Salaamu za Krismasi kutoka Maisha ya ushindi (1)

SCHOLAR  KATIKA HUDUMA KANISANI
SCHOLAR WILLIAM MUNGUSA
BWANA YESU asifiwe. namshukuru MUNGU kwa uzima aliotupa hadi hii leo Dec 25 tunasherekea ukumbusho wa kuja kwa ukombozi duniani maana hakuna uzima popote ila ni kwa YESU KRISTO {Yohana 14:6}. Ndio maana dunia nzima ni shangwe na furaha kwa tukio ambalo limetokea miaka 2013 iliyopita ambapo siku YESU anazaliwa malaika ambao ni jeshi la mbinguni walishangilia na kumsifu sana MUNGU{Luka 2:8-14} na siku hiyo hiyo YESU mwanaume wa ajabu anazaliwa watu wenye heshima na watawala walimsujudia {Mathayo 2:11} hao walijua kuwa aliyezaliwa ni MFALME wa wafalme na BWANA wa mabwana. Pia YESU alizaliwa kwenye hori la ng'ombe ashilio la kwamba wanyama wapumzike maana hakuna tena sadaka ya kuteketezwa kama ilivyokuwa zamani  maana YESU ni dhabihu idumuyo milele ili watu wasamehe dhambi zao na kuurithi uzima wa milele bure kupitia yeye {Waebrania 9:12-15}.na tunasherekea christmas kwa kumwabudu MUNGU na kuonyesha upendo kwa wengine na kuhakisha kwamba  YESU anatenda jambo jipya mioyoni mwetu ili tuzidi kuishi katika neema yake maana kwa ajili yake na kwa neema yake alituhamisha kutoka kwa shetani na sasa tuko huru mbali na kuonewa na wachawi na hata nguvu zozote za giza. 

Nawasalimu na kuwatakia heri za Krismasi na heri za mwaka mpya ndugu zangu wote wakiwemo baba mzazi William akiwa Mwanza, Dada yangu Happy William akiwa Morogoro, Kaka zangu Peter William na Steven William, wana kwaya mwenzangu kanisani KPC, viongozi wa kanisa na kila aliye rafiki yangu. MUNGU awabariki sana.
ujumbe wangu ni kwamba tusherekee kwa amani na kwa kumtii MUNGU, AMEN.




Scholar William Mungusa

Scholar Mungusa, mwenye koti jeusi akiwa na wana Praise & Worship team wenzake KPC , Kawe, Dar es salaam

Hapa nilipo mimi ni kwa neema tu ya MUNGU


 Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12