AINA NNE ZA KUSIKILIZA!

 Na Mchungaji Peter Mitimingi
1. Kusikiliza kwa Kumkubali Mtu (Appreciative Listening)
a. Unamwangalia mtu kwa mtazamo wanje na unam“Judge” kama utamsikiliza au la.
b. Madereva Taxi wengi Humangalia mtu kwa nje akiwa amevaa vizuri kapendeza wanamgombania kumbe mfukoni hana kitu. Aliye vaa hovyo hovyo hakuna anae shughulika naye kumbe huyo mwenye matope katoka Melerani ndio mwenye pesa.
c. Jifunze kumkubali mtu kama alivyo na kumsikiliza. Huwezi kujua ndani yake amebeba nini.

2. Kusikiliza kwa Hisia (Empathic Listening)
Listening to provide emotional support for a listen.
a. Unamsikiliza mzungumzaji na huku ukionyesha hisia zako
• Mfano:
Mshangao Mungu wangu!!!!
Che,che,che,che
Mh! Mh!mh!
Ah! Ah! Ah!
Wow!
b. Mahali kwenye kuonyesha Mshangao onyesha kushangaa
c. Mahali kwenye kuonyesha Kufurahi furahi
d. Mahali kwenye kuonyesha huzuni huzunika ikiwezekana kutoa machozi toa. Labda mtu anakuelezea jinsi mpendwa wake alivyokufa onyesha kusikitika hat kulia.
e. Yohana 11:35
“Yesu akalia Machozi”
3. Kusikiliza kwa kuelewa (Comprehensive Listening)
a. Unasikiliza ili kuelewa hasa nini ambacho mzungumzaji anakimaanisha.
b. Mfano:
Ulisema nani ndiye aliyesababisha!
Samahani hapo unamaanisha nini unaposema hivyo?
Naomba urudie tena hiyo sentesi uliyoisema.
c. Ikiwezekana andika yale ambayo anayaeleza.
4. Kusikiliza kwa Kukosoa (Critical Listening)
a. Unasikiliza kwa makini lakini si kwa lengo la kelewa hasa, bali kwa lengo la kutafuta makosa ya kuyakosoa.
b. Unaweza ukaacha mema 90 yaliyosemwa na ukan’gan’gana kutafuta makosa mawili ya kuyakosoa kutoka kwa mzungumzaji.
c. Mawazo yako yote yapo katika kutafuta mabaya tu nan a sio mema yoyote katika yale ambayo mtu anayaelezea.

NEXT TIME
SABABU NNE KWANINI WATU WENGI HAWAJUI KUSIKILIZA



Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments