UPONYAJI NA NGUVU ZA MUNGU ZASHUKA KAWE PENTECOSTAL CHURCH(KPC)

Mchungaji Elly Boto kushoto na Mwinjilist Daniel wakiombea habasha kwa ajili ya sadaka  ya shukrani
Maisha ya ushindi leo tulikuwepo Kawe Pentecostal Church (KPC) kwa mchungaji Elly Boto ambapo MUNGU alijidhihirisha kwa matendo yake makuu, Watu walitoa shuhuda ambazo MUNGU amewatendea ambapo mmoja katika hao alisema amefaulu mtihani na anaingia mwaka wa pili katika masomo yake ya Digrii katika chuo cha IFM, amesema wakati anafanya mitihani alikuwa kwenye mazingira magumu sana ila maombi tu ya kanisani hapo ndio yamemuokoa na kufeli hivyo anamshukuru sana MUNGU. Mwingine ameshuhudia jinsi ambavyo amerudishia kiwanja chake ambacho aliporwa na watu na mahakama imeamuru alipwe fidia, Mwingine amesema kwamba maombi ya watu wa MUNGU mahali hapo yamesaidia sana maana MUNGU amemlinda mwaka mzima na licha ya vikwazo vyote lakini BWANA YESU amemshindia. MUNGU aibariki sana huduma ya mchungaji huyu na ambaye pia anawatangazia wakati wa Dar es salaamu na maeneo ya jirani kwamba jumapili ijayo kutakuwa na ibaada maalum ya kumshukuru MUNGU kwa ulinzi wake kwa mwaka mzima kwa waumini wote na wote ambao watapenda kujumuika na kanisa , Ndugu popote ulipo na kama unahitaji maombezi kwa njia ya simu au unahitaji ushauri wowote unaweza kuwasiliana na Mchungaji Elly Boto kwa namba  0719640642 au 0752965812 au unaweza kuwasiliana na mchungaji msaidizi Paulo kwa namba 0657361222 pia kama unapenda kuchangia huduma hiyo ili injili iwafikie watu maelfu zaidi unaweza kutuma sadaka yako kwa namba zao watumishi waha au kwa namba hii ya blog hii 0714252292 na sadaka hiyo itapelekwa kanisani na MUNGU atakubariki sana pia kama utapenda kutoa sadaka ya shukrani kwa MUNGU kupitia madhabahu ya kanisa la Kawe Pentecostal Church( KPC)  tuma kwa namba zao au kwa  kwa namba ya blog hii 0714252292. Sadaka hii itakuwa mtetezi wako katika mwaka ujao (Matendo 10:3-4). Zifuatazo ni baadhi ya picha katika ibaada ya leo.
 
kipindi cha kusifu na kuabudu



ni furaha kwa YESU

KWAYA YA WATOTO WAKIIMBA


Kutoka kulia Mwinjilisti Daniel, katikati ni Mchungaji Elly Boto na anayefuata ni Mtumishi Paul







Mapepo yakiwatoka watu


Nguvu ya MUNGU ikiwafungua watu kutoka kwenye minyororo ya shetani

Nguvu ya MUNGU ikiwa imeshuka

Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments