Siku ya pili ya mkutano wa Mtume Peter Nyaga, Tabata kimanga; Watu 120 waokoka

Mtume Peter Nyaga akihubiri siku ya pili ya mkutano.
Urejesho unaendelea katika mkutano wa injili unaoendelea katika viwanja vya serikali za mitaa, Savana , Tabata Kimanga ambapo MUNGU kwa jinsi ya ajabu sana anaendelea kumtumia mtumishi wake mtume Peter Nyaga kutoka RGC Miracle centre, ambapo katika siku ya pili ya mkutano huo yaani jumapili tarehe 29 watu 120 wamempa BWANA YESU maisha yako na watu wengine wengi kurejeshewa baraka zao . Ndugu karibu sana katika mkutano huu wa siku 9 na kama ni mgonjwa uliyeshindikana njoo maana MUNGU anataka kukuponya kabla ya mwaka 2014 ili uanze mwaka ukiwa mzima.
hizi ni baadhi ya picha za siku ya pili ya mkutano.
ni saa ya uponyaji na kufunguliwa, ni saa ya vilema kutembea na viziwi kusikia tena katika jina la YESU KRISTO



Maelfu ya watu wanahudhuria karibu ndugu na wewe upokee muujiza wako
Zacharia Kenyatta  akiimba katika mkutano huo

Tanzania kwa YESU

Neema Mwaipopo akiimba katika mkutano huo.

Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12