 |
Mgeni rasmi, Mh. William Lukuvi. ©Wikipedia |
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, huyu ni William
Lukuvi, ambaye hatimaye ametangazwa kuwa mgeni rasmi wa tamasha la
Krismasi la mwaka 2013, ambapo nyota Solly Mahlangu ataongoza jahazi la
waimbaji kushusha uwepo wa Mungu.
Wageni waalikwa wpo wa kutosha, mabalozi, viongozi wa kisiasa na wengineo wengi watakuwepo.
Akizungumza kwenye studio za WAPO Radio FM, mkurugenzi wa Msama
Promotions, Alex Msama amesema kuwa vyombo vitaingizwa tarehe 21 na
kisha siku mbili za kufunga na pia baada ya hapo ni majaribio - huku saa
mbili asubuhi tarehe 25 vyombo vitakuwa hewani tayari, kwa jukwaa
ambalo limetoka Nairobi, huku tiketi zikichapwa nchini Marekani, na
kufikia saa nne asubuhi milango itakuwa wazi kwa ajili ya tamasha kuanza
saa sita mchana. Tiketi zitapatikana kwa 5,000 za kawaida na viti
maalumu kwa shilingi 10,000 ambayo imegawanyika mara mbili, huku watoto
ikiwa 2,000.
 |
almanusura kijana wa Meru akose zawadi, hapa akiitafakari zawadi ya ushindi. |
 |
Mkurugenzi wa Kapmuni ya Msama Promotions ambaye anaandaa tamasha la Krismasi 2013.
|
 |
by
Gospel Kitaa
Katibu wa kamati ya maandalizi ya tamasha la Krismasi. Ai Lizer. | | |
| | |
Comments