikiwa bila kanuni au utaratibu uliyowekwa na mwenyewe anayebariki, kutaka kibali mbele za Mungu kinyume cha utaratibu na kanuni alizoziweka Mungu ni kama kuvuna katika shamba ambalo wewe hukushughulika na jambo lolote zaidi ya kuvuna,
kwa lugha nyingine kutaka kituambachohujakifanyia kazi ni si vizuri kwakuwa hata Neema tumepewa kwa kuikubali na kuipokea,
waefeso 1:1
Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;
kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.
Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake.

Yaani, kuleta madaraka ya wakati mkamilifu atavijumlisha vitu vyote katika Kristo, vitu vya mbinguni na vitu vya duniani pia. Naam, katika yeye huyo;
 na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.
kuishi kwetu kunahitaji maelekezo ya kila siku yaani kumuomba Mungu atufundishe namna ya kuishi tuwapo hapa Duniani ili kwenda sawa sawa na mpango wa Mungu,

wengi wetu tumebadilisha Maelekezo tuliyopewa na Mungu, baada ya kuishi vile anavyotaka tunaishi vile tunavyotaka sisi na kuanza kumlazimisha Mungu aingie katika mawazo yetu,

Tamani kuingia katika mawazo ya Mungu Usimlazimishe Mungu Kuingia Katika Mawazo Yako,

Maandiko Matakatifu kutoka katika kitabu kilichoandikwa na Mathayo 6:33 

 Mungu hakututuma au kutuagiza kutafuta chakula na kitu cha kunywa bali maagizo ni kutafuta Ufalme wake mengine Tutazidishiwa  Kwa lugha nyepesi sisi tunavyokuwa waaminifu kuutafuta ufalme wake yeye ana hakikisha hatuishiwi kwa jambo lolote lile,
Katika haya yote nidhamu inahitajika sana kwa Mungu na kwa wanadamu wote,
Kumjuwa Mungu Si tatizo kwa watu siku za leo au Kuwa na imani si tatizo kwa watu siku za leo ila imani na kutokuamini ni vitu wiwili tofauti, unaweza kuwa na imani lakini imani uliyo nayo huiamini japo unayo,
kumjuwa Mungu ni habari nyingine  na kumwamini Mungu ni hatuwa ninyinge ,hili linawasumbuwa sana watu wengi Mungu atusaidie sana ,
Amesema Tuutafute ufalme wake yeye si muongo Tufanye hivyo, tena kwa uhakika maandiko Matakatifu yanakazia katika kitabu cha
Mathayo 7:7 
hii inamaanisha tangu kipindi kile cha agano la kale hata sasa Mungu alikuwa ni wautaratibi,
Yeremia29:13/mithali 14:2,ufunuo 13:1.timotheo 1:7 mithali 13:18
  tunafundishwa Kuutafuta Ufalme ili mengine yakae sawa yenyewa,
Kupata kibali kunazuiliwa na mambo mengi sana kwakuwa mawasliano siku zote yanaazia hatuwa ya kwanza kwenda hatuwa ya pili,
Fuatilia hatuwa chache zitakazo kusaidia wewe kupata kibali
  1. Tunatakiwa kujifundisha namna ya kujiadabisha sisi wenyewe kabla ya kuwaadabisha wengine,katika maisha yetu ya kila siku
  2. Mahusiano yako na Mungu yanatakiwa kuongezeka kila siku na si kupunguwa  kwa Maovu unayotenda kwa kusudia au kwakutokusudia
  3. Mahusiano yako na familia/jamii iliyokuzunguka yanamaana kubwa sana Mbele za watu na Mbele za Mungu unayemwamoni na kuyafuata maagizo yake
  4. Mahusiano ya wewe yanatokana na ukaribu wa wewe kushiriki ibada au mafundisho
  5. Ushahidi kwa kila mmoja juu ya maisha yako ya kila siku
  6. Mazingira au maeneo yako ya kutafutia riziki au unakoishi unaishije
 
Msaada namna ya kutumia somo hili unalolisoma sasa hivi
  1. Tenga muda wa maombi na kumtafakari Mungu kwa kikubwa au kidogo ulichopata
  2. ishi maisha ya toba kila wakati kwakuwa hujui saa wala siku ya Yesu kurudi
  3. Nawezaje kuwa mtakatifu? zaburi  119:11
  4. Katika familia usiogopo kuwachapa watoto kisa unataka kujionyesha ni mtakatifu hapana juu ya watoto wanatakiwa wakikosea wachapwe Mithali 23:13,mithali 29:17
  5. Yapo mengi ninaomba haya machache anza nayo kwaza Mathayo 5:6 sisi ni Nuru usikubali kupotesa mwangaza bwana aliyouweka juu yako,
  6. Ikiwa unahitaji masomo ya Nabii Samson Mungu amemwita katika Umri Mdogo sana Lakini Mungu amempaka Mafuta  kuwafunguwa watu katika vifungo Mbalimbali Mungu Anamtumia katika Ishara ya matendo makuu ya Mungu na Miujiza Mingi sana ikiwa unahitaji ushahuri au maombi piga simu yake Utahudumiwa na yeye mwenyewe ni bure kabisa huduma hii piga sasa Nabii samson 0756 809 209
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments