UKWELI KUHUSU MAISHA BAADA YA KIFO



LUka 16:19-31 Habari ya Tajiri Na Maskini Lazaro

19 Akasema, “Palikuwa na tajiri mmoja aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, nguo za gharama kubwa, kila siku. 20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, mwenye vidonda mwili mzima, ALIKUWA AKILETWA MLANGONI KWA HUYO TAJIRI KILA SIKU. 21 Lazaro alikuwa akitamani kula makombo yaliyodondoka mezani kwa tajiri. HATA MBWA WALIKUWA WAKIRAMBA VIDONDA VYAKE.

22 “Hatimaye, yule maskini alikufa. MALAIKA AKAMCHUKUA AKAKE PAMOJA NA IBRAHIM MBINGUNI. Yule tajiri naye pia akafa, akazikwa. 23 AALIPOKUWA KUZIMUNI ambapo ALIKUWA AKITESEKA, alita zama juu, AKAMWONA IBRAHIM KWA MBALI NA LAZARO KARIBU YAKE 24 Akaita, ‘Baba Ibrahimu, nionee huruma umtume Lazaro achovye japo ncha ya kidole chake katika maji aupoze ulimi wangu maana ninateseka kwenye moto huu.’ 25 Lakini Ibrahimu akamjibu, ‘Mwanangu, kumbuka kwamba ulipokuwa hai ulipata kila kitu kizuri uli chotaka, ambapo Lazaro alipokea mabaya. Lakini sasa anafarijika hapa na wewe unateseka. 26 Isitoshe, KATI YETU NA NINYI HUKO KUMEWEKWA BONDE KUBWA LISILOPITIKA ili wale wanaotaka kutoka huku kuja huko au kutoka huko kuja huku wasiweze.’ 27 Akasema, ‘Basi, baba, tafadhali umtume Lazaro aende nyumbani kwa baba yangu, 28 awaonye ndugu zangu, wasije wao pia wakaletwa mahali hapa pa mateso watakapokufa.’ 29 Ibrahimu akamjibu, ‘Ndugu zako wanazo sheria za Musa na maandiko ya Manabii. Itawapasa watii hayo.’ Lakini yule tajiri akazidi kumsihi, 30 ‘Hapana baba Ibrahimu, ndugu zangu hawatashawishiwa na hayo. Lakini mtu kutoka kuzimu akitumwa kwao watatubu na kuziacha dhambi zao.’

31 “Ibrahimu akamwambia, ‘Wasiposikiliza na kutii sheria za Musa na Maandiko ya manabii, hawatashawishika kutubu hata kama mtu akifufuka kutoka kuzimu.”’

MAMBO MUHIMU YA KUJIFUNZA KWENYE HABARI HII
1. Mahali alipokuwa lazaro ni tofauti kabisa na mahali alipokuwa yule Tajiri, LAZARO ALIPELEKWA KUKAA PAMOJA NA IBRAHIM (PARADISO) na TAJIRO ALIPELEKWA KUZIMUNI MAHALA PA MATESO
2. Kuzimu na Paradiso ni sehemu mbili tofauti ambazo zimetenganishwa kabisa, wala hakuna uwezekano wa mtu aliye upande mmoja kwenda upande mwingine
3. KUZIMU ni mahala pa MATESO na PARADISO (kifuani pa ibrahim) NI MAHALI PA MAPUMZIKO NA KUFARIJIWA
4. Kilichompeleka tajiri kuzimu si utajiri wake, bali ni uwakili mbaya wa mali aliyopewa na Mungu ambapo hakuweza kuitumia kudhihirisha wema wa Mungu hasa kwa kuwasaidia wau maskini akiwemo lazaro aliyekuwa akiwekwa mlangoni kwake kila siku. kilichomfikisha kuzimu ni Moyo wa choyo na kiburi.
5.Kilichomfikisha lazaro PARADISO si umaskini, ila ni moyo thabiti wa kumwishia Mungu licha ya kubanwa na hali ya umaskini.
6. Watu walioko KUZIMU wanatamani waliopo duniani wasiende huko, kwa kuwa ni mahali pa mateso
7. Njia pekee ya kufika Paradiso na kupata pimziko uweponi mwa Mungu ni Kutembea sawasawa na neno la Mungu hapa ulimwenguni, kumwishia Mungu na kuwa wakili mwema wa vipawa uivyopewa na Mungu
8.UKISHAKUFA HAKUNA TENA NAFASI YA KUTUBU. tunaona mara baada ya lazaro kufa alipelekwa kifuani pa ibrahim, hakukuwa tena na kikao cha hukumu. kadhalika tajiri naye alipokuwa alipelekwa na malaika moja kwa moja KUZIMU. hakukuwa na majadiliano tena.

HITIMISHO
Achana na habari za Dini, za watu wanaokwambia haiwezekani kuokoka ukiwa hapa ulimwenguni, na maneno ya kwamba haiwezekani kuwa mtakatifu hapa ulimwenguni. Mungu mwenyewe amesema katika Zaburi 16:3 "watakatifu walioko duniani hao ndio walio bora, hao ndio ninaopendezwa nao" bWANA YESU PIA AMESEMA AAMINIYE NA KUBATIZWA "ATAOKOKA" (Marko 16:16)
Elewa kwamba WOKOVU NI LAZIMA kwa yeyote anayetaka kuingia mbinguni, NI HAKIKA KWAMBA WOTE TUTAKUFA, Yesu kristo alishasema katika injili ya Yohana 14:6 Mimi ndimi NJIA na KWELI na UZIMA; MTU HAJI KWA BABA ILA KWA NJIA YA MIMI. Sina shida na Dini yako, wala Mtume wako, wala chochote unachoamini, ila ninachojua ni kwamba kama una tarajio la kuingia mbinguni then jua hilo haliwezekani bila Yesu ndani yako. Kama unataka kuepuka mateso baada ya maisha haya, then Hilo haliwezekani bila yesu ndani yako, bila kuishi maisha matakatifu hapa ulimwenguni. Napenda uelewe kwamba hata sasa hukumu ya Mungu inaendelea, wala si jambo la siku ya mwisho, kwa kuwa HUKUMU YA MUNGU NI PROCESS INAYOPELEKEA KWENYE UHARIBIFU WA ULIMWENGU HUU NA KUDHIHIRISHWA KWA ULIMWENGU MPYA, MBINGU MPYA NA NCHI MPYA AMBAYO BWANA YESU ANAIANDAA TANGU ALIPOPAA MBINGUNI. (hii inaonekana kwenye ufunuo 21 na 22)

OMBI LANGU KWA AJILI YAKO NA YANGU
Mungu akupe moyo wa kuelewa NA NEEMA YA KUPATA WOKOVU, Mungu aondoe moyo wa jiwe ndani yako na kukupa moyo wa nyama ili upokee wokovu na kuepuka hukumu na adhabu ya milele. Kwa wewe uliyeokoka, Mungu akushike kwa mkono wake wenye nguvu ili usije acha wokovu mpaka siku ya mwisho.

SALA YA TOBA.
ikiwa umefanya nia yakuokoka leo hii, TAFADHALI OMBA SALA IFUATAYO NA KISHA NITUMIE SMS UKIELEZA UMEOKOKA LEO ili tuombe pamoja na upate maelekezo ya kukusaidia.
BWANA YESU, NINAKUJA MBELE ZAKO KWA DAMU YAKO YA THAMANI, MIMI NI MWENYE DHAMBI, NIMEKUKOSEA SANA, UOVU WANGU UMEFIKA MBELE ZAKO, NAMI NIMETAMBUA LEO KUWA MAISHA YANGU PASIPO WEWE NI BURE, NINAKUSIHI LEO HII UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE, UNIOSHE KWA DAMU YAKO YA THAMANI, FUTA JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, NA ANDIKA JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA. NAKUSIHI KATIKA JINA LAKO TAKATIFU UNIHAMISHE KUTOKA UFALME WA GIZA NA KUNIINGIZA KATIKA UFALME WA PENDO LAKO SASA, NAKUSIHI UNIJAZE KWA ROHO WAKO MTAKATIFU ANIONGOZE KATIKA KUYATIMIZA MAPENZI YAKO NA KUKUISHIA WEWE SIKU ZOTE. NINAOMBA HAYA YOTE KWA JINA LA YESU KRISTO
AMEN
Mungu akubariki

Comments