Tabata Kimanga, moto unaendelea kuwaka ni katika mkutano wa mtume Peter Nyaga

Siku ya 3 katika mkutano mkubwa wa injili, BWANA YESU anaendelea kumtumia mtumishi wake Mtume Peter Nyaga huko Tabata Kimanga, maeneo ya Savana kwenye viwanja vya serikali ya mitaa. Jumatatu hii ilikuwa ni moto wa MUNGU ukiangamiza kazi zote za shetani ndani ya watu. Hakika BWANA YESU alidhihirishwa ili azivunje kazi zote za shetani(1 Yohana 3:8), na hakika kazi za shetani zinavunjika isivyo kawaida. Ndugu karibu pia na wewe kesho na hadi tarehe 5/ January/ 2014.

Neema Jekonia Chavara akiimba kwenye mkutano huo
Ni saa ya urejesho kwa watu wa MUNGU



Ni saa ya kufunguliwa na kuwekwa huru, hapa Mtume Nyaga akimwombea dada huyu aliyekuwa anasumbuliwa na nguvu za giza na baada ya maombezi akawa huru
What God can do no man can do
ni saa ya kufunguliwa
Mamlaka ya BWANA YESU inatenda kazi sana katika mkutano huu wa siku 9 yaani hadi tarehe 5 january 2014
Zacharia Kenyatta na brother Joshua tayari kumtukuza MUNGU
Upendo Nkone kama kawaida yupo kumtukuza MUNGU



Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio
jina lake; -Yohana 1:12