WAZIRI MWANDOSYA AMJULIA HALI PADRI MWANG'AMBA ALIYEMWAGIWA TINDIKALI


Professa Mark Mwandosya akiwa na Father Mwang'amba wodini alipomtembelea nchini India. ©Issamichuzi.blogspot.com.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais mheshimiwa Mark Mwandosya amemtembelea ili kumjulia hali paroko Anselmo Mwang'amba wa parokia ya Mpendae kanisa katoliki Zanzibar aliyelazwa katika hospitali ya Apollo nchini India akipatiwa matibabu baada ya kumwagiwa tindikali na watu wasiofahamika visiwani Zanzibar mapema mwaka huu.

Paroko huyo ambaye mwili wake uliharibika kutokana na tindikali hiyo, alipelekwa nchini India na kanisa lake kwaajili ya kupatiwa matibabu zaidi kutokana na tukio la kumwagiwa tindikali ambalo watanzania wenye kuipenda na kuitakia amani nchi yao walichukizwa sana na kutaka mamlaka husika kuwatafuta wahusika ili wawajibishwe kwa mujibu wa sheria

Paroko wa Parokia ya Roho Mtakatifu Mpendae Zanzibar, akisaidiwa na Frateri, Richard Haki kupumzika kitandani baada ya kuzungumza na waandishi katika katika Wodi ya Kibasila iliyopo katika Hosipitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijni Dar es Salaam, kabla hajasafirishwa kuelekea nchini India kwa matibabu. Picha Salim Shao

Comments