BWANA YESU asifiwe wapendwa wa BWANA
Habari za sikukuu ya kukumbuka kuja kwa wokovu wa mwanadamu.
leo tunajifunza ujumbe kuhusu tukio la ajabu sana la kukumbuka kuzaliwa kwa BWANA YESU KRISTO au kuja kwa wokovu duniani.
Biblia inaanza kwa kutoa unabii wa kuzaliwa kwa BWANA YESU miaka 700 kabla ya kuzaliwa kwa BWANA YESU.
''Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, MUNGU mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo. -Isaya 9:6-7.''
MUNGU aliupenda ulimwengu yaani aliwapenda wanadamu na akaamua kumleta mwanaye wa pekee ili wanadamu wote wapate uzima wa milele kupitia yeye,(Yohana 3:16). BWANA YESU alikuja duniani kwa lengo moja tu la kuwaokoa wanadamu, kutoka mikononi mwa shetani, hivyo unapompokea unapokea uzima tena unapata kibali cha kumshinda shetani na mawakala wake wote, dhambi ilipoingia ilileta mabaya mengi sana , ilileta magonjwa, vifo, mikosi, ajali, balaa na majanga ya kila aina ndio maana kwa kwa kusudi hilo BWANA YESU alidhihilishwa au alikuja ili kuzivunja na kuziharibu kazi zote za shetani(1 Yohana 3:8b).
Jambo jingine la kukumbuka ni kwamba BWANA YESU hata kabla ya kuja duniani, yaani kuzaliwa na Bikra Mariamu , BWANA YESU alikuwepo tangu milele na wala hana mwanzo wala mwisho(Mika 5:2). nampenda sana BWANA YESU maana anaokoa mwili na roho pia na ukiwa kwake hakika ni furaha sana na sikukuu hii ya Krismasi ndio sikukuu inayoongoza kwa kusherekewa kuliko siku nyingine yeyote kwa maana ndio mwanzo wa WOKOVU na hii ya kusherekea kuzaliwa kwa BWANA YESU haikuanzishwa tu na wanadamu bali MUNGU ndie aliyeanzisha pale ambapo baada tu ya kuzaliwa kwake BWANA YESU utukufu wa MUNGU ulionekana, jeshi kubwa sana la malaika walikua wanaendelea kusherekea na nuru ya ajabu iliwazukia machungaji haya yanapatikana katika Luka 2:8-15(Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku. Malaika wa BWANA akawatokea ghafula, utukufu wa BWANA ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu. Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, MWOKOZI, ndiye KRISTO BWANA. Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng'ombe. Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu MUNGU, na kusema, Atukuzwe MUNGU juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia. Ikawa, malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya, na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika, alilotujulisha BWANA''.
Maana ya CHRISTMASS ni maneno mawili yaani 1. CHRIST(Mesiah au mpakwa mafuta au aliyetengwa kwa kazi maalum) na neno la pili ni 2.MASS yaani kusanyiko (group of .....) Kwa hiyo maana ya CHRISTMASS ni kusanyiko la KRISTO.
Hakika kuzaliwa kwa BWANA ni jambo muhimu sana kwa wanadamu, na tusherekee kwa kumtukuza MUNGU na kukumbuka tukio hili muhimu pia ni muhimu wewe ambae bado hujampokea BWANA ni muhimu sana kufanya hivyo leo maana hakuna uzima wa milele kwingine(Yohana 14:6, Matendo 4:12) na ukimpokea BWANA YESU unakuwa kiumbe kipya, ya kale yanapita na unakuwa mtu mpya ambaye jina lako limeandikwa kwenye kitabu cha uzima.
MUNGU akubariki sana na nakutakia sikukuu njema ya KUSANYIKO LA KRISTO KWA UTUKUFU WA MUNGU.
MERRY CHRISTMAS & HAPPY NEW YEAR 2014.
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula
Maisha ya ushindi Ministry.
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12