SABABU YA KUHITAJI WOKOVU UTOKAO KWA MUNGU MUUMBA

Na Sam Balele

Ashukuriwe Mungu kwa Roho wake, kwakuwa anawafunulia wanadamu ile iliyo kweli na kuwapa nafasi ya kuchagua ili kupokea Wokovu kutoka kwake kwa Njia ya Bwana Yesu Kristo, sawa sawa na Kusudi lake.
Wahubiri wengi wamekuwa wepesi kushambulia matendo fulani fulani na kupiga sana kelele juu ya dhambi hii na dhambi ile, na inayopata mashambulizi mengi ni dhambi ya zinaa. Hata mimi kuna wakati nimeshambulia dhambi fulani fulani, ili kwamba wanadamu wenzangu waache kuzitenda hizo. Kutoshika moja ya Amri 10 ni dhambi, kutotii Neno la Mungu ni dhambi, kutotekeleza maagizo ya Bwana Yesu ni dhambi. Dhambi, Biblia inasema ni uasi, ni kutotii mamlaka halali; kutotii maagizo ya mamlaka halali na kutenda kinyume na maagizo hayo. Adamu na Hawa, wazazi wetu wa kwanza kwa habari ya Biblia walitenda dhambi kwa kutotii agizo walilopewa na Mungu. Walipoamua kumsikiliza nyoka[shetani] na hivyo kutenda kinyume na agizo la Mungu Muumba. Wazazi wetu hawa wakatenda UASI, wakatenda DHAMBI.

Sasa unajua kwa kanuni ya Mungu, wakati wawili hawa wanamuasi Mungu Muumba, wanadamu wote, wale waliokwisha kuwapo duniani, tuliopo sasa, yaani wewe na mimi, na wale watakaozaliwa kesho na siku zijazo; Mungu Muumba kwa hekima yake, alihesabu wanadamu wote hao kuwamo ndani ya kiuno cha Adamu, hivyo kuasi kwake baba yetu kukahesabiwa kuwa sawa na kuasi kwa wanadamu wote. Ndipo Biblia inasema katika Warumi 5:19; "Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja [Adamu] watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja[Yesu] watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki". Kuasi kwa Adamu kuliathiri wanadamu wote, wote wakahesabiwa kuwa wenye dhambi, HIVYO WOTE WANAZALIWA KATIKA HALI YA KUWA WENYE DHAMBI. Maana yake ni hii sasa; Si mpaka utende dhambi ndio uwe mwenye dhambi, ila unahesabiwa mwenye dhambi kwa kuwa Adamu alitenda dhambi na Mungu Muumba kwa hekima yake akahesabu wanadamu wote wametenda dhambi, ukijumuishwa na wewe usomaye post hii.

Hivyo hali ya kuwa mwenye dhambi ni ya kuzaliwa nayo, na kwa kuwa unazaliwa katika hali ya dhambi ndio sababu unatenda dhambi. Nikiazima lugha naweza kusema hivi; We are sinners not because we sin, We sin because we are sinners. Hakuna mwanadamu anayezaliwa safi, wanadamu wote wanazaliwa wakiwa ni sinners mbele za Mungu. Warumi 5:12 imeandikwa; Kwahiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi illingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi". Ukisoma pale mbele zaidi ule mstari wa 14 inasema ile mauti "nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu". Dhambi ilileta mauti; mauti ni utenganisho wa vitu viwili, nikiazima lugha tena; DEATH IS A SEPARATION OF TWO THINGS. Mwili wa mwanadamu unapotengana na roho ya mwanadamu tunasema fulani amekufa, amekutwa na mauti. Sasa unajua roho ya mwanadamu inapotengana na Roho wa Mungu, pia inasemwa mwanadamu amekutwa na mauti japo bado anatembea ulimwenguni akiishi maisha yake. Kuna mauti ya rohoni, na mauti ya mwilini. Dhambi aliyofanya Adamu na Mungu akaihesabu kwa wanadamu wote ilileta mauti zote mbili kwa wanadamu. Kwanza mwanadamu alitengwa na Roho wa Mungu,(Mwanzo 2:16-17) na pia akaambiwa "kwa maana u mavumbi wewe , nawe mavumbini utarudi"( Mwanzo 3:19). Hivyo mauti zote mbili zikachukua nafasi kwa wanadamu wote kuanzia siku hiyo Adamu alipomuasi Mungu Muumba wa wote. Wanadamu wakahesabiwa kuwa wenye dhambi, wakizaliwa katika hali ya dhambi, wakiwa chini ya nguvu ya dhambi na mauti, mauti zote mbili, ya rohoni na ya mwilini.

Ndipo hapa unapokuja u-maana wa kazi aliyokuja kuifanya Yesu Kristo ulimwenguni. Kazi ya kuokoa kilichopotea (Mathayo 18:11).Kazi ya kukomboa kutoka uharibifu wa mauti. Kazi ya kumpatanisha mwanadamu na Mungu wake. Kazi ya kufungua waliofungwa[wanadamu wote] katika kifungo cha dhambi na mauti. Kazi ya kuwanunua wanadamu waliouzwa kwa Shetani kwasababu ya kuasi kwa wazazi wetu wa kwanza, ambao walikubali kudanganywa na Shetani na kutenda dhambi na hivyo kuwaathiri wanadamu wote. Kazi aliyofanya Yesu Kristo msalabani, hata akasema IMEKWISHA (Yohana 19:30), iliisha na ALIIFANYA na KUIMALIZA sawa sawa na mapenzi ya Mungu aliyemtuma kuja ulimwenguni. Yesu Kristo alikuja kuvunja nguvu ya dhambi na mauti iliyoanza kumtawala mwanadamu tangia bustani ya Edeni. Na akazichukua funguo za mauti na kuzimu kutoka kwa Shetani. Anazo Yeye tu, Yeye ndiye Njia, Kweli na Uzima.

I want to emphasize on this, ili ikuingie vizuri kabisa na uelewe hapa; You are a sinner not because you sin,you are a sinner because you are born a sinner. Yani unapozaliwa tayari wewe ni a sinner. Unazaliwa ukiwa umefarakana na Mungu tayari. Unazaliwa ukiwa umetengwa na Roho wa Mungu tayari. Unazaliwa ukiwa uko chini ya nguvu ya dhambi na mauti tayari. Unazaliwa ukiwa ni a reject, a sinner. Kule kutenda kwako matendo maovu, machafu, kutenda dhambi ni matokeo ya hali {ascribed status} unayozaliwa nayo, ambayo ni urithi kutoka kwa wazazi wetu wa kwanza Adamu na Hawa. Naomba Roho Mtakatifu akusaidie kuelewa hili nalosema hapa maana ndipo penye uponyaji wako hapa. Ukipata ufahamu hapa, hutohangaika na 'matawi ya mti' bali utahangaika kwanza na 'shina la mti'. Yesu alikuja ku-deal na 'shina', yaani dhambi na mauti, na kazi aliimaliza vizuri kabisa hata hapakuwa na haja ya mtu mwingine kuongeza chochote na kupotosha wengi na kuleta vurugu ulimwenguni.

Sasa Warumi 5:17-18 imeandikwa hivi; "17 Kwa maana ikiwa kwa kwa kukosa mtu mmoja mauti [ya rohoni na ya mwilini] ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa [gift] cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo. 18 Basi tena kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu [mauti]. kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima. 19 Kwa sababu kama kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki".

Alichokuja kufanya Yesu ni kinyume ya kile alichofanya Adamu, ndomana Biblia inamtaja Yesu kama Adamu wa pili [the second Adam]. Kuasi kwa Adamu wa kwanza kuliwaingiza wanadamu wote katika utumwa wa nguvu ya dhambi na mauti. Adhabu ya kuasi kwa Adamu wa kwanza ilikuwa ni mauti, mauti ya rohoni na mauti ya mwilini. Uzima aliokusudia Mungu kwa wanadamu ulitoweka. Utakatifu aliokusudia Mungu kwa wanadamu ulitoweka. Ndomana katika Agano la Kale, damu za wanyama zilikuwa zinafunika tu dhambi, bali katika Agano Jipya, damu ya Yesu haifuniki bali inafuta kabisa makosa yote a sinner amefanya. Kinyume cha dhambi na mauti ni utakatifu na uzima. Adamu wa kwanza aliwaingiza wanadamu wote katika dhambi na mauti, Adamu wa pili amewaingiza wanadamu wote katika utakatifu na uzima. Kutii kwake kumeleta haki yaani msamaha wa makosa ya wanadamu, kufutiwa dhambi zao walizotenda sababu ya hali ya urithi kutoka kwa Adamu wa kwanza.
2 Petro 1:3 imeandikwa hivi; "Kwa kuwa uweza wake na Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo Uzima na Utauwa[Utakatifu], kwa kumjua Yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe"

Sasa umeshaona urithi wako wa hali ya dhambi kutoka kwa Adamu wa kwanza, hivyo haijalishi utafanya juhudi na bidii kiasi gani za namna ya kidini/kidhehebu ama hekima ya kibinadamu kuepuka kutenda dhambi, ujue kuwa wewe mbele ya Mungu ni sinner tu hata ufanye nini, kwakuwa umezaliwa hivyo na si kwamba Mungu anakuhesabu a sinner sababu umevunja moja ya zile Amri 10 maarufu sana katika dini ulimwenguni. Hata ukizishika zote bado wewe ni sinner tu. Kuna kitu yakupasa ufanye ili utoke katika status hiyo uliyozaliwa nayo, nitakupa mfano mmoja kutoka katika Biblia ili uelewe kwa wepesi zaidi....kuna mtu mmoja alimwambia Bwana Yesu kuwa yeye amezishika amri 10 vizuri tu, Yesu mwishowe akamwambia kauze vyote ulivyonavyo kisha njoo unifuate (Mathayo 19:16-22). Sasa unajua watu wengi wamekuwa wanfocus zaidi katika ishu ya mali na utajiri wa yule mtu katika habari hii, lakini kitu cha muhimu hapa zaidi ni condition ambayo Bwana Yesu alimpa yule mtu nayo ni hii, KISHA NJOO UNIFUATE. Kuuza mali nI kujikana, ni kuamua kugeuka, ni kuamua kuacha mawazo yako na njia yako na kumgeukia Mungu kijumla bila kumchanganya na Shetani, na ili ufike kwa Mungu ni lazima umfuate Yesu Kristo, hakuna short cut wala long cut. Na hii ni kwa sababu ni Yeye tu aliye KIPATANISHO kati ya Mungu na wanadamu (1 Yohana 1:2). Ni Yeye tu mwenye kuweza kumtoa mwanadamu kutoka dhambi na mauti na kumuingiza katika utakatifu na uzima (1 Yohana 3:13a). Ni kwa Njia yake Yeye tu. Hakuna Njia nyingine.

Habari njema ni kuwa Yesu Kristo alishapiga kazi msalabani na kumwaga damu yake, na akasema imekwisha, tena akaenda na kuzichukua funguo za mauti na kuzimu kutoka kwa Shetani. Hivyo kwa kazi yake nzuri akatangaza uhuru kwa wanadamu wote. Akatangaza ushindi juu ya dhambi na mauti. Akatangaza Utakatifu na Uzima badala ya dhambi na mauti. Akatangaza upatanisho kati ya roho ya mwanadamu na Roho wa Mungu. Akatangaza uzima badala ya uharibifu ambalo ni tumaini la wale wanaompokea. Akatangaza msamaha wa makosa na dhambi za wanadamu wote. Akatangaza Wokovu na Ukombozi kwa wanadamu wote.

Ila sasa kwa hekima ya Mungu, huwa hafanyi mambo kwa kulazimisha, amempa mwanadamu free will. Ndomana imeandikwa katika Yohana 1:12; "Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa si kwa damu wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu bali kwa Mungu". Tena imeandikwa katika Yohana 3:19; "Na hii ndo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni na watu wakapenda giza kuliko nuru, kwa maana matendo yao yalikuwa maovu".

Ni hivi you are a sinner because you were born a sinner and not because you sin. You sin because you are a sinner, full stop. But the good news is that, Jesus Christ came and worked on this problem, it is no longer there. However to receive this work in your life and walk in the work that Jesus Christ did on the cross, requires you to to accept and profess it [believe it & confess it] (Warumi 10: 9-10). God will never enforce nor impose it on you, He only makes it known to you kama hivi ninavyokujulisha then the rest of the pie is up to you; kuchagua nuru ama giza. Wanadamu wote wamezaliwa katika giza, katika dhambi na mauti, it is up to you kuamua kutoka katika giza na kuhamia katika nuru, Ukiamua kuhama ndani ya moyo wako, Mungu achunguzaye mioyo ataona kilichomo ndani ya moyo wako nae Mungu atakuhamisha papo hapo (Wakolosai 1:13). Ukiamua kubaki, unakuwa umeamua kubaki mwenyewe kwakuwa matendo yako ni maovu, hivyo waona unafuu hapo ulipo katika dini ama dhehebu lako.

Bwana Yesu alisema nimekuja kutafuta kilichopotea. Wanadamu wote tulipotea tukiwa ndani ya Adamu. Wote tulitenda dhambi na kuingizwa katika mauti ya rohoni na mwilini. Wote tulitengwa na Mungu. Wote tuliuzwa kwa Shetani. Wote tulifanywa wenye dhambi.

Namshukuru Mungu Muumba kwa upendo wake wa kuamua kuandaa utaratibu wa kuwarejesha wanadamu katika himaya yake sawa sawa na Kusudi lake. Kwa Yesu Kristo ametukirimia wanadamu uzima na utakatifu. Lakini nataka ujue siri hii moja hapa kuwa Mungu huwa anafanya kazi na wanadamu, hivyo mwanadamu imempasa kufanya ile iliyo sehemu yake. Bwana Yesu alimwambia yule mtu tajiri kile kimpasacho kufanya na akashindwa na kwakuwa alipenda giza alienda hakurudi tena. Kumfuata Yesu Kristo ni kuikubali nuru kwakuwa Yeye ni Nuru, na Nuru haichangamani na matendo ya giza. Yesu Kristo si dini wala dhehebu. Yesu Kristo ni Yesu Kristo. Dini na madhehebu yana urafiki na matendo ya giza.

Warumi 1:28-32 imeandikwa hivi;
Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya, wamejawa na husuda na uuaji na fitina na hadaa, watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema, ambao wakijua sana hukumu ya Mungu, ya kwamba wayatendayo hayo wamestahili mauti [rohoni na mwilini], wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao"

Kama umeweza kuisoma post hii yote, sasa namuomba Roho Mtakatifu azidi kutia ufahamu moyoni mwako, akushuhudie ili uamue kumfuata Yesu Kristo, awe Mwokozi wa maisha yako na Bwana wako. Akiwa Bwana wako, maana yake utamsikiliza Yeye, na kumsikiliza Yeye kunaanza na kutenda sawa sawa na maagizo yaliyo katika Neno la Mungu[Biblia], ili kubadilisha tabia na mwenendo wako, ufananishwe na mfano wake Yeye Yesu Kristo.

MUNGU AKUBARIKI.

By Sam Balele

 
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12