TUUTAFUTE KWANZA UFALME WA MUNGU.


Siku hizi watu wamekuwa busy wakiangaika kutafuta utajiri na uponjaji na miujiza,badala ya kuutafuta ufalme wa Mungu ili atuzidishie mahitaji yetu Mathayo 6:33-34.Watu wametekwa na mafundisho
ya utajirisho zaidi kuliko kumjua Mungu Ayubu 22:21"Mjue sana MUNGU,ili uwe na amani.Ndivyo mema yatakavyokujia" pia 2 Petro 3:18 "Lakini kueni katika neema,na katika kumjua BWANA wetu na Mwokozi YESU KRISTO.Utukufu una yeye sasa nahata milele"Kwa maana hiyo tumjue kwanza yeye ndipo hayo tunayoyaangaikia tutapewa tena kwa mazidisho.Ili tuweze kuwa karibu na Mungu lazima kwanza tuokoke Warumi 10:9-11


Yafuatayo ni lazima sana ili tupondeke mioyo yetu na kuvunjika roho zetu Zaburi 34:18
 
1.Tuishi maisha matakatifu  

 1Petro 1:16 "Kwa imeandikwa.Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu"

2.Tuishi maisha ya utakaso
Yohana 17:17 "Uwatakase kwa ile kweli;neno lako ndiyo kweli"

 
Vinginevyo ni mbinu za adui shetani kutufanya tumjue Mungu kwa maana neno lake.Amka wewe usinziaye sasa na ubadili mwenendo kazana kumjua Mungu acha kufukuzana na pesa fukuzana ili ulijue neno la Mungu.Mungu wetu na akubariki.

Comments