SIKU KUU YA KRISMASI.

Mwl. Sospeter Simon Ndabagoye/ New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.


Utangulizi.

Dhana ya Jina la Krismasi.
Neno krismasi, linatokana na maneno mawili, Kris(Kristo) linalo maanisha masihi wa Bwana, yaani mpakwa mafuta wa Bwana. Masi(mass) likimaniisha kusanyiko; hivyo dhana Krismasi ni kusanyiko la wakristo, au kusanyiko kwaajili ya kristo. Epukana na dhana nyingine zisizofaa kama vile XMASS- ambayo huweza kupotosha maana halisi. Kumbaka kuwa hakuna krismasi bila Kristo, kwa hiyo neno XMASS ni neno linaloweza kuwa na dhana kamili iliyotofauti na Krismasi.

Asili ya krismasi.
Wazo la Krismasi liliasisiwa na Mungu mwenyewe alipokuwa akipanga mbinu ya ukombozi baada ya dhambi kumtenga mwanadamu na Mungu wake. Hivyo Mungu akauweka mpango makili wa ukombozi. (Rumi 5:12, Efeso 2:1-3).

Swali la kujiuliza ni je, kama Mungu alijua kuwa kupitia Mariamu ulimwengu utakombolewa, kwanini hakumwona kuwa anatosha yeye mwenyewe peke yake kuukomboa ulimwengu?

Huku tukiendelea kujiuliza vichwani mwetu, tutabaini kuwa, licha ya Mungu kumuumba mwanadamu na kumpa mamlaka ya kurithi na kutawala na kutisha, lakini ibilisi aliweza kumwangusha; hivyo ikambidi aweke mkakati maalum kutoka mbinguni kwa kuwa hata asili ya shetani ni mbinguni japo hawezi kurudi kamwe, hivyo Mungu akamleta mwanae wa pekee kutoka huko(mbinguni) ili aje na kuukomboa ulimwengu dhidi ya utumwa wa dhambi.
Hivyo, Yesu alikuja na kuishi kwetu kama mwanadamu japo alikuwa Mungu kamili.(Luka 1:26-35). Alikuwepo tangu asili hata kabla ya ulimwengu kuwako.(Yohana 1:1,3&14).

Je kusudi la yesu kuja duniani ni nini?

Kuna sababu kadha wa kadha za ujio wa Yesu, zifuatazo ni baadhi tu ya sababu kuu za ujio wake.

(a) Kutukomboa wanadamu.
Ili kumtoa mwanadam chini ya utumwa wa dhambi na utawala wa shetani. Mwanadam alianza kuishi chini ya utawala huu, tangu alipokubali kuitii sauti ya ibilisi na umtenda Mungu dhambi kwa kula tunda alilokatazwa,hivyo, mwanadam alipoisikia sauti ya ibilisi, tayari alivunja uhusiano wake na Mungu.
Kwa kigezo hicho, ujio wa Yesu ni kwaajili ya kututoa mateka (Kolosai 1:13, Luka 19:10) chini ya udhibiti wa joka la zamani, mwenye gadhabu audanganye ulimwengu.

(b) Kurejesha Ushirika wetu na Mungu.
Baada ya dhambi kuingia ulimwenguni, mwanadamu aliungana na ibilisi na kuwa mali yake (1Yohana 1:3), mpaka Mungu alipomtuma Yesu aje kumrejesha upya. Hivyo, kazi kuu ya Yesu ilikuwa kuurudisha uhusiano ulioporwa na shetani (the lost opportunity).
Kwa hiyo, ujio wa Yesu umemweka mwanadamu katika familia ya Mungu. (Yohana 1:12, 1Yahana 3:1&2).

(c) Kutununua.
Yesu alifanyika fidia kwa kuutoa uhai wake msalabani (Mathayo 20:28), kwa kigezo hicho, damu na maji ya Yesu, vilifanyika toba ya kweli na msamaha kwa ulimwengu na kuwa patanisho la milele na Mungu.
Kupitia kifo cha msalaba, mwanadamu aliyekuwa chini ya utumwa na umiliki wa ibilisi, simba aungurumae mchana/ chatu mwenye njaa na gadhabu nyingi alipata tumaini jipya la uzima wa milele kwa kuwekwa huru na kutengwa na dhambi(1Yohana 5:11&12, Yohana 3:16&17, 10:10).

(d) Kututenga mbali za kazi za shetani.
Yesu alikuja kuvunja na kuharibu kazi za mfalme wa giza alie ibilisi(1Yohana 3:8). Ifahamikie kuwa, mwanadamu alipoacha kumtumikia Mungu, basi alianza kumtumikia shetani, hivyo Yesu alikuja kuvunja mkataba huo na ndiyo maana aligharimia mkataba huo kwa damu yake.

(e) Ili kuwani ishara ya upendo wa Mungu kwa mwanadamu (1Yohana 4:9&10,Rumi 5:8)
Yesu alikuja kwaajili ya watu wote, na aliwakomboa kwa pamoja, bila kujali sura, asili, mali n.k. hivyo, ili kuonesha upendo wake wa dhati, ilimbidi ashuke chini na anyeneyekee hadi kifo cha msalaba.
HITIMISHO.
Hatahivyo, Mungu alipanga kuonesha uwezo wake na nguvu zake kuwa ziko juu zaidi. Ndiyo maana, ujio wa Yesu ulimabatana na kuzibatilisha kazi za ibilisi zikimabatana na miujiza (Yoha 6:1-21, Marko 4:37-41),Uponyaji (Mathayo 4:24,Yohana 9:1-7),Utoaji wa pepo na kufungua vifungo vyote (Marko 1:34, 5:1-7,) hata kufufua waliokufa tayari (Yohana 11:43&44). Hili lilienga kutoa mamlaka kuu zaidi kwa watao mwamini ili watende haya na zaidi ya haya. Haleluyaaaaaaaa.
New Elshaddai Minisries NEM-Tanzania inawatakia Kila la Kheri, muwe na siki kuu njema, iliyojaa amani, upendo na furaha.
Mungu awabariki sana.
Na. Mwl. Sospeter Simon S. Ndabagoye.
 

 
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12