Yohana 14:23,24
Makao ni sehemu au mahali palipotengenezwa ili kitu au kiumbe kiishi.,Neno la Mungu linasema kuwa sisi
ni makao yake Yesu kristo.Yohana15:5
nyakati hizi ambazo kibiblia zinaonekana kuwa ni za mwisho wanadamu  wameamua kumfukuza Yesu ndani yao na kuruhusu
Yule  roho asi ambaye ni shetani. Yohana15;7 anasisitizia umuhimu wa sisi
kuwa makao  na anaahidi kutufanyia yale
yote tunayomwomba tukiamini kwa jina lake atatupa.Moja ya sababu  zinazoleta shida ndani ya mioyo ya wanadamu
ni kutokuwa na Mungu ndani yetu, na hili linawapata wakristo wanaojichanganya,ambao
kanisani kuingia kwao ni desturi dini wanaziheshimu wakiingia kanisani wanasifu,   sadaka na michango mbalimbali wantoa lakini
bado hawaamini uweza wa kriso ndani yao,na kristo mwenyewe ndani yao hayumo. 
       Kupitia neno la
Kristo anasema neno lake likikaa ndani yetu na yeye atakaa ndani yetu,na
kupitia neno la Mungu unamruhusu Yesu mwenyewe aje kukaa na wewe.jitahidi kila
neno linapokuja kwako uliruhusu likae ili kristo akae na wewe.Yohana 6:63’’Roho ndiyo itiayo uzima mwili
haufai kitu’’ Ufalme wa Mungu umeenea kila mahali na  wakristo wameukataa na kuutupilia mbali
,ndiyo maana utashuhudia maajabu mengi ya kushangaza wanayafanya wakristo na
siyo wapagani.Yohana 6:64.Kuamini ni
kusadiki na kusadiki ni kuwa ni mmja wa waliosikia,wakristo wengi licha 
ya
kushuhudia na kuona mambo makuu wanayotendewa na Mungu  bado 
kuamini kwao kuko mbali  kwamaana
hiyo wamempa nafasi shetani  ya kukaa
kwao.Na kama hulisikii neno la Mungu 
juwa wazi kuwa sauti utakazozisikia ni zashetani  kwa kuwa  zipo njia 
zilizompa uhalali wa  yeye kukaa kwako na  Mtu anaye tumkishwa na 
shetani anaweza kuwa
mchawi hata bila yeye kujua.
,Kutoka 22:18 ,19.
Maana mchawi kila akikaa anakuwa na hamu ya kuwaua wenzake  na huyu siku
 zote anamuhusu shetani  na ameshampa kibali cha kukaa ndani
yake.Wakristo wengi licha na kumshuhudia Kristo katika maisha yao bado
wanaendelea  kutambikia na kutoa kafara
mbalimbali kwa shetani na maagano haya yanawapatanisha na shetani  ndiyo
 yanayomfanya  ibilisi apate nafasi ya kukaa ndani yetu na
kutumiliki .Kumb18:22.
  Wapo manabii na watumishi ambao shetani  ndani yao ameweka pepo saba za utambuzi na
wamekuwa wakiwapotosha walio wengi wakidhani kuwa ni Mungu aliyejiinua,na ili
kuziepuka  roho hizi ni kuwa mtu wa
kusali na kuomba ili Mungu mwenyewe ajidhihirishe kwako.Kumb 5:7,jambo linalotupoteza wakristo wengi ni  juu ya kusikiliza mafundisho na mafunuo  ya Miungu 
au ya watu ambao  wanakaa na
shetani na roho hizo za uasi zinakaa ndani yao.Katika maandiko Mungu anazungumza
juu ya kujua mti wa mema na mbaya  ambao
ni uhalali wa  kufanya uchaguzi ,ikifika
mahali  ndani yako ukaanza kusikia hali
ya kuwachukia watumishi bila sababu yoyote 
jua ndani yako  shetani ameshapata
nafasi,na kazi kubwa ni kuondoa kuamini kile Kristo alichofanya ndani yetu,na
ukiona hivyo basi omba ibada ya upatanisho na Mungu ili Kristo aweze kutukuzwa
ndani yako.        
Wakolosai 1:21
Neno linasema kuwa ni Yesu
awezaye  kutupatanisha  na Mungu baba kwa njia ya neno lake,Wapo
wakristo wengi wanafanya dhambi kwa  siri
wakiwaficha wachungaji wao,wakristo wenzao na kusahau kuwa hao ni wanadamu na
hawana mbingu ya kuwapeleka,na neno linatuweka wazi kuwa  Mungu huichunguza mioyo na viuno vyake na
kwake hakuna siri kwa kuwa anajua  kesho
na keshokutwa ya mwanadamu.Dhambi hizi 
anazofanya mwanadamu ndizo zinasababisha 
asipokee baraka,(Yeremia 48:7-8
)kwa maana hiyo ukiruhusu dhambi wewe mwenyewe kwa makusudi jua wazi kuwa
huwezi kumwona Mungu wala kupokea Baraka kutoka kwake.
Kwa maana hiyo muombe Roho mtakatifu akukumbushe  dhambi ulizozifanya  aidha wakati unajua au hujui,ili kwamba uweze
kufanya  matengenezo ya maisha yako ili
uweze kujenga mahusiano mema na Mungu baba ambaye neno linasema kuwa ni mwema
wa yote lakini pia ni mwingi wa rehema,na huwanyeshea mvua walimao na
wasiolima,kwa maana hiyo hana ubaguzi wa mtu, ukitubu yeye ni mwema anasamehe
na kusahau kabisa.Basi msihi roho mtakatifu aliyeko ndani yako aendelee kufanya
mabadiliko ndani yako na Yesu mwenyewe aweze kukaa kwako milele.
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12
