Papa Francis wa kanisa katoliki duniani wiki hii ameshuhudia kwa waumini wa kanisa hilo nje ya Roma akidai kwamba katika maisha yake ya zamani nchini Argentina alikotokea amewahi kuwa baunsa katika kumbi za starehe usiku pamoja na kufanya kazi ya ufagiaji na udobi.
Hata hivyo Papa akuzungumzia kwa undani zaidi juu ya matukio hayo lakini shirika la habari la Marekani CNN katika taarifa yake ambayo GK imenukuu imesema katika mazungumzo waliyofanya na mmoja wa wanafunzi waliowahi kuishi pamoja na papa Francis katika seminari ya Jesuit huko Argentina miaka ya 80 amesema Papa Francis alikuwa akiishi kwa mfano katika seminari hiyo akiwa kiongozi wa wanaseminari wengine wapatao 100
Papa Francis alikuwa akiwataka wenzake kusoma kwa bidii katika seminari hiyo lakini pia aliwataka kuwa na ukaribu na jamii ya watu masikini inayowazunguka kwa kujichanganya nao kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwao kabla ya kuwafundisha jambo lolote. Aidha mchungaji huyo amedai Papa alikuwa akiwafanyisha kazi ya kusafisha vyoo na mabafu katika seminari hiyo ikiwa ni njia moja wapo ya wao kujifunza maisha tofauti ya kuwatumikia watu.
Mchungaji huyo akaongeza kwamba kuna mtu amewahi kumkariri Papa Francis akisema kwamba ukaribu na watu masikini ni msingi mkubwa kwa mtumishi wa kanisa. Aidha alipoulizwa na mwandishi wa CNN kwamba wamejifunza nini kutoka kwa uongozi wa Papa Francis ambaye kwa wakati huo alikuwa akijulikana kwa jina lake halisi la Jorge Bergoglio, amesema ni mtu wa mfano kwakuwa aliwataka watu wote katika seminari hiyo kuishi kama familia moja na kusaidiana katika kila hali.
Lakini kama haitoshi licha ya kwamba alikuwa kiongozi wao alikuwa kiongozi wa mfano ambapo wakati wengine wakiamka saa 11:30 alfajiri tayari walikuwa wakimkuta Papa Francis alikwisha amka akiendelea na usafi pamoja na kufanya kazi ya udobi kwakukusanya mashuka na nguo nyingine na kuziweka kwenye mashine tayari kwa kuzifua. Pamoja na hayo yote Papa Francis amekuwa akilitaka kanisa kushiriki kikamilifu katika injili na kusaidia watu waliokatika matatizo mbalimbali kwakuwa hiyo ndiyo kazi ya kanisa.
Aidha katika maelezo zaidi ya mahojiano hayo ni maeleo zaidi ya sifa za kiongozi ni zipi hasa zikitaka kiongozi kuwa mfano kwa wengine si kwakutoa maelekezo tu namna ambavyo kazi zinatakiwa kufanyika bali pia anahitaji kushiriki katika kazi hiyo ili kuinua hari ya wafanyakazi wake na kuachana na tabia ya baadhi ya viongozi kuwafanyisha kazi binadamu wenzao kama vifaa vingine bali wanahitaji kuwatambua na kushirikiana nao katika kazi.
CHANZO: Gospel kitaa
Comments