UJUMBE WANGU WA MWAKA MPYA,IKIWA MASAA MACHACHE YAMEBAKIA KUUMALIZA MWAKA 2013 NA KUUKARIBISHA 2014.


Bwana Yesu asifiwe...
Na Mtumishi Gasper Madumla
Bwana Yesu asifiwe...
Napenda nikuambie hivi;
*Upo mpaka saa hii kwa sababu ya neema na rehema za Mungu Baba,na wala sio kwa ujanja wako hata mimi nipo hivi sio kwa ujanja wangu,bali ni kwa neema tu.

Ukilitambua hilo,basi ni dhahili utapomoka kifudi-fudi na kumshukuru BWANA MUNGU kwa namna ya kipekee akupavyo pumzi ya bure,
Maana wengine walitamani kufika hata muda huu lakini hawakufika,
Yamkini wengine wapo mahospitalini,
wengine wameshavunjika miguu na viungo vingine kwa ajali,N.K
Lakini wewe upo salama kabisaa,
Tena hata hukusikia taharifa mbaya kutoka katika familia,au hata ukoo wako.

Ukiona hivyo,basi ujue LIPO KUSUDI LA MSINGI KWAKO ambalo unatakiwa ulifanye kwa Bwana.
Mwaka 2013 ulikuwa ni mwaka wako wa kulitangaza Jina la Bwana kwa watu wote,lakini ikiwa ulifanya kwa sehemu basi Mungu akusaidie wewe pamoja nami tukalitangaze jina la Bwana kwa watu wote.

Sasa hivi;
Wakati wengine wapo katika ma-bar wakinywa na kulewa,
wakati wengine wakimchezea shetani nyimbo zake katika makumbi ya starehe,
Wakati wengine wanafanya dhambi,
BALI WEWE NENDA NYUMBANI MWA BWANA MUNGU,
KALIITIE JINA LAKE KATIKA KUSHUKURU,KUSIFU,NA KUABUDU KWA KUUNGANA NA WAZEE 24 NA WENYE UHAI WA NNE
WASEMAO,
MTAKATIFU,MTAKATIFU,MTAKATIFU,
UNASTAHILI KUABUDIWA....

*NAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA,WENYE MAFANIKIO TELE YA KIROHO NA KIMWILI PIA.
UBARIKIWE.

 
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12